Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? Sehemu Ya 48
Sakina akiwa nyumbani kwake usiku, akapigiwa simu na mwanae huku akimuomba mama yake aongee na Sabrina,
"Haitawezekana Jeff, saizi nipo nyumbani kwani Leo nimeamua kulala kwangu"
"Sawa mama, ila shida yangu ilikuwa ni ya muhimu sana kwa maisha ya mamdogo"
"Hakuna tatizo, nitaenda kesho asubuhi halafu nipigie ili nikupe uongee nae kwahiyo usijali mwanangu"
Basi Jeff akaagana na mama yake pale na kukata ile simu.
Sabrina akiwa nyumbani kwao kwa usiku huo, alijaribu kuvuta kumbukumbu za huyo mtu wa kuitwa Jeff kwani hakuwa na kumbukumbu yoyote juu yake ila alimtafakari sana kwa maneno ambayo alimwambia na pia akamtafakari Dorry binti ambaye ametajiwa na Sakina.
"Hivi huyu Jeff ni wa aina gani? Eti ni mtoto wa Sakina, iweje kwenye simu aniambie kuwa ananipenda sana. Na kwanini aseme huyu mtoto wangu ni wake pia? Na mbona Sakina kasema kuwa huyo Dorry anamimba ya huyo Jeff? Na mbona alinikataza kumueleza chochote Sakina sababu ni mama yake? Kama Sakina ni mama yake halafu mimi kwa Sakina ni kama mtu na mdogo wake, iweje niwe na mahusiano na mwanae?"
Sabrina alipiga piga kichwa chake ili aone kama kuna kumbukumbu yoyote atapata ila hakukumbuka chochote kile na kuamua kulala tu.
Asubuhi na mapema, Sakina akapigiwa tena simu na mwanae kwa lengo lile lile la kuongea na Sabrina.
Kwahiyo Sakina akaona ni vyema aende kwa wakina Sabrina kwani hakujua huo ujumbe unaumuhimu gani mpaka Jeff kuukazania kwa kiasi kile.
Aliondoka kwake na kwenda kwa wakina Sabrina, na alimkuta akicheza cheza na mtoto wake.
Wakasalimiana pale na baada ya salamu tu muda huo huo akapigiwa simu na Jeff akitaka kuongea na Sabrina kama kawaida, wakati Sakina anamkabidhi Sabrina ile simu Sabrina aliikataa kwa kumuuliza,
"Nani huyo tena?"
"Ni mwanangu anataka kuongea na wewe"
"Mwanao yupi? Yule yule?"
"Ndio ni Jeff"
"Kama ni yeye sitaki kuongea nae"
Sakina akajitahidi kumwambia Sabrina apokee ile simu ila bado Sabrina alikataa kabisa kuongea na ile simu na wala Sakina hakujua ni kwanini Sabrina kagoma kuongea na ile simu,
"Jeff, mamako mdogo kakataa kabisa kuongea na wewe"
"Kwanini mama?"
"Mi sijui kwakweli"
"Basi hakuna tatizo"
Kisha akaikata ile simu.
Sakina akamsogelea Sabrina na kumuuliza sababu ya kukataa kuongea na Jeff,
"Sitaki mazoea naye tu"
"Hutaki mazoea nae kivipi Sabrina jamani? Huyu Jeff ni mwanangu na wewe ni kama mwanao pia, sasa hutaki mazoea nae kivipi?"
"Sitaki tu"
Sakina hakuweza kumuelewa Sabrina anachomaanisha ila a limshangaa tu kwajinsi anavyokataa kuzungumza na Jeff kwa madai kuwa hataki mazoea naye.
Sakina aliamua kumuaga na kurudi nyumbani kwake.
Sabrina alibaki mwenyewe na mwanae, na sababu kubwa iliyomfanya agome kuongea na Jeff ni kuwa hataki kuweka mambo anayoona kumtatiza ukizingatia kashapoteza kumbukumbu.
"Nisije siku nikaropoka mambo ya kuniumbua kwakweli maana hakuna ninachokumbuka hapa. Natakiwa kuwa mpole tu na mambo yanayonichanganya niwe mbali nayo kwanza"
Sabrina aliwaza hayo na kuendelea kucheza na mwanae kwani hakukumbuka chochote kuhusu maisha yake.
Ila mama yake alipokuja karibu aliamua kumuuliza,
"Hivi mama, sisi hatuna ndugu yeyote zaidi ya baba? Mimi wadogo zangu wako wapi?"
Mama yake akasikitika tu kwani ndugu zao asilimia kubwa ni watu wasiojali.
"Mdogo wako yupo, na kaka yako pia. Watakuja tu hata usijali, ndugu nao tunao watakuja tu. Ila yule kaka yako James si alikuja hujamkumbuka?"
"Nimemkumbuka, ila mbona hajaja tena?"
"Atakuja tu"
"Na huyo mume wangu?"
"Achana na khabari zake kwanza ila atakuja tu, tushukuru Mungu unaendelea njema kwa sasa"
Wakiwa wanaendelea na maongezi pale akafika James kaka wa Sabrina na kumkuta pale mama yake na dada yake ambapo Joy hakutaka hata kuzungumza na mwanae huyo na kumfanya ainuke na kwenda ndani.
James hakupenda kile kitendo cha mama yake kuondoka pale.
Akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Uwe makini na wewe huenda huyu sio baba yako pia"
Sabrina akamshangaa tu James kwani hakumuelewa anaongelea kitu gani kisha James akaondoka.
James alipotoka pale alipita hospitali kumuangalia baba yake ambapo alimkuta akiendelea vizuri kiasi na daktari akamwambia kuwa kuna uwezekano wa kuruhusiwa kesho.
"Itakuwa vizuri baba ukiruhusiwa"
"Hata sitamani kurudi nyumbani, ni bora hata ningekufa tu"
James akajitahidi pale kumbembeleza na kumwambia maneno ya kumfariji ili kumtia moyo.
Kisha akamuaga na kuelekea nyumbani kwake.
James akiwa nyumbani kwake bado hakuwa na muafaka juu ya mke wake kwani tayari alishakuwa dada yake.
"Niambie ukweli mume wangu, wewe husemi chochote na baba nae hasemi kwanini?"
"Unajua nini Joy! Mimi ni kaka yako"
Joy akashangaa na kuuliza kwa makini,
"Kaka yangu? Kaka yangu kivipi?"
Ingawa James alikaa kimya kwa siku zote hizi ila hakuwa na jinsi zaidi ya kumueleza Joy ukweli tu juu ya hali halisi ya undugu wao na kumfanya Joy ashangae maradufu.
"Bado sijakuelewa James, sijakuelewa kabisa. Inamaana mimi na wewe baba yetu ni mmoja?"
"Ndio ni mmoja Joy, kwahiyo mi na wewe ni kaka na dada"
"Haiwezekani, mi nakataa"
"Joy, hata mi sikuamini hivyo hivyo mwanzoni"
"Kwahiyo itakuwaje sasa?"
"Sijui, ila ndio hivyo mi na wewe ni kaka na dada. Kwahiyo tutangoja maamuzi ya baba"
Joy hakutaka kuelewa kabisa kuwa maamuzi ya baba yao yatakuwa ni nini, akifikiria kwajinsi vile anavyopendana na James.
Akimfikiria yule mtoto wao mdogo na yule aliyepo tumboni.
"Haiwezekani, nasema haiwezekani"
Aliona kama nyumba yao inawaka moto kwenye akili zake na hakuweza tena kulala mule ndani kwake na mumewe ambaye ni kaka yake, akaamua kuondoka na kwenda kwao kabisa ili kutuliza mawazo.
Sam akiwa kazini, alipigiwa simu na Neema kuwa anashida naye sana na angependa waonane.
Sam hakuweza kukataa kwavile tayari alikuwa anampenda Neema.
Na alipotoka kazini kakwe tu alienda moja kwa moja kwa Neema na kuwakuta ndani akiwa pamoja na Rose.
Wakasalimiana pale na kuanza mazungumzo kidogo,
"Duh hatukujua kama shemeji utawahi kiasi hiki"
Neema nae akadakia,
"Mi sikujua kama atakuja moja kwa moja huku kwangu tena saizi"
Sam akawashangaa na kuwauliza,
"Kwani tatizo ni nini? Mimi kuwahi au jambo gani?"
"Hakuna tatizo shemeji"
Kisha Rose na mwenzie Neema wakainuka huku Neema akidai kuwa anamsindikiza kidogo Rose na kumuacha Sam mule ndani akiwangoja.
Baada ya muda mfupi akafika kijana mmoja ambaye Sam hakumjua na kumuuliza Sam,
"Wewe ni nani?"
Sam akamshangaa huyu kijana na kumuuliza,
"Kwani vipi?"
"Jibu swali wewe ni nani?"
Sam akatikisa kichwa kwani hakumuelewa huyu kijana anamaana gani.
"Yani huyu malaya ananiambia nisije kumbe kuna malaya mwenzie humu ndani!"
Kisha yule kijana akampiga Sam ngumi ya sura, na kumfanya Sam atokwe na damu mdomoni.
Baada ya muda mfupi akafika kijana mmoja
ambaye Sam hakumjua na kumuuliza Sam,
"Wewe ni nani?"
Sam akamshangaa huyu kijana na kumuuliza,
"Kwani vipi?"
"Jibu swali wewe ni nani?"
Sam akatikisa kichwa kwani hakumuelewa huyu
kijana anamaana gani.
"Yani huyu malaya ananiambia nisije kumbe kuna
malaya mwenzie humu ndani!"
Kisha yule kijana akampiga Sam ngumi ya sura, na
kumfanya Sam atokwe na damu mdomoni.
Huyu kijana hakuachia hapo, akamuinua Sam na kumpiga kwa ngumi nyingine na kumfanya Sam azidi kutoka na damu mdomoni.
Sam akapatwa na hasira zaidi kwa ule upuuzi aliofanyiwa na yule kijana na kuamua kutoa bastora yake anayotembea nayo kila mahari kama ulinzi wake.
Yule kijana kuona bastora akaona hali mbaya na kutaka kukimbia, ila kabla hajakimbia Sam akamfyatua na risasi moja ya begani na kumfanya aanguke chini akiugulia.
Na Sam kuona vile akatoka nje na kumuacha yule kijana pale sebleni kisha yeye kuondoka zake.
Neema na Rose waliokuwa wamesimama njiani wakiongea, wakashangaa kuona gari ya Sam ikiwapita na kuishia, wakajikuta wakiulizana.
"Vipi tena mbona Sam ameondoka bila kutuaga? Au dawa zimeanza kuisha nguvu?"
"Na ubaya kaondoka kabla ya kukamilisha mpango wetu"
"Au lile chizi lako limekuja Neema?"
"Sijui ila nilimzuia asije"
Wakakubaliana Neema ampigie simu Sam ili amuulize kuwa kwanini kaondoka bila kuaga ila simu haikupokelewa kabisa.
"Mmh hebu turudi nyumbani nisije nikaibiwa bure"
Waliamua kurudi tena nyumbani kwa Neema, walishangaa walipoingia ndani na kukuta damu imetapakaa pale chini na kumkuta yule kijana akiwa chini.
Neema alimfata pale chini huku akilia,
"Jamani John wangu nini hiki jamani"
"Neema, tufanye utaratibu wa kumpeleka hospitali. Kulia hapatasaidia kwa sasa"
Ikabidi waende kuomba msaada wa kumuwaisha yule John hospitali.
Walifika hospitali na kumuwahisha kwa daktari ambaye mwanzoni alikuwa akikataa kumuhudumia ili wakalete PF3 kwani aligundua kama amepigwa na risasi, ila baada ya kumuomba sana aliamua kumuhudumia yule kijana kwani alikuwa mahututi.
Neema na Rose walikuwa hawajielewi huku wakijiuliza tu wao wenyewe kuwa kwanini Sam ampige yule John risasi.
"Kumbe Sam anatembea na bastora?"
"Sasa tunauhakika gani kama aliyempiga ni Sam?"
"Atakuwa ni yeye tu na ndiomana ameondoka bila kuaga"
Daktari naye akawaita katika ofisi yake,
"Tumefanikiwa kumtoa huyu kijana risasi, ila hali yake si nzuri. Mnatakiwa mkaripoti polisi ili huyu mtu ashughulikiwe, mi mwenyewe nimewasaidia tu ingawa hairuhusiwi kumuhudumia mtu wa hivi bila kibali"
Kisha akawataka kumueleza ilivyokuwa, ila hata wao hawakuelewa chochote kwavile hakuna aliyeona tukio.
"Haya, nendeni mkatoe taarifa polisi"
Wakaongea kidogo pale na kuondoka.
Njiani wakafikiria kuhusu kutoa taarifa polisi,
"Inamaana Sam atakamatwa, na akishakamatwa je?"
"Si atafungwa, bora afungwe sababu ni muuaji. Mtu gani anatembea na bastora?"
"Akifungwa na mpango wetu itakuwaje? Ila huyu John naye ni mpumbavu. Mi nimeliambia vizuri tu kuwa lisije ila cha kushangaza limekuja na kuzua mabalaa kwetu sasa. Hela zote zimenitoka mie, uhuni huu umeniponza jamani"
Kwahiyo wakahairisha safari ya kwenda polisi na kuamua kurudi nyumbani, na kwavile muda ulishaenda, waliamua kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Rose na kulala huko.
Sam hakukaa nyumbani kwake kwani alijua wazi kuwa kashafanya kosa, kwahiyo akamtafuta mwanasheria wake na kuongea nae vizuri ili kama kitatokea chochote ajue jinsi gani atamsaidia.
Na kesho yake alfajiri na mapema akasafiri na kuelekea kwao Arusha.
Joy mke wa James, alikuwa kwao akilia tu muda wote na kumfanya mama yake amshangae zaidi na hata alipomuuliza hakuweza kujibu na kumuacha apumzike kwanza.
Ila kulipokucha, aliamua kumuuliza tena mwanae juu ya jambo linalomtatiza,
"Mama, sitaki kuachana na mume wangu. Kwanini iwe hivi kwetu jamani mama?"
"Kwani imekuwaje mwanangu? Na kwanini uachane na mumeo wakati mmefunga ndoa takatifu kabisa!"
"Roho inaniuma sana mama, sitaki kukubali wala kuamini hili. Kwanini iwe hivi jamani kwanini mama, kwanini sisi?"
Bado ilikuwa ngumu kumuelewa kitu anacholalamikia au anachomaanisha.
Wakati huo, James naye alikuwa hospitali kumuona baba yao ambaye alikuwa amepewa ruhusa ya kurudi nyumbani siku hiyo.
James ndio akachukua jukumu la kurudi nae kwani mama wa Joy hakuonekana hapo hospitali kwa muda huo.
Mama wa Joy alikazana nyumbani kumuuliza mwanae kitu kinachomtatiza na kumfanya awe katika hali ile.
"Mama, James ni kaka yangu"
"Kaka yako? Kivipi?"
James na baba yao nao wakawa wamewasili muda ule ule na kumfanya mama wa Joy kwenda kuwapokea na kuwakaribisha ndani.
Baba wa Joy bado hakujielewa kwani hakujua hata anaanzaje kumueleza mke wake ila aliona ni vyema tu atoe dukuduku lake la moyoni na kumwambia ukweli kuhusu James kuwa ni mtoto wake na kumfanya mama wa Joy abaki na mshangao na kuelewa sababu ya Joy kulia na kutamka yale maneno,
"Ndiomana Joy analia! Nimeelewa sasa"
Baba wa Joy naye akaongea kwa masikitiko sana,
"Najiona sina thamani kwenye maisha haya. Itakuwaje kwa hawa wanangu? Nawezaje kuwatazama wakiishi pamoja kama mke na mume? Bora ningekufa tu kuepusha hii aibu"
Joy naye akasogea karibu ya James huku wakisikiliza hoja za wazazi wao ila muda wote Joy alionekana kutoa machozi, huku mama wa Joy akiendelea kumbembeleza mumewe,
"Usiseme hivyo mume wangu, bado tunakuhitaji sana katika maisha yetu. Mi nimekusamehe mume wangu"
"Na watoto je? Itakuwaje kuhusu James na Joy? Maana mi sitaweza kuvumilia kuwaona kama mke na mume ilihali baba yao ni mie"
Joy aliongea kwa masikitiko pia,
"Utakuwa hujatutendea haki baba, mi siwezi kuishi bila James. Kumbuka tuna mtoto tayari na sasa nina mimba yake"
Joy alionekana kuumia zaidi kuhusu hili kwani hakufikiria kuwa ipo siku atatengana na James tena kwa namna ya undugu, aliendelea kuongea kwa uchungu sana,
"Siko tayari kumuona James akiwa na mwanamke mwingine, siko tayari kabisa nampenda sana"
Ikabidi mama yake asogee karibu na mwanae akimbembeleza.
Muda huo baba yao nae akamtazama James ili kusikia maamuzi ya James pia,
"Nakusikiliza nawe mwanangu"
"Mimi hata sijielewi hapa nilipo sababu sidhani kama itatokea siku nikampenda mwanamke mwingine kama ninavyompenda Joy. Yani nampenda sana, yani sijui hata......."
Gafla baba yao akaanguka na kupoteza fahamu, ikabidi wamuwahishe hospitali.
Neema na Rose hawakutaka tena kurudi hospitali kwa kuogopa kudaiwa kibali cha polisi, walichofanya ni kuwapigia simu ndugu wa John na kuwajulisha kuwa ndugu yao amelazwa bila ya wao kujulikana.
"Kwahiyo hatutaenda kumuona huyu John"
"Bora tusiende kuliko kuanza uchunguzi na polisi, mambo yashatokea ndiobasi tena"
"Ila wewe Rose unaongea hivyo sababu John hakuhusu, ila mimi nampenda sana sema tamaa tu hii ndio inaniponza"
"Na wewe Neema acha zako hizo, huyu John kajitakia mwenyewe na alivyomkorofi nina uhakika alianzisha fujo humu ndiomana Sam akamfanya vile"
"Ila kumbuka, John akitoka hospitali hata sisi tutadakwa. Bora twende kwa Sam tukubaliane cha kufanya"
Ikabidi waondoke pale na kuelekea nyumbani kwa Sam.
Sakina kama kawaida yake, alienda tena kwakina Sabrina ili kumshawishi amkumbuke mumewe.
"Labda twende tena Sabrina, unaweza ukarejesha kumbukumbu zako"
"Kule nilipong'atwa na nyoka siwezi kwenda tena, labda uende mwenyewe"
"Sabrina, jihurumie mdogo wangu. Hapo una mtoto mdogo na mimba nyingine halafu ulee mwenyewe, tafadhari twende urejeshe kumbukumbu zako. Kwanini uteseke wakati watoto wako baba yao yupo!"
"Kwanza sina uhakika kama yule ni baba yao"
Sakina akashtuka na kumuuliza kwa makini,
"Unamaana gani Sabrina?"
Sabrina naye akajishtukia kwa maneno yake,
"Aaah sina maana yoyote ile"
Sakina hakumuelewa Sabrina ingawa alimbembeleza na kuchoka kuwa waende nyumbani kwa Sam ila Sabrina alikataa kabisa na kumfanya Sakina kuamua kwenda kuendelea na shughuli zake zingine.
Wakina Neema walipofika kwa Sam wakashangaa kumkosa, na mlinzi aliwajibu kuwa Sam amesafiri na kuwafanya kuwa na mawazo zaidi.
Wakaenda pembeni kujadiliana,
"Sasa itakuwaje? Au dawa zimeisha nguvu kweli?"
"Mi siamini kama dawa zimeisha nguvu, na kama zingekuwa zimeisha nguvu basi angekuwa ameenda kwa Sabrina na sio kusafiri. Hapa tufanye kitu tu"
"Kitu gani tufanye?"
"Hebu jaribu kuwasiliana nae na kumuomba uende alipo, akikubali tukamilishe ule mpango wetu"
Neema akakubali na kumtafuta Sam hewani ambapo Sam aliipokea ile simu na kuongea nae kwani tayari alishamkumbuka pia, hata ombi la Neema kwenda alipo aliliona kuwa ni wazo jema kwani hakuweza kupingana na moyo wake kuwa kwa kipindi hicho ni anampenda sana Neema.
Walipomaliza kuongea na simu, Neema akamwambia Rose ile khabari njema na kuifurahia kisha kuondoka na kurudi nyumbani kwa Rose kwa lengo la kujiandaa na hiyo safari.
Sam akiwa Arusha alijikuta akiwaza mambo mengi sana, akakumbuka siku ile ya kwanza kumuona Sabrina.
Akakumbuka alivyompenda na kujitoa kwaajili yake,
"Kwanini leo simpendi tena? Kwanini Sabrina amenitoka kwenye moyo wangu kabla ya kumwambia ukweli halisi kuhusu mimi? Ni nani nitakayeweza kumwambia siri yangu? Neema! Hapana, nampenda ila siwezi kumwambia hili. Na je ataweza kunivumilia kama Sabrina alivyofanya?"
Akawaza sana Sam bila ya jibu ila ukweli ulibaki pale kuwa alimpenda sana Sabrina ingawa dawa zimemfanya amchukie.
Joy alibaki nyumbani wakati wamemkimbiza baba yao hospitali kwani alikuwa kama ameshachanganyikiwa vile.
Alikaa mahali peke yake na hakutaka kuongea na mtu yeyote.
Alikuwepo mdogo wake ambaye hakuelewa ni kitu gani kinaendelea kwenye ile familia yao kwa kipindi hiko, alijaribu kwenda kukaa na dada yake ili ajue tatizo ila alimuona kuwa ameshachanganyikiwa na Joy hakutaka kabisa kuongea na mdogo wake huyo.
Na kwajinsi yule mdogo wake alipoona Joy anazidi kuchanganyikiwa, akaamua kumpigia simu mama yao ili aweze kurudi nyumbani kwa haraka.
Mama wa Joy aliamua kurudi nyumbani na kumuacha James hospitali akiendelea kungoja maelezo ya daktari kuhusu baba yao.
Alipofika nyumbani moja kwa moja akaelekea alipo Joy na kumkuta akitaka kunywa vidonge kwa lengo la kujiua.
Mama yake alishtuka sana,
"Wee Joy mwanangu jamani Joy mama nini mwanangu? Kwanini ujiue?"
"Sitaki kuishi tena mama, bora nife"
"Usifanye hivyo mwanangu, unanitesa mimi mama yako"
"Sipo tayari kuachana na James, bora nife mama"
Joy alikuwa akilia sana kama kawaida, mama yake alielewa kuwa ile mimba ndio iliyomfanya Joy awe na uchungu kiasi kile.
"Huwezi kuachana na James mwanangu, ondoa shaka juu ya hilo"
"Baba hawezi kukubali mama, bora mimi nife"
Mama wa Joy akasikitika,
" Yani nyie watu mnanifanya nitoe siri niliyoitunza miaka yote hii"
"Siri gani?"
"Nisamehe mwanangu, ila ukweli ni kuwa huyu sio baba yako mzazi"
Joy akashangaa sana na ikawa ni ngumu kumuelewa mama yake.
Neema alijiandaa kwa safari na kupanga mambo yote na Rose.
"Jitahidi safari hii ufanikiwe, maana hiyo dawa lazima ujengewe ghorofa shoga yangu"
Wakafurahiana pale na muda ulipofika, wakaelekea uwanja wa ndege kwa lengo la kusafiri kwa Neema.
Neema alifika Arusha na kupokelewa na Sam kama walivyowasiliana, na moja kwa moja akampeleka hotelini ambako Neema alifurahi sana kufikishwa hotelini.
"Twende nikakutembeze kidogo uone mandhari ya Arusha"
"Hapana, muda ushaenda na pia mi ningependa tukae tupate vinywaji na kuongea kidogo"
"Sawa hakuna tatizo, twende tukakae pale baa tunywe basi"
"Hapana, mi nataka tunywe humu ndani"
Sam hakupinga kitu na kumpigia simu muhudumu kisha kumuagiza vinywaji wanavyotaka.
Muhudumu naye hakuchelewa na kuwaletea vinywaji.
Kwavile Neema alikuwa na hamu sana na ile dawa ya kumfanyia Sam ndiomana alikuwa anaharakisha ili asije kusahau.
"Sam, samahani"
"Bila samahani"
"Naomba kanichumie jani la mti wowote nje, kuna kitu nataka kukuonyesha"
Sam hakupinga kitu na kutoka nje, Neema akatumia muda huo kuweka dawa kwenye kinywaji cha Sam.
Muda kidogo Sam akarudi bila ya jani wala nini na kumfanya Neema amshangae,
"Mbona hujaniletea jani?"
Sam akacheka na kusema,
"Nimekuona ulichokuwa unafanya, haya kwa usalama wako kunywa mwenyewe hicho kinywaji"
Sam akatoa bastora na kumlengeshea Neema.
Muda kidogo Sam akarudi bila ya jani wala nini na
kumfanya Neema amshangae,
"Mbona hujaniletea jani?"
Sam akacheka na kusema,
"Nimekuona ulichokuwa unafanya, haya kwa
usalama wako kunywa mwenyewe hicho kinywaji"
Sam akatoa bastora na kumlengeshea Neema.
Neema akatetemeka sana huku ameishika ile glasi na kujikuta akiibwaga chini na kuvunjika, ila Sam akatabasamu tu kisha akairudishia bastora yake na kukaa kwenye kitanda.
Neema alisimama vile vile akitetemeka, Sam akamuangalia na kumwambia
"Unapofanya kitu uwe unajiamini, njoo ukae hapa"
Neema alikuwa akitetemeka tu na kusitasita, ila Sam akamshika mkono na kumfanya akae.
Kisha akaanza kumuhoji,
"Sasa Neema ulikuwa unaniwekea dawa ili iweje?"
"Naomba unisamehe Sam, sikuwa na nia mbaya"
"Ulikuwa na nia gani gani?"
"Samahani, naomba unisamehe. Nia yangu ilikuwa ni kulala na wewe, na ile dawa ilikuwa ni kukufanya ulale"
Sam akacheka na kutikisa kichwa, Neema wewe ni mpumbavu kwakweli. Umeshindwa kufanya chochote cha kuniwezesha mimi kulala hadi uniwekee dawa? Mi nakupenda tayari kwahiyo sina cha kupinga kwako, na una bahati nakupenda maana vinginevyo ungebaki historia. Haya unataka kulala na mimi kiaje?"
Neema akaangalia chini na kujibu,
"Kimapenzi"
"Kwahiyo unataka kusex na mimi?"
Neema akaitikia kwa kichwa, Sam akatabasamu kisha akatulia akitafakari kitu kidogo.
"Ila huwa sipendi kufanya hivyo na mwanamke nimpendae au niliyemzoea."
"Kwanini Sam, ilihali tunapendana? Tafadhari Sam, nahitaji penzi lako."
"Basi nipe siku mbili nitakupa jibu"
Neema akamshangaa kuwa huyu ni mwanaume wa aina gani huyu ambaye kulala mpaka afikirie? Alikosa jibu na kuamua kungoja jibu baada ya hizo siku mbili.
Siku hiyo Sam alimuacha Neema peke yake na yeye kwenda kulala kwingine.
Neema aliwaza juu ya maamuzi ya Sam kwa usiku wote na kuamua kumpigia simu rafiki yake Rose kwa ushauri.
"Yani na wewe umekubali kusubiri hizo siku mbili?"
"Sasa nifanyaje hapo shoga yangu?"
"Wewe ni mwanamke, fanya kitu. Kumbuka una mimba tayari, sasa utambambikiaje kuwa ni yake? Muwahi sasa, usichelewe"
"Jamani shoga yangu, unanipa mawazo ujue?"
"Mawazo gani? Fanya kitu mpigie simu aje mlale wote, mwambie huwezi kulala mwenyewe. Yani Neema nawe hebu acha upumbavu, umeweza kutembea na wanaume wangapi hadi huyu akushinde? Mwonyeshe makeke yako ukizingatia kukupenda kashakupenda tayari"
Neema akaingiwa akilini na yake maneno ya Rose na kuona wazi kuwa achangamkie hilo wazo mapema.
Alipokata tu ile simu akaanza kumpigia Sam ili kumshawishi akalale nae, huku akijiwazia
"Yani huyu mwanaume sijui ni wa aina gani? Wanaume wenzie huwa wanalazimisha wadada kulala nao, eti yeye ndio nimlazimishe. Mmh ila sikubali hadi aje kulala na mimi"
Akaongea nae kwenye simu na kumwambia kama alivyoambiwa na rafiki yake.
"Kwahiyo nia yako nije tu kulala huko basi!"
"Ndio uje tu kulala na mimi"
"Sawa basi nakuja"
Neema akafurahi na kuona kuwa sasa atimize azma yake aliyopanga na Rose.
Muda kidogo, Sam akafika mule chumbani alipolala Neema na kama ambavyo Neema alipanga, alimkaribisha kwa makeke yote.
Sam akamuangalia tu na kumuuliza,
"Huwezi kulala peke yako?"
"Ndio siwezi, nalalaje peke yangu wakati mpenzi wangu upo?"
"Sawa basi tulale wote"
Sam akapanda pale kitandani na kujilaza, Neema alikuwa akimshangaa tu Sam na kujaribu kumfanyia mambo mbalimbali ya kumshawishi ila Sam hakuonekana kabisa kushawishika, ikabidi Neema amwambie tu tena,
"Tafadhari Sam naomba"
"Unaomba nini Neema?"
"Naomba penzi lako"
Sam akatabasamu na kumjibu,
"Mi siwezi Neema"
"Kumbe Sam hunipendi eeh!"
"Sikupendi kivipi? Nakupenda sana tu ila siwezi kukufanyia hili"
"Basi utakuwa ni mwanaume ambaye hajakamilika"
Neema alijikuta akiropoka na kumfanya Sam achukie,
"Unasema mimi ni mwanaume ambaye sijakamilika? Na nisipofanya hivi na wewe ni kuwa sikupendi?"
Neema akaangalia chini na kumfanya Sam amsogelee na kumkumbatia kisha akamwambia,
"Mi nakupenda sana Neema tena sana na ndiomana sikuweza kukudhuru kwavile nakupenda tena kuliko nilivyokuwa nampenda mke wangu Sabrina. Ila kwavile umesema bila kufanya hivyo itakuwa sikupendi basi mi nitafanya, na kwavile umesema nitakuwa sijakamilika basi mi nitakuonyesha kama ni mwanaume niliyekamilika kabisa ila nilikuwa nakuhurumia kwavile nakupenda"
Neema akatabasamu kwani aliona huo ni muda muafaka wa wao kufurahia mapenzi yao.
Kisha Sam akamtaka Neema kuzima taa ili waweze kukamilisha azma yao.
Inaendeleaah
No comments: