Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? Sehemu Ya 47


Deo aliporudi nyumbani kwake alikuwa amesha chekecha akili vya kutosha kabisa na kumuaga mkewe.
"Kesho nasafiri"
"Mbona gafla hivyo? Na unaenda wapi?"
"Kwani kila siku ninaposafiri huwa naenda wapi? Wewe tambua tu kwamba kesho nasafiri, acha nikatulize akili yangu kwanza"
"Naomba unisamehe mume wangu, ila mimi sikukusudia hili"
"Sikia Joy, sikuwa mpumbavu kumkubali huyu mtoto toka alipokuwa mdogo ingawa kosa lilishatendeka. Sikuwa mjinga kumlea kama damu yangu na kumpa chochote alichotaka. Na sikuwa mjinga kwa kutokumjua huyo mwanaume ambaye ni baba yake mzazi kwani ilinisaidia kuepusha mambo mengi kwenye fikra yangu. Na sio mpumbavu kwasasa kukuaga kuwa nasafiri ili nikapumzishe akili yangu mbali na nyumbani. Nawe hunabudi kuniacha niende"
Mama wa Sabrina akamtazama mumewe kwa masikitiko ila hakuwa na namna zaidi ya kumruhusu tu.
Na kulipokucha Deo akasafiri na kumuacha Sabrina na mama yake.

Sakina bado alitamani kumwambia mama wa Sabrina kuhusu yule mganga ila alikuwa akijifikiria kuwa ataweza kumwambia kwa namna gani ukizingatia mama wa Sabrina hayapendi mambo ya kishirikina, kwahiyo alikuwa anaenda tu kwakina Sabrina na kubaki na hoja yake moyoni.
Siku hiyo aliporudi kwake alikuwa na mawazo zaidi kuhusu Sabrina, Dorry naye alikuwa karibu kumpa moyo.
"Mama, hakuna namna hapo. Ni kumuomba Mungu tu"
"Tatizo hujui Dorry, kama mama Sabrina angekuwa muelewa basi mi ningeshamueleza na Sabrina angekuwa ameshapona."
"Kwakweli watu huwa wanabadilika jamani, yani imeshindikana kabisa kwa Sam kuja kumuona mamdogo Sabrina mmh!"
"Ni ushirikina tu mwanangu"
"Mi nitajaribu kufanya kitu mama"
"Kitu gani?"
"Subiri tu utaona mama"
Sakina akaachana na maneno ya Dorry kwani aliona hayana faida kwake.

Sam naye akiwa nyumbani kwake, alijaribu kuchekecha mambo katika akili yake ila hakuweza kuelewa.
Akakumbuka siku anaenda kumuona Sabrina hospitali na kupigiwa simu na Neema kuwa anaumwa sana.
"Mbona sikumkuta na ugonjwa wowote? Na kwanini sijisikii kwenda kumuona Sabrina? Kwani nina matatizo gani mimi siku hizi?"
Bado Sam hakujielewa ila alijiona kumjali zaidi Neema kuliko kumjali Sabrina na ubaya zaidi ni kule kutokutamani kumuona Sabrina kabisa.

Baada ya wiki moja, mama wa Sabrina akashangazwa na hali ya mguu wa mtoto wake kwani siku hiyo waliamka na kukuta ule mguu umevimba sana halafu unavuja maji.
"Jamani huo mguu tena vipi mwanangu?"
"Hata mimi sielewi mama, nimeshangaa tu leo umevimba zaidi na huku unavuja maji"
Mama hakujua cha kufanya zaidi ya kumpigia simu dereva wa gari za kukodi ili wampeleke hospitali.
Muda kidogo kabla dereva hajafika, alikuja Sakina na yeye pia kushangaa ile hali ya mguu wa Sabrina.
"Sasa mama umeamua nini juu ya hilo?"
"Niamue nini mwanangu na hali kama hiyo. Nimempigia simu dereva atupeleke hospitali"
"Hapana mama tusiende hospitali"
"Kheee Sakina, tusiende hospitali halafu twende wapi?"
"Samahani mama ila Sabrina huo ugonjwa wake ni wa kurogwa"
"Kwahiyo twende wapi?"
"Twende kwa mtaalamu mama, ila samahani kwa hilo"
"Yani Sakina akili yako mmh! Badala useme twende kwenye maombi unasema twende kwa waganga jamani loh! Twende tu hospitali"
Sakina hakuwa na la kuongezea zaidi ya kukubaliana na hali halisi tu.
Alipofika dereva wakapanda gari kwa lengo la kwenda hospitali sasa.

Walipofika hospitali moja kwa moja Sabrina akapelekwa kwa daktari.
Akampima na kila kitu kisha kuwaita mama wa Sabrina na Sakina awaeleze kwa kifupi ilivyokuwa.
Sakina akamuelezea kila kitu, lakini bado daktari alitikisa kichwa kana kwamba anautafuta ule ugonjwa kwa akili.
Kisha akawaandikia dawa,
"Leo akanywe dawa hizi, ila kesho hali ikiendelea hivi itabidi tumchome sindano"
Mama wa Sabrina akadakia,
"Kwanini usingemchoma leo sindano daktari?"
"Kila kitu huenda kwa mpangilio mama, acha leo akatumie hizi dawa"
Ikabidi wakubali pale na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwa kutumia gari ile ile ya kukodi.

Walifika nyumbani kisha Sakina akawaacha hapo na kurudi nyumbani kwake huku akiwa na masikitiko makubwa sana.
Kama kawaida, akenda kutuliza mawazo yake kwa kushauriana na Dorry kidogo.
"Hata sijui nifanyeje, yani ingekuwa amri yangu au ningekuwa na uwezo basi ningetafuta hao ng'ombe mwenyewe ili Sabrina apone. Kwakweli namuhurumia sana. Lazima Sabrina atakuwa ametupiwa jini tu"
"Sasa hapo utafanyaje mama?"
"Sijui, ila ninachojua ni kuwa jini halipatani na sindano. Na kwa mtindo huu limejidhihirisha wazi kwa kumvimbisha Sabrina mguu, basi hapa inawezekana Sabrina akichomwa sindano tutampoteza kabisa. Jamani Sabrina mdogo wangu namuhurumia sana, yote hiyo wanamtesa kwa wivu wa kuolewa na mume tajiri"
Sakina alikuwa akisikitika tu huku akijaribu kutafakari cha kufanya.
Muda kidogo wakapigiwa simu na Jeff na kumfanya Sakina atabasamu kidogo kwani ni kitambo hajapata mawasiliano na mwanae.
"Mama, mbona mpo kimya sana! Na vipi mamdogo nae anaendeleaje?"
Sakina akaamua kumueleza kidogo Jeff kuhusu hali ya Sabrina kwani alijua kama akimueleza kiundani zaidi atamchanganya.
"Sam naye anasemaje kuhusu hilo maana naye simpati kabisa"
"Yani mwanangu ya huku yaache tu maana hali ni mbaya. Huyo Sam hata hajui huku Sabrina anaendeleaje"
Jeff akaongea na mama yake pale na mwisho wa siku akaikata ile simu.

Usiku wa siku hiyo Dorry akiwa chumbani, akashangaa kuona namba mpya ikimpigia.
Akashtuka sana kwavile ilikuwa ni namba ya nchi za nje.
Akaipokea kwa mashaka, akashangaa kusikia ni sauti ya Jeff na kujiuliza kuwa kwanini Jeff ameamua kumpigia siku hiyo.
Sauti ilikuwa ni ya Jeff ila Dorry alishangaa huyo Jeff akiongea kwa ustaarabu na kwa maelekezo zaidi.
Yani hadi ile simu inakatika bado Dorry alikuwa akishangaa ila alikumbuka maelekezo yote aliyopewa kwenye simu.

Kulipokucha asubuhi na mapema, Dorry aliamka na kujiandaa kisha akamuaga mama mkwe wake.
"Wapi asubuhi yote hii?"
"Kuna mahari naenda mama"
"Khee ndio asubuhi yote hii? Ila mi hutonikuta ukirudi hapa nitakuwa kwakina Sabrina"
Basi Dorry akaaga pale na kuondoka hadi alipoelekezwa.
Ilikuwa ni barabarani tu akingoja gari ya Sam ipite.
Na ilipopita tu akaisimamisha na kupanda.
"Khee Dorry, nimeshangaa kukuona hapo barabarani"
"Sawa, ila nilikuwa nakungoja wewe Sam. Tena chonde chonde nakuomba twende ukamuone Sabrina"
"Muda huu? Acha niende ofisini kwanza, nitakuja badae kumuona"
"Mi nakuomba Sam, wewe ni kama kaka yangu. Nakuomba twende muda huu na wala sitakusumbua tena"
Sam akaona ni vyema amridhishe tu huyu Dorry kwa kwenda kumuona huyo Sabrina.

Sakina naye alifika nyumbani kwakina Sabrina na kumkuta mama Sabrina alishamtoa Sabrina nje wakisubiri gari waende hospitali.
"Jamani, mguu ndio umevimba zaidi"
Sakina alisikitika na kutoa machozi kwani alimuhurumia Sabrina kwa ile mimba na hali aliyonayo kwa kipindi hicho.
Walikaa pale nje wakimngoja dereva tax, na muda kidogo dereva akafika na kuwafanya waanze kumkongoja Sabrina kuelekea kwenye gari.
Muda huo Sam na Dorry nao wakafika, Dorry akamuomba Sam ashuke kisha akawaita wakina Sabrina.
Sam na Dorry wakaanza kuelekea waliko kwani walisimama baada ya kuitwa, Sam akamshangaa Sabrina kwa jinsi mguu ulivyovimba na kuuliza kwa mshangao.
"Imekuwaje tena?"
Hakuna aliyemjibu, Sam akasogea na kumshika bega Sabrina kamavile mtu anayehitaji jibu.
Ila kabla ya yeyote kati yao kusema chochote, wakashangaa kumuona Sam akianguka chini na kuwa kimya kabisa.


Hakuna aliyemjibu, Sam akasogea na kumshika
bega Sabrina kamavile mtu anayehitaji jibu.
Ila kabla ya yeyote kati yao kusema chochote,
wakashangaa kumuona Sam akianguka chini na
kuwa kimya kabisa.
Ikawa heka heka nyingine sasa ya kumuinua Sam pale chini huku wakitaka wampakize kwenye gari na wampeleke hospitali.
Ila Dorry akawapinga,
"Hapana, msimpeleke hospitali"
Mama wa Sabrina akauliza kwa mshangao,
"Kwanini?!"
"Mimi ndio nimekuja nae, tusaidiane kumuingiza ndani ila tusimpeleke hospitali."
Ikabidi wasaidiane nae pale na kumuingiza ndani, kisha kumlaza sehemu nzuri kidogo ambapo Dorry aliwataka wakamlaze kitandani kwa Sabrina nao wakafanya hivyo ila kila mmoja kati yao alimshangaa Dorry hata yule dereva wa gari za kukodi aliamua kuondoka tu ili kukwepa lingine la kuzuka.
Wote kwa wakati huo walisahau kabisa kuhusu mguu wa Sabrina na kukazana kujadili kuhusu Sam.

Muda kidogo wakamuona Sam akitoka chumbani, naye alifika na kuwashangaa.
"Jamani, nimefikaje hapa?"
Wote wakashtuka kwa kumuangalia Sam na hakuna aliyemjibu, Sam naye aliwatazama kwa zamu kisha akaangalia saa yake ya mkononi na kuona wazi kuwa muda umeenda sana.
"Aah! Mpaka muda huu, ni kitu gani kimenileta huku? Ngoja niende ofisini kwanza nikitoka nitapita ili mniambie vizuri"
Sam akatoka na kuondoka zake.
Dorry naye akainuka na kumuacha pale Sakina, Sabrina na mama Sabrina kisha yeye akaondoka.
Wote walibaki wameduwaa na kumfanya mama Sabrina aulize tena,
"Ni kitu gani hiki jamani?"
"Hata sielewi"
Wakapata na wazo la kuangalia mguu wa Sabrina, nao ulionekana kuwa mzima kabisa yani haukuvimba wala kuwa na jeraha lolote.
"Hivi haya ni maajabu, miujiza au ni kitu gani jamani? Au naota mimi mama Sabrina jamani"
Kila mmoja hakuelewa kabisa, ikabidi Sakina awaage pale na kwenda nyumbani kwake ili akamuulize vizuri Dorry kwani hata yeye alibaki njiapanda.
Kwahiyo pale akabaki Sabrina na mama yake,
"Vipi na maumivu ya mguu sasa?"
"Siyasikii kabisa mama, kwani ni mambo gani yanatendeka haya? Ila namshukuru Mungu nimepona huu mguu maana ulikuwa unaniuma balaa"
"Pole sana, ila tutajua tu kisa na mkasa. Yani hadi sasa naona kamavile naota hata siamini haya yaliyotokea jamani"
Hakuna aliyeamini ila kila mmoja aliamua kuendelea na mambo mengine tu.

Sakina alifika nyumbani kwake na kumkuta Dorry akiwa amejiinamia tu.
Akamfata kwa karibu na kumuuliza,
"Hivi imekuwaje Dorry, hebu niambie maana sielewi kabisa"
"Hata mimi sielewi ila sina budi kukueleza mama"
Sakina akatulia kwa makini akingoja kuelezwa na Dorry, naye akamueleza yote toka alivyopigiwa simu na maelekezo aliyopewa,
"Kwahiyo yote niliyoyafanya leo ni maelekezo niliyopewa na Jeff kwenye simu"
"Unauhakika ni Jeff amekupa maelekezo hayo?"
"Ndio ni Jeff mama"
"Mmh! Mbona hayo maelekezo kamavile umepewa na mganga wa kienyeji? Hivi Jeff mwanangu na mambo hayo ya utaalamu wapi na wapi?"
"Kama huamini mama mpigie simu umsikie mwenyewe, maana hata mimi nimeshangaa ukizingatia haya mambo ni mageni kabisa kwangu"
Sakina alijikuta akiguna na kuchukua simu yake, akaangalia salio kwanza alipoona lipo la kutosha akampigia simu mwanae kumuuliza.
Baada ya salamu akaamua kumuuliza,
"Mwanangu kwani siku hizi umekuwa mganga wa kienyeji?"
"Kwanini mama?"
"Ila twashukuru sababu mgonjwa amepona, ila niambie ulivyo sasa mwanangu?"
"Kwani vipi mama? Mbona sikuelewi?"
"Jana umempigia simu Dorry hapa, umempa maelekezo ya kiganga kabisa ila yamesaidia"
"Nimempigia simu Dorry? Kwanza Dorry yupi?"
"Si huyu Dorry mchumba wako mwanangu"
"Kwanza kabisa mama huyo Dorry sio mchumba wangu, pili sijampigia simu kwani hata namba yake sina nilishaifutaga zamani sana"
"Khee wewe Jeff una wazimu au? Dorry sio mchumba wako wakati ana mimba yako hapa!"
Dorry naye akaishiwa pozi kwa yale mazungumzo kwani aliona wazi mamamkwe wake akizidi kuharibu kwa kusema kuwa Dorry ana mimba.
Muda huo Jeff naye alikuwa akimshangaa mama yake.
"Mama jamani mama yangu, sijawahi kuwa na mahusiano na huyo Dorry. Kwakifupi sio mchumba wangu wala mpenzi wangu. Sasa hiyo mimba unayosema imetokea wapi jamani mama....."
Simu ikakatika kwani vocha nayo ilishakata.
Sakina akamuangalia Dorry na kujikuta wakitazamana,
"Mbona maajabu haya, Jeff anasema hajakupigia simu na wala haitambui hiyo....."
Kabla hajamaliza, Dorry alidakia kwa kushika simu yake,
"Kama hajanipigia mbona namba yake ipo humu kwenye simu kuwa alinipigia"
Huku akijaribu kuipekua ili amuonyeshe Sakina.
Cha kushangaza ile namba hakuiona na kumfanya ajishangae mwenyewe.
"Sasa namba imeenda wapi?"
"Unaniuliza mimi wakati simu yako unayo mwenyewe muda wote"
"Ndio, ila namba siioni humu. Mbona mauzauza haya!!"
Dorry hakuelewa kabisa, akaingia chumbani na kutoka nje na begi lake kisha kumuaga mama mkwe wake.
"Sasa unaenda wapi?"
"Naenda nyumbani mama, acha nikatafakari haya nyumbani kwetu kwamaana nashindwa kuelewa kabisa mama yangu yani sielewi kitu hapa."
"Sasa kuondoka ndio suluhisho jamani?"
"Mama acha tu, akili ikikaa sawa nitarudi hata kesho"
Dorry aliogopa kuulizwa tena kuhusu ile mimba yake na kuamua kuondoka kwanza.
Sakina nae akaona kwake hapakaliki na kuamua kwenda kwakina Sabrina kwa muda.

Sam akiwa ofisini, wafanyakazi wake walimshangaa kwani alionekana ni mtu mwenye mawazo halafu shati lake lilionekana kuwa na vumbi baadhi ya sehemu ila waliogopa kumuuliza.
Muda kidogo Sam akafatwa na Rose yule rafiki wa Neema,
"Shemeji, kuna tatizo kidogo nakuomba twende tafadhari"
"Wapi tena?"
"Nyumbani kwa Neema"
Sam aliamua kutoka pale ofisini na kuondoka na Rose hadi nyumbani kwa Neema ambapo walimkuta Neema akiwa hoi kabisa.
"Sasa mtu anaumwa hivyo unashindwa kumpeleka hospitali kweli Rose? Kwanini sasa?"
"Tatizo sio ugonjwa wa hospitali"
"Ni ugonjwa wa wapi sasa?"
"Subiri"
Rose akachukua kikombe na kuweka maji, alikuwa na karatasi mkononi akafungua na kutoa kitu kama ungaunga akachanganya na maji, kisha akagawa yale maji kwenye vikombe viwili.
"Shemeji, hii ni dawa inatakiwa unywe wewe na Neema, yani kunywa kwako hii dawa ndio kuokoa maisha ya Neema."
"Mmh! Mambo gani haya? Ndio wanaita ushirikina au ni vitu gani hivi?"
"Sio ushirikina shemeji, kuna bibi yetu ndio kanipa hii dawa. Yani Neema anaumwa hivi sababu ya kukupenda wewe sana shemeji"
"Mmh hebu mpe kwanza Neema hiyo dawa halafu mi ndio nitakunywa"
Rose akampa Neema ile dawa na kuinywa yote huku akiumwa sana, kisha Sam naye akainywa ile dawa na muda huo huo Neema akawa mzima.
Sam alijikuta akistaajabu ila alishindwa kuuliza kuwa kwanini inakuwa vile.
Walikaa pale hadi jioni kabisa kisha Sam akawaaga na kuondoka zake.

Sakina nae akaenda kumueleza mama wa Sabrina alichoambiwa na Dorry na jinsi alivyojibiwa na Jeff baada ya kumuuliza.
"Khee sasa mbona haya ni mauzauza?"
"Ni mauzauza kweli mmh!"
"Ila bora mwanangu ni mzima, mengine tumuachie Mungu tu. Kwahiyo Dorry yuko wapi?"
"Mmh kaondoka hata sijui kwanini? Labda anaogopa mauzauza"
"Mmh mnanikumbusha mauzauza ya wifi yangu Sabrina leo"
"Yalikuwaje kwani"
"Mmh ni historia ndefu na sipendi ijirudie kwenye maisha yetu maana yalikuwa majanga tena majanga haswaaa"
Sakina akatamani kuyajua hayo majanga ila kwavile mama wa Sabrina aliyakatishia njiani hakuweza kumuuliza zaidi.
Ila bado aliendelea kuwepo pale kwakina Sabrina,
"Yani leo sijisikii hata kurudi kwangu"
"Kwanini uhangaike Sakina? Vyumba vipo hapa vya kutosha tu, leo lala hapa kwetu"
Wakakubaliana hivyo.

Sam alipofika nyumbani kwake akajaribu kutafakari matukio bila ya kupata jibu la aina yoyote.
"Niliondoka hapa asubuhi nikielekea kazini. Sasa niliendaje kwakina Sabrina? Na iweje nikajikuta nimelala mule ndani kwao? Mbona sielewi, eti Neema kaumwa yani dawa ninywe mimi halafu apone yeye. Mbona nimekuwa mpumbavu kiasi hiki! Kwani nina matatizo gani?"
Sam alijihoji bila ya kupata jibu la maswali yake kabisa.
Na kuamua kulala tu.

Kesho yake, Neema na rafiki yake Rose waliamua kujadiliana juu ya hali halisi.
"Kwakweli Rose nimechoka yani nimechoka kabisa, ipo siku nitakufa najiona jamani"
"Unachokaje mapema hivyo Neema? Bado hata hatujavuna matunda unachokaje kwa mfano? Dawa ni kupata mimba ya Sam tu halafu ndio tuachane na hizi dawa sababu lazima atalea mtoto wake"
"Hivi kwa unavyomuona huyu Sam kuna hata dalili ya kulala nae kweli? Mi naona tunamtesa bure tu Sabrina. Ila mi nimechoka shoga yangu, maana huyo Sam akienda tu kuonana na huyo Sabrina mi nakuwa hoi. Unajua nitakufa mimi bila sababu!"
"Maji tumeshayavulia nguo shoga yangu hatunabudi kuyaoga tu. Hapa hakuna la kufanya, ndiomana mimi nilipoona jana hali imekuchachia nikaamua kukimbilia kwa yule mganga ndio akanipa ile dawa"
"Kwahiyo ndio ilitakiwa tunywe wote mi na Sam?"
"Ndio, unadhani ningempa peke yake angekubali? Yule mganga kiboko. Ila leo hebu twende akatueleze vizuri maana kama mambo yenyewe haya wakionana tu unakuwa hoi hata mimi yatanishinda"
Wakakubaliana pale kuwa waende wote kwa mganga ili awaelekeze vizuri.
Kisha wakajiandaa na kuondoka.

Walifika kwa yule mtaalamu wao ili waweze kupata maelezo zaidi.
Yule mganga aliwaangalia kwa jicho kali sana,
"Jamani hapa tunacheza na moto, jana nilikupa tu dawa kuepusha ya mbali ila cha msingi mnatakiwa kumdhibiti yule mwanaume asiende kabisa kule. Jitahidi umuwekee ile dawa tena kwenye chakula"
"Ila kwanini unasema tunacheza na moto?"
"Kuna kitu nakiona kwa huyu dada tunayemfatilia, nadhani kuna kitu kinamlinda na ndio kilichopelekea yule kijana aende na alipofika kauvuta ugonjwa wote na kuja kwako"
Yule mganga akawaonyesha kwenye kioo chake ambapo ilionekana kama video.
Walimuona Sam alipofika kwakina Sabrina na kumgusa Sabrina kisha akaanguka na kumpeleka chumbani.
Neema na Rose walishangaa na kuduwaa,
"Khee ni wachawi nini?"
"Bado sijajua ila kuna kitu nitachunguza ili nijue ilikuwaje mpaka kuwa hivi. Ila kwasasa hivi mkawe makini sana."
Walimalizana nae pale na kuamua kuondoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakiwa njiani walijidadisi sana,
"Ila huyu mganga ni noma, unajua Sabrina hatakiwi kabisa kukanyaga nyumbani kwa Sam ndiomana akang'atwa na nyoka!"
"Naelewa hilo Rose, ila kama hawa wakina Sabrina ni wachawi hapa kazi ipo sababu itakuwa tunavutana kwa kumpa madawa Sam"
Rose akacheka,
"Ndiomana wanaume wanakuwaga vichaa jamani. Ila usiwe na shaka Neema sababu Sabrina pale alipo bado hana kumbukumbu"
Walijikuta wakimuongelea Sabrina njia nzima.
Nyuma yao alikuwepo Francis na kuwaita, nao wakashtuka sana kwani hawakutegemea uwepo wa mtu anayewafahamu nyuma yao.
"Mbona mmeshtuka hivyo?"
Wakacheka na kusalimiana nae.
"Nimewasikia kama mkimtaja Sabrina, je ni huyu ninayemjua mimi au ni Sabrina yupi?"
"Francis, dunia hii ni kubwa sana na Sabrina huyupo mmoja duniani. Halafu tumtaje huyo Sabrina unayemjua wewe kwa lipi? Hapa ni mambo yetu tu"
Francis hakutaka kubishana na hawa wadada kwahiyo alichokifanya ni kuwaaga na kuendelea na safari yake tu.

Sakina bado alikuwa nyumbani kwa wakina Sabrina kwa siku hiyo pia kwani hakujisikia kabisa kurudi nyumbani kwake ukizingatia akirudi anakuwa peke yake nyumba nzima.
Akiwa pale akapigiwa simu na mtoto wake Jeff kwa siku hiyo ambapo Jeff alikuwa na hoja yake ile ile ya jana.
"Yani mama kama huyo Dorry alikwambia mimi nilimpigia simu ujue ni muongo tena muongo hafai"
"Ila Jeff mwanangu sikuelewi na hata sijui umepatwa na nini huko."
"Sijapatwa na chochote mama ila ndio hivyo. Na wala sina mahusiano na huyo msichana"
"Na ile mimba je?"
"Mimba? Mimba gani? Mama huyo msichana atakuchanganya akili tu mi simtambui. Ila nimemkumbuka sana mamdogo Sabrina naomba umsalimie sana"
"Nipo nae hapa, ngoja nimpe umsalimie"
"Wow, itakuwa vizuri sana maana simpati hewani siku hizi"
Sakina akachukua ile simu na kumkabidhi Sabrina ili aongee na Jeff.
Sabrina aliichukua ile simu na kuanza kuongea, mara gafla akaanza kulia na kumfanya Sakina ashtuke.


Sakina akachukua ile simu na kumkabidhi Sabrina
ili aongee na Jeff.
Sabrina aliichukua ile simu na kuanza kuongea,
mara gafla akaanza kulia na kumfanya Sakina
ashtuke.
Sakina akazidi kumshangaa Sabrina na kumuuliza kinachomliza kwa muda huo.
Sabrina hakujibu kwanza na kumkabidhi Sakina ile simu kisha Sakina akazungumza na Jeff,
"Vipi wewe? Mbona umemuacha mamako mdogo na kilio?"
"Hata mi nashangaa anacholilia, hebu mbembeleze mama. Tutaongea muda mwingine"
Jeff akaikata ile simu, Sakina bado akamshangaa Sabrina na kumuuliza tena kwani muda huu alikuwa kanyamaza.
"Kwani ulikuwa unalia nini Sabrina?"
"Kuna maneno kaniambia mazuri sana, ila imeniuma sababu simkumbuki"
"Maneno gani hayo?"
"Alikuwa ananiambia hivi mmh...."
Sabrina akaguna na kufikiria kidogo ila kabla hajasema cha zaidi, ile simu ya Sakina ikapigwa tena na Jeff kisha Sakina akaipokea,
"Naomba kuongea tena na mamdogo"
Sakina akampa Sabrina ile simu ambapo ilionekana kama mwanzo kuwa Jeff ndio aliyetawala maongezi yote kwani Sabrina alionekana kuitikia tu ila safari hii hakutoa machozi kama mwanzo hadi alipoikata ile simu ambapo Sakina alimuangalia na kumuuliza tena.
"Saizi kakwambia nini? Na mwanzo alikwambia nini hadi ukalia?"
"Kweli huyu ni mwanao?"
"Ndio ni mwanangu"
"Mwanao kabisa kabisa wa kumzaa?"
"Ndio, kwani tatizo ni nini Sabrina?"
"Mmh basi tuyaache tu kama yalivyo"
"Tuyaache vipi wakati ulikuwa unalia hapa mwanzoni?"
"Nililia kwavile sijamkumbuka"
"Mmh kwani alikwambia maneno gani?"
Sabrina akaamua kubadilisha mada yani ingawa hakuwa na kumbukumbu yoyote ila kwa maneno aliyoambiwa na Jeff aliweza kuelewa kitu na kuweza kubadilisha mada ingawa bado alimuacha Sakina akiwa na maswali ya kila namna.

Bado Dorry alikuwa na mawazo juu ya mtu aliyempigia simu na kuanza kumuelekeza cha kufanya kumuokoa Sabrina na jinsi Sam alivyozimia na Sabrina kupona.
"Mbona sielewi jamani ni kitu gani hiki? Maana aliyenipigia simu ni Jeff kabisa yule halafu kesho yake ananikana kwa mama yake halafu huku kwangu eti namba haipo tena"
Akashtuka kidogo na kujiuliza tena,
"Hivi huyu Jeff ni mtu wa aina gani? Mmh wanaume wengine tunawapendaga usikute sio binadamu wa kawaida. Napata mashaka juu yake jamani."
Aliwaza sana Dorry na kuogopa hata kurudi nyumbani kwa Sakina.
Muda kidogo akapigiwa na Sakina, swali lilikuwa ni atarudi lini.
"Kwakweli mama sitarudi kwasasa hivi ila nitarudi tu"
"Uje bwana mkwe wangu, njoo hata twende kwa mtaalamu tuone alikuwa ni nani"
Ikabidi Dorry ampe moyo tu kuwa ataenda ingawa hakuwa na mpango huo kwa kipindi hicho.

Sabrina alikuwa akimsikiliza kwa makini Sakina na ile simu aliyokuwa akizungumza nayo ili aweze kumuuliza anayoyahisi yeye.
Alipomaliza tu kuongea ndipo alipoanza kumuuliza,
"Kwani huyo binti ni nani?"
"Ni yule binti niliyekuwa nakaanae pale kwangu, ni mkwe wangu yule anaiwa Dorry"
"Mkwe wako kivipi?"
"Ni mchumba wa mwanangu na ana mimba yake tayari"
"Mwanao yupi?"
"Khee Sabrina, mi nina mtoto mmoja tu. Sina mtoto mwingine kabisa"
"Kwahiyo ndio huyu huyu niliyeongea nae mimi muda ule?"
"Ndio ni Jeff, mtoto wangu ni yeye tu"
Sabrina akaonekana kama kufikiria kitu.
Sakina akamuuliza,
"Kwanini umeniuliza maswali yote hayo?"
"Nilitaka kuelewa tu, halafu nipe namba za simu za huyo mwanao ili badae niongee nae"
Sakina hakuelewa lengo la Sabrina ni nini ingawa alimpatia ile namba ya Jeff na muda huo Sabrina akawa anajisachi,
"Kheee hivi sina simu eeh!"
"Inamaana siku zote hizi hujui kama huna simu Sabrina?"
"Ila si nilikuwa nayo zamani?"
"Kweli wewe umeshachanganyikiwa jamani yani hujui chochote kweli! Pole sana, simu ulikuwa nayo ndio ila uliiacha kule kwako, mi nakumbuka vizuri"
Sabrina alimuangalia tu Sakina kwani hakuwa na kumbukumbu yoyote juu ya kilichomtokea.
Sakina nae aliongea nao pale kisha kuwaaga na kurudi nyumbani kwake kwani alishapakumbuka tayari.

Maisha kwa upande wa Neema yalikuwa ni burudani ila alikosa jambo moja tu muhimu kutoka kwa Sam ambaye kwa kipindi hiko alikuwa ni mwanaume aliyempa chochote alichotaka.
Aliamua kukaa na kujadiliana na rafiki yake ili wajue cha kufanya,
"Unajua Rose, mwenzio huyu Sam simuelewi kabisa. Inamaana Sabrina ndio alikuwa mwanamke pekee kwake?"
"Kwani wewe unataka nini shoga yangu ikiwa pesa unapewa?"
"Nahitaji mapenzi, nini maana ya kuwa na pesa? Nahitaji mapenzi, napenda nami nizae na Sam ili anithamini kama ambavyo anamthamini Sabrina hata kama dawa zikiisha"
"Basi vumilia shoga yangu, tutamuandalia tego huyo Sam"
Wakakubaliana pale kumuandalia mtego Sam ili aweze kuwa na Neema kimwili na lengo kubwa la Neema ni kupata mimba ya Sam ili kumfanya Sam ampende sana.

Sam hakupata hata wazo la kuwasiliana tena na ndugu wa Sabrina hata Jeff ambaye alimpeleka mwenyewe kusoma.
Ila siku hiyo Jeff alimpigia simu Sam na baada ya salamu alimuuliza swali moja,
"Unampenda Sabrina?"
Sam akamshangaa Jeff kwa swali hilo naye akamuuliza,
"Kwani wewe unataka nini?"
"Nataka jibu tu"
"Simpendi tena Sabrina"
"Unampenda nani sasa?"
"Nampenda Neema hata nashangaa kwanini nimechelewa kutambua hili"
"Sawa, nashukuru kwa jibu lako"
Jeff akaikata ile simu ambapo Sam bado alikuwa na mashaka kuwa kwanini Jeff ampigie simu na kumuuliza maswali kama yale.
Ila kwavile hakuwa na upendo tena juu ya Sabrina aliamua kupuuzia kile kitendo na kujisemea,
"Mwache Sabrina akawe na wanaume wanaombaka hovyo na kumzalisha na kumuacha"
Kidogo akashtuka na kukumbuka kitu ila aliamua kukipuuzia kwani aliona hakina umuhimu kwake ukizingatia anampenda sana Neema kwa kipindi hiki.

Inaendeleeaah


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.