Simulizi: Je Haya ni mapenzi? sehemu ya 49
Nyumbani kwakina Joy bado ilikuwa ni kizungumkuti kwani Joy alishindwa kumuelewa mama yake kabisa kuwa yeye yule sio baba yake kivipi.
Usiku huo James alirudi nyumbani na kuwataarifu kuwa baba yao atarudi kesho yake, ikabidi Joy amfate James na kumueleza alichoambiwa na mama yake,
"Sasa huyu sio baba yako mzazi kivipi?"
"Mama hajaniambia kivipi, ila hata mimi nina maswali najiuliza. Sasa baba yangu mimi ni nani kama sio huyu?"
"Kheee! Ila mbona wamama ni waongo sana. Lazima tumuulize kivipi"
"Mwache, baba akirudi atamuuliza mwenyewe"
Kwasiku hiyo, James alilala kwa amani kidogo ila Joy alijikuta na mawazo juu ya alichoambiwa na mama yake.
Kulipokucha, James alienda hospitali na mama mkwe wake na kuruhusiwa kuondoka na mgonjwa na kurudi nae nyumbani kwani alikuwa na hali nzuri kiasi kwa siku hiyo.
Kwahiyo wakafanya safari ya kurudi nyumbani.
Walipofika nyumbani kama kawaida wakawakuta wengine na Joy pia aliyeenda kumpokea baba yao na kumkaribisha ndani.
Ila baba yao alipoingia ndani tu, hakutaka hata kupoteza muda kwani akawaita tena wote kwa mahojiano yale yale,
"Eeh, mmefikiria nini hadi sasa?"
Joy alikuwa wa kwanza kujibu kwa kumshangaa,
"Khee baba, bado unayo hayo hayo?"
"Nahitaji kujua hitimisho la haya mambo kwanza"
Ikabidi mama wa Joy amuombe mumewe waende kuzungumza wawili kwanza kwani ile khabari alijua wazi Joy anaweza kuropoka na kutawafanya washindwe kupata hitimisho lao, kwahiyo waliamua kwenda chumbani kwaajili ya kuyazungumzia hayo mambo.
Alijadiliana na mumewe ambaye alionekana kutokumuelewa kabisa, alimweleza ukweli kuhusu Joy kuwa si mtoto wake mzazi na ilikuwa ngumu kwa baba Joy kuelewa hili.
Alikuwa akitikisa kichwa tu,
"Hivi nyie wanawake mnamatatizo gani? Mapenzi gani haya? Tumeishi siku zote, miaka yote kumbe Joy sio damu yangu? Ndio kunipenda huku kwa kunidanganya kuhusu mtoto?"
"Naomba unisamehe mume wangu, haikuwa kusudio langu kufanya hivi. Nisamehe sana"
"Na kwanini ufanye hivi? Kwanini unidanganye jamani? Mama Joy, si ni wewe uliyekuwa ukiniambia usiku na mchana kuwa unanipenda sana nisije nikakusaliti? Sasa haya ndio mapenzi uliyokuwa ukiyasema? Kunidanganya kweli? Siwezi kukusamehe kwa hili?"
Mama Joy alionekana kusononeka sana,
"Mbona mi nimekusamehe na unamtoto wa nje jamani?"
"Tena usitake kuniudhi? Umenisamehe mimi kwavile unajijua kuwa unamakosa tayari, na jambo lingine mimi hili si kosa langu ila ni kosa la mwanamke kama wewe mnaopenda kuwanyima watu haki zao kwamadai mpo kwenye mapenzi ya kweli ila kiuhalisia haya si mapenzi mama Joy, si mapenzi kabisa"
Baba Joy alipaniki sana na kuumia moyo wake kwani hakutarajia hili kutoka kwa mkewe.
"Nisamehe mume wangu"
"Niache mama Joy, niache kabisa nifikirie mambo yangu"
Mama Joy akaona ni vyema atoke ili asiendelee kugombana pale na mume wake.
Kwakweli siku hiyo baba Joy hakuweza kulala kwani alijikuta akiwa na mawazo mengi sana.
Aliwaza kipindi cha kukutana na Joyce yani mama wa Sabrina, akakumbuka jinsi alivyokuwa akimpenda ila hakuweza kumwambia kwavile alikuwa ni mke wa mtu tayari.
Akakumbuka jinsi Joyce alivyoonyesha kumjali na kuwa nae karibu ingawa bado moyo wake haukuweza kumwambia wazi Joyce kuwa anampenda ingawa kiuhalisia alikuwa akimpenda sana.
Akakumbuka kipindi alipotembelewa na Joy wakati wa mgonjwa wake na kumuingilia kinguvu bila kujua kile kitendo ndio kilichofanya mimba ya James kutungwa.
Akakumbuka sasa alipokutana na mama Joyce ambaye ndiye mke wake kwa kipindi hiki anayeitwa Lucy na kupendana nae sana, huku huyu Lucy akionekana kuwa na hamu kubwa ya ndoa.
Kipindi hiko naye hakutaka kulaza damu kwani alipenda kuheshimika na kufanya wafanye mipango ya haraka dhidi ya ndoa yao huku akimtunzia mkewe huyu heshima ya kutofanya naye chochote hadi kukamilika kwa ndoa yao.
Akakumbuka mwezi mmoja baada ya ndoa yao akapata khabari njema toka kwa mkewe kuwa ni mjamzito na kuwafanya wafurahi sana.
Na kipindi kilipofika mkewe alipata mtoto wa kike na kuwafanya wafurahi sana huku mkewe akilalamika kuwa amejifungua mtoto huyo kabla ya miezi kufika na kuwafanya wamshukuru sana Mungu kwani mtoto alikuwa salama kabisa.
Ndipo alipoamua kumpa binti yao jina la Joyce kwani alikuwa ni mwanamke aliyempenda sana ingawa mkewe hakutambua hilo.
James aliwaza sana hadi kichwa kumuuma kwa yale mawazo na usingizi kukosekana kabisa hadi panakucha yeye alikuwa macho.
Kwa asubuhi hii Neema alionekana kujiinamia huku akilia sana, alilia hadi kichwa kumuuma.
Muda huu Sam alijaribu hata kumletea kinywaji ili ampunguze zile hasira alizokuwa nazo.
"Niache Sam, bora ungeniambia ukweli"
"Ukweli gani Neema?"
"Ungeniambia kama wewe sio mwanaume wa kawaida"
"Ningekuwa sio mwanaume wa kawaida ungekuwa nami usiku wote? Ungekuwa nami muda huu? Inamaana mimi sio mwanaume wa kawaida ila ni jini au ni kitu gani? Nakupenda sana Neema ila si kwa namna hii ya kutaka kunivunjia heshima"
"Sawa, ila basi mi naomba kuondoka. Acha nirudi zangu"
"Utaondokaje kwa hali hiyo? Tafadhari usiondoke"
"Basi naomba simu niwasiliane na ndugu zangu"
"Tafadhari, usimwambie yeyote kilichotokea baina yangu mimi na wewe. Na hiyo ibaki kuwa siri yako hadi pale nitakapokuruhusu mimi"
Halafu Sam akatoka bila hata ya kumkabidhi Neema simu zake aweze kuwasiliana.
Neema alibaki akilia mule chumbani na kulaumu tamaa yake,
"Tamaa imeniponza mimi, bora ningebaki na John wangu. Tulikuwa tunapendana tu na uzuri alikuwa akinielewa sana, sasa nimejitumbukiza kwenye shimo, kwenye mdomo wa mamba. Nilijua nitafaidi kumbe atanifaidi mimi, nini hatma yangu? Pesa imeniponza Neema mimi."
Hakuweza kuendelea kuwepo mahali pale kwani alijua wazi kuwa hata wahudumu wakiingia pale itakuwa ni jambo la aibu.
Kwahiyo akajiandaa kinyemela na kuondoka kwa machale sana.
Alifanikiwa kutoka nje ya ile hoteli na kukutana na bodaboda kisha akapanda na kuondoka nayo ili hata apate basi lolote la kwenda Dar kwani hakuwa na hali wala hamu ya kuendelea kubaki Arusha.
Muda kidogo Sam akaenda tena kwenye chumba alichomuacha Neema na kushangaa kumkosa.
"Huyu mwanamke ni mpumbavu sana"
Aliwaita wahudumu ili wafanye usafi kwenye kile chumba kisha yeye kujaribu kumfatilia Neema.
"Ila ananilaumu bure tu sababu nilishampa onyo kabla, labda anahisi Sabrina alikuwa akifaidi sana kwangu wakati Sabrina alikuwa ndio dawa yangu ya kusubiria matibabu. Pole yake Neema, nampenda sana ndiomana namuhurumia kwani akisema tu ndio mwisho wa khabari yake"
Sam aliongea mwenyewe huku akiendelea kumfatilia Neema kwa kukisia sehemu aliyoenda.
Neema alipofika stendi akashuka toka kwenye ile bodaboda na kumlipa yule mwenye bodaboda pesa yake.
Wakati Neema anaondoka, yule wa bodaboda akamuita.
"Dada nakuomba mara moja"
Ilibidi Neema arudi pale kwenye bodaboda,
"Samahani dada, umenichafulia bodaboda yangu"
Neema akaangalia pale kwenye kiti na kuona damu.
Aibu ikamjaa, akatoa kitambaa na kufuta kisha akachukua mtandio na kujifunga kwani alijua wazi kuwa lazima amelowa na watu watamshangaa njiani.
Kisha akatafuta sehemu ya mliwato kwenda kujisafisha, huku akitafakari namna atakavyofika mjini kwani akili yake ilishavurugika tayari na alitamani afike ili akamueleze Rose kilichompata na waweze kujadiliana cha kufanya.
Sabrina akiwa kwao bila ya kuwa na wazo lolote la kumkumbusha vitu vya nyuma, akashangaa kuona matone ya damu mbele yake kisha akasikia sauti iliyomwogopesha.
Sabrina akiwa kwao bila ya kuwa na wazo lolote la kumkumbusha vitu vya nyuma, akashangaa kuona matone ya damu mbele yake kisha akasikia sauti iliyomwogopesha.
Sauti ile ilimwambia Sabrina,
"Msaidie huyu dada"
Ila Sabrina hakuelewa chochote zaidi ya kutetemeka tu, kwa bahati alifika Sakina pale nyumbani kwakina Sabrina na kumuona Sabrina kama mtu asiyejielewa.
"Mawazo yatakumaliza mdogo wangu"
Akamuangalia Sakina na kujaribu kuangalia tena yale matone ya damu ila hakuona chochote na kumfanya atikise kichwa tu.
Sakina akaona bora ampe ushauri Sabrina ya kuwa asipende kukaa mahali pamoja kamavile na kumuomba wakatembee kidogo.
Sabrina akakubali kwani hata yeye aliona wazi kuwa kukaa ndio kunamfanya awe na mawazo.
Akaenda kujiandaa kwaajili ya matembezi hayo, kisha wakamuaga pale mama Sabrina na kuanza safari yao kidogo kidogo huku Sakina akiwa amembeba mtoto wa Sabrina.
Wakiwa njiani Sabrina na Sakina, kuna mdada akawafata na kuwasimamisha huku akionekana kumfahamu Sabrina ila kwavile Sabrina hakuwa na kumbukumbu ikawa ni ngumu kwake kumkumbuka huyu dada kabisa ila yule dada alionekana vyema kumfahamu na kumkumbuka Sabrina, kisha kuanza kumuuliza.
"Wewe si ndio mke wa yule bosi Sam?"
Ikabidi Sakina aitikie kwa niaba ya Sabrina,
"Ndio ni yeye, na huyu mgongoni ndiye mtoto wao"
"Kheee makubwa haya, Sam ana mtoto?"
"Ndio, huyu hapa"
"Na huyu dada ana mimba nyingine!!"
Huyu dada alionekana kushangaa sana na kumfanya Sakina nae amuulize kwa mshangao,
"Kwani vipi?"
"Huyu dada hanikumbuki ila mimi niliwahi kuonana nae kwenye baa fulani ambayo bosi Sam alikuwa akiipenda sana, nikatamani kumwambia ukweli kuhusu bosi Sam ila mwenyewe akatokea na kufanya nishindwe kumwambia"
"Ukweli gani huo?"
Sakina aliuliza kwa mshangao sana, na huyu dada nae akajibu kwa mshangao wa kumshangaa Sabrina,
"Yani hata nashangaa hapa kuona huyu dada ana mtoto aliyezaa na bosi Sam na ana mimba nyingine. Labda kama haya maneno walimzushia tu sababu ya hela zake, ila mimi nina rafiki zangu wawili waliokufa nikiwashuhudia sababu ya huyo bosi"
Sakina nae akashangaa,
"Kivipi dada, hebu tueleweshe"
"Yani yule bosi alikuwa akilala na mwanamke sijui anamuwekea vinini maana huyo mwanamke ataingia siku zake maisha yote na anamkataza kusema, na pindi akitaka kusema tu anakufa papo hapo. Rafiki zangu wawili wamekufa nikiwatazama hivi kwa macho yangu ila hawakuweza kusema walichofanyiwa kwani walipotaka tu kusema ikawa mwisho wao. Mara nyingi tumekuwa karibu kuwatahadharisha watu kuhusu huyu bosi, na akaendaga Arusha ili kufuta haya kwanza. Ndio nikashangaa kumuona tena Dar akiwa na huyu dada, ndio siku ile nilitaka kumwambia huyu dada kuwa amchune tu yule bosi ila asikubali kulala nae ila sikufanikiwa kumwambia hayo sababu mwenyewe alitokeza na akanisemea kwa bosi wangu nami nikafukuzwa kazi ndio hadi leo nakuona tena hapa"
Sakina na Sabrina walibaki wakitazamana tu kwani hawakuelewa mbichi wala mbivu, Sabrina akajikuta akiuliza.
"Kama ndio hivyo mbona mimi nina watoto nae sasa?"
"Kwakweli sijui, ila sikuwa na nia mbaya ndugu zangu nilitaka utambue tu azma yangu ya siku ile."
Basi Sakina akaongea nae pale na kumwambia asione Sabrina kuonyesha kuwa hamjui, akamjulisha kuwa Sabrina hana kumbukumbu kwa kipindi hiko.
"Duh pole sana dada, pole sana. Mungu atakusaidia kumbukumbu zako zimerudi, ilimradi umeweza kudumu hivi na bosi Sam ujue unamaisha marefu sana"
Wakaongea nae pale na kuagana nae.
Sabrina hakuelewa kitu ila Sakina nae alijikuta na maswali ya kujiuliza, kisha akamuuliza Sabrina,
"Hivi ulikuwa unalalaje na Sam?"
Sabrina akacheka na kujibu,
"Mi sijui ila nadhani tulikuwa tunalala kawaida tu kama wengine ndiomana tukapata watoto hawa"
"Mmh! Au hayo matatizo wewe hayajakupata ila yamekimbilia kwenye kumbukumbu zako?"
"Mi sijui kwakweli sijui"
"Sabrina, naomba ukubaliane nami kuhusu hili"
"Lipi hilo?"
"Naomba twende kwa mganga akakuangalie matatizo yako"
Sabrina akafikiria kidogo kisha akamjibu,
"Kwa muda huu hapana, acha kwanza turudi nyumbani nikatafakari"
"Sio kwa muda huu bhana, namaanisha hata kesho"
Basi wakakubaliana kurudi nyumbani kwanza.
Neema akafanikiwa kupanda basi la kurudi Dar, na hakutaka kushuka popote hadi walipoingia mjini kwani alijua wazi kuwa atakuwa amechafua pale kwenye kiti.
Walipofika mjini walishuka wote, na yeye akawa wa mwisho kushuka kwa kujifunga mtandio mwingine juu yake.
Alitoka hadi nje ya stendi na kuita bodaboda kisha kuianza safari ya kumpeleka nyumbani kwake.
Neema wa leo hakuwa kama Neema yule wa juzi aliyeondoka kwa shauku na bashasha kwani leo alionekana kujichokea kupita maelezo ya kawaida.
Kwa bahati, alipofika kwake, alimuona rafiki yake Rose.
Alifurahi sana na kumuomba amsaidie kulipa pesa ya ile pikipiki ambapo Rose akaitoa ile pesa, ila Neema aliposhuka tu akatoa mtandio mwingine na kufuta pale alipokuwa amekaa kwenye ile bodaboda.
Kisha akaingia ndani na rafiki yake Rose.
"Vipi Neema mbona hivyo? Kwenye simu hujapatikana wala nini siku nzima ya leo. Na mbona unatoa harufu ya damu? Vipi mimba imetoka au ni nini?"
"Acha tu rafiki yangu, kwanza shukuru Mungu nimefika. Ila jua kwamba umeniponza sana"
"Nimekuponza kivipi?"
"Ngoja nikajisafishe kwanza"
Neema aliinuka pale chini na kuelekea maliwatoni moja kwa moja.
Baba wa Joy hakutaka hata kumuona mkewe kwani na yeye siku hiyo aliondoka kabisa pale nyumbani kwake na hakuna aliyeweza kumfata ili kumzuia kuwa asiende mbali sana.
Alipoondoka pale kwake, akaenda moja kwa moja kwenye ufukwe wa bahari.
Akakaa sehemu moja yenye michanga huku akitazama maji ya bahari yanavyoenda, mbele yake kidogo akamuona mtu anayemfahamu na kujikuta akiamua kumfata.
Mtu huyo alikuwa ni Deo yani baba wa Sabrina ambaye alikuwa amesimama tu akiangalia maji pia.
Akamsogelea na kumsalimia,
"Habari mr. Deo"
"Salama"
Deo alionekana kumshangaa kidogo kwavile hakuwa na mazoea naye,
"Samahani, naitwa James. Nimewahi kuwa mwalimu wa kwaya kwenye kanisa alilokuwa anasali mkeo"
Deo akatikisa kichwa kuashiria kwamba lile jina si geni kwenye masikio yake na wala yule mtu si mgeni pia.
Kisha baba wa Joy alijikuta akimueleza matatizo yake Deo huku akificha ukweli halisi kuwa mke wa Deo pia anahusika kwa hilo.
"Pole sana, wewe ni mwanaume unatakiwa kujikaza. Jifunze jambo moja kwenye akili yako kuwa kitanda hakizai haramu"
"Unamaana gani? Unatambua kuwa James sio mwanao?"
Deo akatabasamu,
"Natambua ndio, mimi ni mwanaume wa pekee sana. Nilikubaliana na hali halisi, tukamlea yule mtoto na kuwapata wengine na hadi leo bado naishi na mke wangu. Nilitambua kuwa haikuwa dhamira yake kunisaliti, dunia ni mzunguko. Unachokifanya leo kwa mwenzio usishange kukutokea wewe miaka ijayo"
"Kwanini unasema hivyo?"
"Stori yako na binti yako ndio inayonifanya niseme hivyo. Huyo binti ni mwanao endelea kumlea vizuri, ulicheza faulo kwa mke wangu na akatokea wa kucheza faulo kwa mkeo pia"
Baba Joy akashtuka sana baada ya kugundua kuwa Deo ameshamgundua.
Akajikuta akimuomba msamaha kwa yale aliyoyatenda miaka ya nyuma iliyopita,
"Nilishakusamehe kitambo sana, na ninampenda mke wangu. Nawe umsamehe mkeo na uendelee kumpenda. Huyo ni wako, wamwenzio si wako. Jali ulichokuwa nacho, epuka kuwafanyia wengine matatizo kwani na wewe yatakugeukia tu siku moja."
Kisha Deo akamuaga James hapo na kuondoka zake.
Baba Joy alijikuta akikosa usemi kabisa na kuona wazi amelipiziwa,
"Ila mbaya wangu ni nani? Je na yeye yatamtokea kama yaliyonitokea mimi? Inamaana siku zote huyu mzee alikuwa anajua kama mimi ndiye mbaya wake?"
Alijihoji sana na kuamua kurudi nyumbani kwake tu.
Rose alikuwa akimngoja Neema kwa hamu ili amwambie kilichojiri na kwanini yupo kwenye hali ile.
Neema alipotoka maliwatoni alienda kukaa moja kwa moja,
"Niambie Neema, umepatwa na nini?"
"Acha tu Rose, sasa nimeamini ule msemo usemao kwamba si kila king'aacho ni dhahabu, vingine ni chupa"
"Unamaanisha nini Neema?"
"Nimetembea na kila dizaini ya mwanaume, weupe, weusi, wanene, wembamba, warefu, wafupi, wakawaida na wote niliwamudu bila tatizo ila safari hii nimekutana na moto tena moto wa jehanamu sijui kama nitapona mimi. Tamaa imeniponza mie Neema."
"Jamani shoga yangu pole, ila nini kimekupata?"
Neema akakumbuka alichoambiwa na Sam kuwa asimwambie mtu yeyote na kujikuta akiendelea kulalamika tu,
"Siwezi kusema ila siku moja nitasema ili wenye tamaa kama mimi waache. Natamani nirudishe siku nyuma ili nisiwe nimeenda kwa mganga na kuchukua ile dawa ya kumteka Sam ambapo badala yake nimejiteka mimi mwenyewe. Najuta mimi Neema"
Ilikuwa ngumu sana kwa Rose kumuelewa rafiki yake huyu na kila alipojaribu kumdadisi bado alionekana kuongea kwa mafumbo tu mwanzo mwisho.
Akaona vyema amshauri kuwa akapumzike kwanza, naye Neema akafata ushauri na kwenda kujilaza kitandani kwake huku akiombea kuwa mambo yote yaliyompata yawe ni ndoto tu ili atakapoamka aanze kujipanga upya kwa maisha haya.
Sam naye alionekana kujutia kwa kitendo alichomfanyia Neema, roho ikamuuma sana.
"Niliapa kutofanya hivi na mwanamke yeyote nimpendaye. Kwanini nimemfanyia Neema? Mbona sikuweza kumfanyia Sabrina mwanamke niliyelala nae na kuamka nae kitanda kimoja kila siku?"
Akatafakari sana na kukosa jibu, ila alimuhurumia Neema kwa kuhofia kutangaza kwa watu kwani akithubutu tu kufanya hivyo itakuwa ni mwisho wake.
Aliona ni vyema na yeye arudi Dar, ila kabla ya kufanya hivyo aliamua kwenda kijijini kwao kwanza kusalimia.
Sabrina akiwa nyumbani kwao akamueleza mama yake vile alivyoshauriwa na Sakina kuhusu kwenda kwa mganga.
"Mwanangu, huyu Sakina muangaliage tu hivyo hivyo. Anapenda sana ushirikina na wala si mtu wa kumsikiliza kwakweli."
"Hata mi nimemshangaa ujue mama, yani yeye kila akiongea na mimi anazungumzia maswala ya uganga tu. Ila mama kuna kitu nataka nikwambie"
"Kitu gani?"
Sabrina akamueleza mama yake kuhusu matone ya damu aliyoyaona na sauti aliyosikia.
"Kheee! Na wewe umeanza mauzauza kama ya shangazi yako? Huyo mdada wa kumsaidia ni mdada gani?"
"Sijui mama, ila ile sauti ilinisisitizia sana kuwa nimsaidie huyo mdada"
"Sasa hayo makubwa, ndio huo ushirikina nisioupenda mimi. Haya sasa ukiamua kwenda kwa huyo mganga sababu ya hayo nendeni ila khabari za waganga mie ndio hata msinishirikishe jamani"
Muda kidogo, Deo yani baba wa Sabrina akawasili na kumfanya mama wa Sabrina kufurahi sana kwa kumuona mumewe kwani tangu aliposafiri ndio siku hiyo alikuwa amerudi.
Baba wa Joy nae alirudi nyumbani kwake na kuwaita Joy na James huku wote wakijiuliza anachotaka kuwaambia.
"Joy na James, nyie wote ni wanangu. Nendeni muendelee kuishi kwa upendo na amani."
Kisha akamuangalia Joy na kumwambia,
"Joy mwanangu, wewe ni mtoto wa kike. Unasiri kubwa ya kizazi chako, kuwa makini mshirikishe mumeo kwa kila jambo maana nyie sasa ni mwili mmoja. Msifichane chochote, James mwanangu mie ni baba yako mzazi ila aliyekulea pia ni baba yako. Jifunze kutoka kwetu, epuka kufanya makosa ya makusudi kwani makosa ya makusudi huwa yanamtindo wa kujirudia. Kuwa makini na maisha yako, mshirikishe mkeo kwa kila kitu huku mkiendelea kumtanguliza Mungu. Yangu ni hayo tu, natumaini ni wengi watajifunza kupitia mimi. Nawapenda sana, na ikumbukwe kuwa kila kitu hutokea kwasababu fulani katika hii dunia"
Alimaliza kuongea pale na kuwapa baraka zake kisha kuwaruhusu warudi kwao.
Neema alishtuka kwenye mida ya saa nne usiku, aliangalia kitanda chake na kukuta shuka lote limejaa damu.
Akapata jibu kuwa lazima mimba yake itakuwa imetoka, na kile kitendo cha damu kumtoka mfululizo toka ametoka Arusha akaona kuna uwezekano wa yeye kupungukiwa damu.
Hivyobasi akaona ni vyema kunapokucha aende hospitali kucheki afya yake, huku akikumbukia alichofanyiwa na Sam kisha machozi kumbubujika tu.
Kulipokucha asubuhi na mapema, Sakina akaenda kwakina Sabrina kwa lengo lile lile la kwenda nae kwa mtaalamu.
Ila leo Sabrina hakupinga na kuamua kumuachia mtoto mama Sabrina kisha wao kwenda kwa mtaalamu.
Walifika kwa mtaalamu na kukuta watu wengi sana na kumfanya Sabrina alalamike.
"Watu wengi hivi? Mi siwezi kusubiri, narudi nyumbani"
"Usijali, ngoja twende kwa mwingine"
Ikabidi waende kwa mtaalamu mwingine.
Na walipofika walikuta ana mtu mmoja ndani, wakasubiri atoke kisha wakaingia wao.
Yule mganga alipowaona akacheka sana na kuwaambia,
"Karibuni sana, nimewaona tokea mbali mkija"
Wakakaa chini na kumsikiliza,
"Nakuona mama umeongozana na mkwe wako, mmekuja kupata ukweli wa mambo"
Neno la mama na mkwe liliwashtua Sabrina na Sakina na kujikuta wakiangaliana tu.
Yule mganga alipowaona akacheka sana na
kuwaambia,
"Karibuni sana, nimewaona tokea mbali mkija"
Wakakaa chini na kumsikiliza,
"Nakuona mama umeongozana na mkwe wako,
mmekuja kupata ukweli wa mambo"
Neno la mama na mkwe liliwashtua Sabrina na
Sakina na kujikuta wakiangaliana tu.
Kisha wakajikuta wakiongea kwa pamoja tena kwa mshangao,
"Mama na mkwe wake!!"
Yule mganga akajua wameshangaa kuwa kawajuaje na kuanza kuwahabarisha,
"Mimi nina utambuzi mpana sana na nimejua toka mnakuja kuwa ni mtu na mkwe wake"
Sakina akamuuliza,
"Kivipi mtaalamu?"
"Kivipi tena! Huyu si ni mke wa mtoto wako?"
Sabrina akauliza kwa mshangao pia,
"Mke wa mtoto wake! Kivipi?"
Huyu mganga hakuwaelewa kuwa kwanini wanashangaa kwavile hakufanya tafiti yoyote ya kuwahusu hawa wawili.
Sakina akamuangalia Sabrina kisha akamkonyeza na kuamua kuinuka na kuondoka huku wakimuacha yule mtaalamu akicheka.
Waliondoka kabisa eneo lile na Sakina ndiye aliyeanzisha mazungumzo.
"Huyu mganga ni muongo sana ndiomana huwa hana watu"
"Leo nimeamini msemo wa mama kuwa waganga ni waongo, mtu gani anaongea ujinga tu"
"Ila sio waganga wote waongo, ni huyu huyu tu. Bora turudi kwa yule wa mwanzo."
"Hapana dada, bora tu kurudi nyumbani"
Ikabidi wakubaliane kurudi nyumbani huku njia nzima Sakina akilalamika kuhusu yule mganga.
"Hana akili yule, mi nina mtoto mmoja tu ambaye ni Jeff na wakati huo huo Jeff ni mdogo sana halafu huku anaibuka eti umekuja na mkweo, yani Sabrina uwe mkwe wangu kweli? Anajua mahusiano yetu huyu? Kweli miwaganga mingine inavamia fani tu. Sijui ni la wapi hili liganga. Najuta kuja tena kwake maana leo ndio amenichefua zaidi kuliko siku zote za nyuma."
Sakina aliendelea kulalamika tu njia nzima.
Neema nae alidamka asubuhi na mapema huku akielekea hospitali.
Alifika na kwenda kwa daktari moja kwa moja.
Kisha akamueleza tatizo lake la kutoa damu.
"Hilo tatizo limeanzaje?"
"Limeanza gafla tu, sasa nina mashaka kuwa na mimba yangu imetoka pia."
"Pole sana, je kuna maumivu yoyote unayapata?"
"Yani dokta, sina maumivu yoyote zaidi ya damu kunitoka tu"
Daktari aliamua kumpima na kugundua kuwa hana mimba tena.
"Uwii mimba yangu imetoka?"
"Pole sana dada, ngoja nikupe dawa za kukusafisha tu"
Daktari akamuandikia Neema dawa kisha Neema akaondoka pale hospitali akielekea duka la dawa.
Alipokuwa njiani kwa bahati akawaona Sakina na Sabrina ikawa alijua wazi itakuwa ni ngumu kwa Sabrina kumkumbuka yeye kwavile hakuwa na kumbukumbu ila aliamua kumuita tu.
Sabrina alimuangalia Neema kwa kumshangaa tu.
Neema akamsalimia Sabrina pale kisha akamwambia,
"Naomba unisamehe Sabrina"
Sabrina alimshangaa na kumuuliza,
"Nikusamehe kwa lipi?"
"Kwakweli nimekukosea mamangu, nimekukosea sana. Sijui kama nitaweza kusameheka. Ila je wewe umewezaje kuzaa na Sam?"
Sabrina alijikuta akitazamana na Sakina kwa mshangao, kisha akajibu,
"Kuwezaje kivipi? Kwani wengine wanazaaje na waume zao?"
"Najua huna kumbukumbu Sabrina, nisamehe bure"
Sakina naye akauliza,
"Umejuaje kama hana kumbukumbu?"
Neema akawatazama na kuwajibu,
"Niliambiwa na Sam pindi alipokuwa anaumwa"
Sakina akamuangalia tu Neema huku Neema nae akitamani kumuuliza kwa undani Sabrina ila hakuweza na kuamua kuwaaga kisha kuondoka.
Sabrina akasikia kama kitu kikimwambia moyoni mwake,
"Ni huyo dada msaidie"
Akabaki kumuangalia tu Neema akitokomea kwani hakujua kuwa atamsaidia kwa namna gani.
Sakina akamuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Mbona unamuangalia sana? Umemkumbuka kwani?"
"Hapana sijamkumbuka ila kuna kitu kinaniambia nimsaidie hata sijui nimsaidiaje"
"Mmh umsaidie? Kivipi? Nina mashaka na hiyo sauti inayokwambia"
"Una mashaka nayo kivipi?"
"Inawezekana ukawa na jini Sabrina ndio linalokuelekeza hayo, ndiomana mimi nakukazania kuwa twende kwa wataalamu"
Ile sauti ikaendelea kumwambia Sabrina kuwa amsaidie yule dada.
Ikabidi waamue kumfatilia kwa nyuma na kumuita kwa Neema alikuwa akitembea taratibu.
Neema akawasikia na kugeuka nyuma kisha wao wakamfata alipo.
Alianza Sakina kwa kumuuliza swali Neema,
"Je unatatizo lolote dada?"
Neema akatabasamu kwa kujilazimisha na kutikisa kichwa huku akiwajibu,
"Hapana, sina tatizo lolote"
Sabrina akaguna na kumuuliza,
"Mmh! Mbona kuna kitu kinaniambia kuwa nikusaidie"
"Unisaidie? Unisaidie nini sasa? Mi nipo sawa bhana"
Huku Neema akiwa na mashaka kuwa huenda wamegundua tatizo lake.
Sakina alipoona kuwa huyu dada anamashaka nao ikabidi ajigeleshe kwa kumuomba msamaha.
"Samahani dada, hatukuwa na nia mbaya dada yangu"
"Usijali lakini"
Kisha wakaagana tena na Neema akaondoka zake.
Sakina na Sabrina waliamua kurudi nyumbani huku sauti ile ikiendelea kumwambia Sabrina kuwa amsaidie yule dada.
Sabrina aliamua kumueleza Sakina kuhusu yale matone ya damu aliyoyaona na sauti aliyoisikia.
"Sasa nadhani kuwa kuna uhusiano katika haya mambo mawili"
"Usiwaze sana Sabrina, mambo kama haya unatakiwa kuwa nayo makini sana. Ukizingatia huna kumbukumbu za nyuma. Unatakiwa kuwa makini mdogo wangu"
Wakakubaliana pale kisha Sakina akamuacha Sabrina pale kwao na kumwambia kabisa mama Sabrina kuwa wamesharudi tayari.
Neema alipofika kwake alikaa na kupumzika.
Akakumbukia walivyoonana na wakina Sabrina na akakumbuka jinsi Sabrina alivyokuwa anasema kuwa kuna kitu kinamwambia amsaidie.
Akakumbuka matatizo ya Sabrina, wakati akifikiria hayo rafiki yake Rose alikuja kumuuliza kuhusu majibu ya hospitali.
Ila Neema hakumwambia kwanza khabari za hospitali bali alimueleza alivyokutana na Sabrina na mambo yaliyoendelea.
"Sasa kwanini umekataa asikusaidie?"
"Kumbuka yule hana kumbukumbu, na je atanisaidiaje?"
"Inamaana umesahau kama yule ndio anatakiwa kubeba matatizo yako wewe?"
"Kubeba kivipi?"
"Umesahau yule mganga alivyotuambia kuwa anamtupia jini yule Sabrina kisha matatizo yako yote atakuwa anayabeba yeye, umesahau?"
"Nimeanza kukumbuka sasa ila atanisaidiaje?"
"Unakumbuka Sabrina alivyoenda kwa Sam akang'atwa na nyoka?"
"Nakumbuka ndio"
"Na aliugua sana ila Sam alipoenda kuonana nae yale matatizo yote yakarudi kwako hadi nilipoenda kufata dawa tena kwa yule mganga"
"Hayo yote nakumbuka, kwahiyo nikitaka haya matatizo yaende kwa Sabrina inatakiwa akaonane na Sam?"
"Hapana, ila Sabrina anatakiwa aende nyumbani kwa Sam ili aweze kuyabeba matatizo yako yote. Sasa pale ulitakiwa kumjibu kuwa ndio unaweza kunisaidia ila itabidi uende nyumbani kwa mumeo kwanza, na akienda tu khabari itakuwa imeishia hapo kwavile atabeba ugonjwa wako wote"
"Mmh namuonea huruma maana yote nimemsababishia mimi"
"Huruma ya nini wewe? Yani uteseke wakati wa kuwapa matatizo wapo"
"Dah! Atazidi kutia huruma, kwanza mpaka hapa sio kosa lake, ni kosa langu mimi mwenyewe na tamaa zangu ya kumng'ang'ania mwanaume ambaye hata kumjua vizuri simjui, yani huyu Sabrina namuonea tu"
"Acha ujinga wewe, halafu mmh samahani shoga yangu, mbona kama kuna kiharufu nasikia!"
"Kiharufu! Kivipi?"
"Yani kiharufu kama cha kitu kimeoza"
"Mmmh hata sijui"
Neema hakutaka kumjibu kuwa ni kiharufu cha nini bali alijigelesha tu kisha akainuka na kwenda kuoga.
Inaendeleaaah
No comments: