Simulizi: Je haya ni mapenzi? sehemu ya 56


Sam alikuwa akijiuliza maswali na akaona ni vyema akutane na Sabrina na aweze kumueleza ukweli huku akihisi kuwa huenda hiyo ndio njia pekee ya kumfanya yeye asahau kuhusu swala zima la kumsaliti na mwisho wa siku kuwa karibu nae.
"Yani wakati nipo na Sabrina sikuthubutu kufanya makosa, nilikuwa makini sana kupita maelezo ya kawaida ila toka yupo mbali nami kwa hii miezi michache tu nimejikuta nikimaliza hawa wadada. Nifanye nini kupunguza mawazo ikiwa hawa wadada ndio wenyewe wanaoniingiza katika vishawishi? Nifanyeje mie?"
Alijiwazia sana bila ya jibu na kuamua kwenda baa kwa asubuhi hiyo ili anywe hata supu aweze kuchangamsha akili yake.

Wakati Sam alipokuwa pale baa akinywa supu, alikuja mdada kumsalimia ambapo aligundua kuwa ni rafiki wa Sia,
"Shemeji, sijakuona kwenye mazishi jana"
"Mbona nilikuwepo, hili ni pigo letu sote"
"Yani mi hadi leo nashindwa kuamini, mara ya mwisho aliniaga kuwa anakuja kwako nikashangaa kupigiwa simu kuwa amekufa gafla akiwa kwakina Aisha yani hata sijui amepatwa na kitu gani kwakweli. Inasikitisha sana, hivi shemeji ulionana nae kweli marehemu Sia ile juzi?"
Sam akakaa kimya kidogo huku akitafakari cha kumjibu,
"Nilionana nae ndio ila aliniaga kuwa kuna mtu anamuwahi, maskini kumbe alikuwa anakiwahi kifo!"
Walijikuta wakisikitika kwa pamoja bila huyu rafiki wa Sia kujua siri iliyopo kwa Sam.
"Basi ndio hivyo tulimpenda ila Mungu kampenda zaidi. Tumuachie Mungu tu haya mambo kwakweli. Hivi na wewe unaitwa nani vile?"
Sam alimuuliza jina huyu rafiki wa Sia,
"Kumbe umesahau jina langu, mi naitwa Ritha"
"Sawa Ritha, sitalisahau tena"
Kisha Sam akamuaga Ritha kuwa anaondoka ila Ritha akamuomba namba ya simu kwanza,
"Samahani shem, unaweza kunipatia namba yako"
Sam hakuwa na tatizo juu ya kutoa namba yake, alimtajia pale kisha yeye akaondoka zake.

Wazo kubwa lililokaa kwenye kichwa cha Ritha muda huo ni kuhusu kupata kazi kwani alikuwa na shida sana kuhusu swala zima la kazi kwahiyo alipoelezewa kuwa Sam ana ofisi yake ndipo wazo la kutafutiwa kazi lilipomkaa kwenye akili yake.
Aliona hapa sasa ni mahali pa matumaini.
"Ila Sia angekuwepo ndio ingekuwa rahisi kwakweli maana angenisaidia juu ya kumshawishi huyu shemeji. Maskini rafiki yangu, Mungu akupokee"
Alimaliza kuongea huku akiumizwa na swala zima la kufa kwa Sia.

Jeff alimfata mama yake nyumbani na kujaribu kumbembeleza kwani alijua wazi kuwa ni lazima mama yake atakuwa amechukia baada ya Sabrina kumcheka kwahiyo alikuwa nae kumbembeleza.
"Mama, mbona kuchukia vitu vidogo tu vile?"
"Vidogo wakati mlikuwa mnanicheka jamani"
"Sio hivyo mama, usipaniki ilikuwa ni katika hali ya utani tu"
"Utani wakati kuna mambo mnanificha"
"Jamani mama, tumekuficha nini tena?"
"Nakushangaa sana Jeff mwanangu, mamako nahangaika kulea watoto wa wengine wakati wajukuu wangu wa kiukweli wapo jamani! Mnachonifanyia sio sawa kabisa"
Jeff akajaribu kutafakari kwa haraka haraka na kugundua kuwa lazima kuna kitu ambacho mama yake anakihisia kuhusu yeye na Sabrina ila anawezaje kumwambia mama yake kuwa mawazo anayoyawaza ni ya kweli.
Alitamani kumwambia mama yake ukweli lakini aliona kuwa ni wazi atamchukiza Sabrina kama tu atasema ukweli kuhusu wao, ila bado Sakina alimtolea macho mwanae akifikiria kama lipo jibu atakalopewa ila Jeff alikuwa kimya tu na kuelekea chumbani kwake.
Sakina alimuangalia mwanae bila ya kummaliza kwakweli.

Sabrina alibaki mwenyewe sasa na kwenda kuwasafisha wanae ambapo alikuta mama yake ameshafanya hivyo,
"Ila mama unanipenda sana"
"Lazima nikupende mwanangu, kwanza kabisa wewe ndio mtoto pekee wa kike kwenye tumbo langu"
Sabrina akapata upenyo wa kumuuliza mama yake swali,
"Hivi mama unaonaje mapenzi ya mdada mtu mzima na kijana mdogo wa kiume?"
"Ingawa sijakuelewa unataka nini, ila swala la mapenzi ni swala pana sana"
"Ndio nimekuuliza swali hilo, mapenzi ya kijana mdogo wa kiume na mdada mtu mzima. Je hayo ni mapenzi?"
"Kwanza kabisa utambue kwamba mapenzi yanamaanisha upendo, kama huyo kijana na huyo mdada wanapendana basi hayo ni mapenzi. Na kama ilivyo, mapenzi huwa hayachagui yani hutegemea tu na upendo uliopo baina ya hao watu wawili"
"Mmh mama, na mtu anayeolewa na mwanaume halafu hawafanyi chochote ndani kama mke na mume namaanisha lile tendo la ndoa, vipi hayo ni mapenzi?"
"Mmh Sabrina mwanangu kwani tatizo ni nini? Ningejua tatizo ingekuwa rahisi kukujibu, mume aishi na mke ndani na hawafanyi chochote mmh labda kama huyo mwanaume anatatizo ila bado sijaelewa mwanangu kwani kuna chochote kinachokutatiza?"
"Nitakueleza vizuri mama, upo muda nitakueleza vizuri tu na utanielewa mama yangu. Ni kweli kuna mambo mengi yanayonitatiza ila nitakwambia tu"
Mama Sabrina alimuangalia mwanae na kumsikitikia kwani aliumizwa sana na kitendo chake cha kufanya siri siku zote ila alishukuru hata kwa maswali aliyoulizwa na mwanae na kuona kuwa ni wazi ipo siku atamwambia siri zake.

Fredy alipigiwa simu na Neema na kwenda nyumbani kwake,
"Kaka yangu Fredy, nina ombi moja tu kwako"
"Niambie dada usiwe na wasiwasi"
Fredy alimsikiliza Neema huku akivumilia ile harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kwa Neema.
"Nakuomba uniletee Sabrina hapa, nina shida nae nina maongezi nae"
"Mmh sidhani kama itakuwa rahisi dada, si unajua kama ana mtoto mdogo kwasasa?"
"Najua ndio, ila ningependa aje nizungumze nae tafadhari. Naomba ufanye njia yoyote uniletee Sabrina"
Fredy akajifikiria sana jinsi ya kumshawishi Sabrina ila mwisho wa siku ilibidi akubaliane na hali halisi tu kuwa Neema anashida na Sabrina kwa siku hizo na kumuahidi kulitekeleza swala lake.
Fredy alipoondoka, Aisha alimuuliza Neema kuhusu Sabrina aliyekuwa akiongelewa pale.
"Nasikia huyo Sabrina ni mtu mbaya sana"
"Hapana Sabrina si mtu mbaya ila sisi wenyewe ndio wabaya"
Kisha Neema akamuomba Sia ampatie karatasi na peni ambako alianza kuandika vitu alivyokuwa akivijua yeye mwenyewe kwani Aisha hakuelewa chochote ukizingatia hakupewa kuvisoma.

Kesho yake Fredy alifanikiwa kumshawishi Sabrina kisha kuondoka naye pale kwake hadi nyumbani kwa Neema, ambapo Aisha aliwakaribisha na wao kuingia ndani.
Sabrina alimuhurumia sana Neema kwa ile hali aliyomuona nayo, ila Neema hakusema chochote zaidi ya kuitoa ile barua aliyoiandaa na kumpa Sabrina, ambapo Sabrina alifungua ile barua na kuanza kuisoma taratibu.
Sabrina alishtushwa sana na kilichoandikwa na Neema, na alipojaribu kumtazama Neema alimuona kalala huku damu zikimtoka mdomoni.
Sabrina alishtuka na kuwashtua Fredy na Aisha.

Sabrina alishtushwa sana na kilichoandikwa na
Neema, na alipojaribu kumtazama Neema alimuona
kalala huku damu zikimtoka mdomoni.
Sabrina alishtuka na kuwashtua Fredy na Aisha.
Wakamuangalia Neema vizuri sasa na alikuwa kimya kabisa, Sabrina alihisi kama kuchanganyikiwa ila kabla ya yote alikunja ile barua na kuweka kifuani pake kisha akainama alipo Neema akimtingisha na kumuamsha ila Neema alikuwa kimya kabisa na kuwafanya wote waumie.
Fredy alienda kufata gari kisha wakasaidiana kumbeba Neema na kumuwahisha hospitali huku wote wakiwa na hofu kuwa huenda Neema amepatwa na umauti na ndivyo walivyopewa jibu na daktari baada ya muda mchache tu kuwa Neema amefariki.
Sabrina alichanganyikiwa zaidi na hakujielewa kwa wakati huo kwani hata alisahau kama alienda na mkoba kwa Neema na kuuacha huko huko.

Fredy ndiye aliyekuwa mtu pekee wa kuweza kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki kuhusiana na kifo cha Neema kwani hata Aisha alikuwa kachanganyikiwa tayari kwa kifo hicho na kumfanya ashindwe hata kulia kwa mshtuko wa gafla uliompata, alijikuta tu akiongea peke yake kwa masikitiko,
"Dada Neema, ulikuwa badala ya dada yangu Rose. Nikakuthamini na kukujali, sikujali harufu mbaya iliyotoka kwako kwani nilikupenda na nilikuombea siku zote urudi katika hali yako ya kawaida dada. Jamani jana umeandika barua ndefu sana, hukutaka hata kuniambia inahusu nini ila kumbuka dada uliniahidi kunieleza mambo mengi sana. Ila mbona umekufa bila ya kuniambia chochote? Kwanini dada Neema umekufa? Kwanini lakini? Kwanini dada?"
Sabrina alijikuta akimuhurumia sana Aisha na kwenda kumkumbatia kwa uchungu, ni hapo ndipo machozi yakamtoka Aisha kwani alikumbuka maneno ya Neema kuwa Sabrina hana kosa lolote kwani Neema aliamini hivyo na kujiona kuwa yeye ndio mwenye makosa kwa kufosi penzi la mume wa mtu.
Sabrina alikumbatiana pale na Aisha huku machozi yakiwatoka.
Fredy alisogea na kumuomba Sabrina kuwa amrudishe nyumbani ila kwavile Sabrina alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa alijikuta akikataa kuondoka kabisa na kumfanya Fredy ashindwe la kufanya zaidi ya kuamua kumpigia simu mama wa Sabrina na kumwambia hali halisi ilivyo.

Muda Fredy anampigia simu mama Sabrina ni muda huo huo Jeff nae alikuwa nyumbani kwakina Sabrina kwa lengo la kumuona.
Akamshangaa mama Sabrina kuanza kulalamika simu ilipokatika,
"Yani huyu Sabrina huyu sijui vipi, eti amegoma kurudi nyumbani"
"Amegoma? Kwani yuko wapi?"
"Sijui hospitali sijui nani kafa huko na yeye kagoma, eti mimi nikambembeleze arudi na watoto hapa itakuwaje mbona huyu Sabrina ana matatizo jamani"
"Hebu nieleze vizuri nikamfate mie mama"
"Khee mie bibi yako wewe sio mama yako, ngoja tumpigie tena simu mtu huyu atuelekeze"
Mama Sabrina akampigia simu tena Fredy aliyewapa maelekezo na muda huo huo Jeff akaondoka kwenda kumfata.

Siku ya leo Sam alikuwa nyumbani kwake na kupatwa na maumivu ya moyo ya gafla sana, akajua kuwa lazima kuna tukio limetokea, tena tukio sio la kawaida. Kengele ya khatari ikagonga kwenye akili yake,
"Ni kifo, Mungu wangu nani kafa tena?"
Hofu ikamjaa na kumuwazia Neema, akachukua simu yake na kumpigia Neema ambapo iliita tu bila ya kupokelewa.
Sam alitamani kujua kilichotokea kwani moyo wake ulikuwa na maumivu sana.
Aliamua kutoka kwenye nyumba yake na kuelekea hotelini ili tu aweze kujiliwaza japo kidogo.

Jeff alifika hospitali na kuwasiliana na Fredy aliyemuelekeza walipo.
Jeff aliwafata na kumuona Sabrina kajiinamia tu, Jeff akamsogelea Sabrina na kumfanya ainuke na kumkumbatia huku machozi yakimtoka kwa mfululizo,
"Tafadhari Sabrina, twende nyumbani"
"Sijisikii kwenda nyumbani Jeff, natamani nikae hapa hapa"
"Najua una uchungu sana, lakini fikiria kuhusu watoto wetu. Watoto wanakuhitaji mama yao, tafadhari twende mama"
Fredy alikuwa pembeni akimuangalia Jeff na harakati zake za kumbembeleza Sabrina, ila swala la kusema 'watoto wetu' hata yeye lilimshangaza kwakweli, ila baada ya maneno hayo alimuona Sabrina akikubali kuondoka kisha Jeff akamshika mkono na kumuaga Fredy pale.

Jeff alikodi gari ndogo ya kuwarudisha kwani kwajinsi Sabrina alivyoonekana kuchanganyikiwa akaona isingekuwa vyema kupanda nae daladala.
Alikaa nae karibu akimbembeleza na kumpa moyo huku akimwambia yote amwachie Mungu,
"Sabrina usichanganyikiwe, bali mshukuru Mungu kwa kila jambo mama angu. Kila kitu hutokea kwasababu fulani, usichanganyikiwe sana"
Sabrina alijiona kupata faraja ya kuwa karibu na Jeff kwani alionekana kumbembeleza sana na kumfanya hata ajisikie vizuri kiasi.
Walifika nyumbani na kushuka huku Jeff akiwa amemshika mkono na kuingia nae ndani.
Walipokuwa wanaingia, Sabrina akaona kuna nguo ya mwanae imeanguka na kuinama kuiokota, ila alipoinama na ile barua ikaanguka na kuokotwa na Jeff ambaye aliiweka mfukoni mwake bila ya kuwmwambia chochote kile Sabrina ambaye aliingia ndani na kwenda kuoga kwanza kabla ya kuwashika wanae.

Sabrina alipotoka kuoga Jeff alikuwa ameondoka kitambo sana na mama Sabrina ndiye aliyekuwepo pale sebleni na watoto ambapo Sabrina alitakiwa kumnyonyesha kwanza mtoto kabla ya mambo mengine kuendelea ndiomana akaoga kwanza.
Muda kidogo mtoto alilala na kwenda kumlaza, Sabrina akakumbuka kuhusu ile barua na kukumbuka kabisa kama aliiweka kifuani ila alipekua kwenye nguo zake bila ya kuiona na kujiuliza kuwa barua ile iko wapi,
"Mmh sijui nimeiangusha?"
Alitaka kuimalizia kuisoma kwani anakumbuka wazi kuwa aliishia mahali palipoandikwa kuwa,
"Sijui kama utafanikiwa kuimaliza barua hii kabla ya mimi mauti kunikumba"
Ni mahali hapo palipofanya amtazame Neema na kumuona akitoa damu mdomoni na huo ukawa ndio mwisho wake.
Sabrina aliumia sana kuiangusha barua hiyo ingawa alitambua kuwa chanzo cha mambo yote ni Sam.

Jeff aliingia ndani kwao na kuitoa ile barua ili aisome ila kabla ya kufanya hivyo mama yake alimuita na kumfanya aiache kwanza ile barua.
"Dorry kanipigia simu leo na kusema kuwa ameoteshwa ndoto mbaya sana"
"Ndoto mbaya? Mmh huyo Dorry nae ameanzwa kuchanganyikiwa sasa, ndoto gani hiyo?"
"Tatizo mwanangu unapenda kupinga vitu sana, ila jaribu kuwasiliana nae anaweza kukueleza vizuri"
Jeff akaona isiwe tatizo na kukubaliana na mama yake pale kisha kuwasiliana na Dorry ambaye alimwambia kuwa asingeweza kumweleza kwenye simu ila labda aende na kumfanya Jeff afunge mlango wake kisha kumuaga mama yake na kutoka akielekea kwakina Dorry.
"Sasa si utachelewa sana kurudi?"
"Ndio mama, si unajua kama kule ni mbali mama"
"Sawa basi"
Jeff akaondoka zake.

Sam alikuwa vinywaji vyake pale na kutamani hata kulala pale pale hotelini.
Ila alipigiwa simu na Ritha na kumuelekeza alipo ambaye nae alienda pale hotelini kama kumpa kampani tu ila Sam alionekana kulewa tayari,
"Kwanini ulale hapa wakati una nyumbani kwako jamani"
"Sipapendi nyumbani kwangu, pamepooza sana. Mke wangu alinikimbia, mambo hayaeleweki kabisa"
"Pole sana, ila kwanini mkeo alikukimbia?"
"Historia ndefu ila mke wangu kanikimbia, kwangu kumepooza sana"
Halafu Sam alionekana kama kulengwa na machozi na kumfanya Ritha amuonee huruma sana,
"Basi mi nakuomba, nipo chini ya miguu yako twende nyumbani. Ni usiku huu tayari"
"Nimekwambia kwangu kumepooza"
"Usijali nitakupa kampani"
"Kweli? Utanipa kampani kama hivi?"
"Ndio, wee niamini tu. Twende nyumbani tafadhari"
Sam aliona ni jambo jema kuwa na kampani na kwavile Ritha alionekana ni mdada mpole na mstaharabu hakuhisi kama anaweza kufanya nae chochote kibaya.
Kwahiyo wakapanda gari na kuelekea nyumbani kwa Sam.

Jeff alifika kwakina Dorry na kumkuta Dorry ambaye alikwenda kumkumbatia.
Jeff nae akamkumbatia pia ili aweze kumsikiliza hoja zake, ila kabla ya yote alimuuliza kwanza kuhusu mtoto,
"Mtoto yuko wapi Dorry?"
"Yupo kalala"
"Eeh niambie hiyo ndoto mbaya uliyoota kuhusu mie"
"Mmh ndio kwa kusimama hivi, hebu tuingie ndani kwanza"
Jeff akakubali na kuwafanya waingie na kukaa sebleni ila leo nyumba yakina Dorry ilikuwa kimya sana na kumfanya Jeff aulizie na hili pia.
"Vipi mbona leo kimya sana hapa kwenu? Wengine wako wapi?"
"Wameenda kwenye sherehe, yani nimebaki mwenyewe hapa basi nyumba inaboa balaa"
"Pole kwa kubaki mwenyewe, ila nieleze kuhusu hiyo ndoto si unajua huku kwenu ni mbali na giza limeshaanza lakini!"
"Naelewa hilo, ila kabla sijakwambia naomba nikuulize kitu"
"Niulize tu"
"Hivi wewe yule Sabrina unampendea nini?"
Jeff akamshangaa Dorry kwa swali lake na kujikuta akimuangalia tu kisha akamuuliza,
"Kumpendaje pendaje yani sijakuelewa"
"Mmh Jeff umenielewa vizuri sana. Mi najiuliza siku zote wewe umempendea nini Sabrina? Kwanza yule mdada ni mtu mzima kwako, pili ni kama ndugu yako, tatu mabinti wa rika lako tupo tena tuna mvuto kuliko huyo bibi. Hebu nitazame vizuri mimi nilivyo Jeff"
Dorry aliinuka na kuanza kujinengulisha kwa Jeff kuwa amtazame vizuri ila Jeff alikuwa kimya tu bila ya kuongea chochote ambapo Dorry aliendelea kusema,
"Pia yule kakomaa, si mama yako mdogo yule? Hivi umempendea nini mwanamke mtu mzima kama yule Jeff, unajua kwamba unasikitisha wewe! Yule ni mtu mzima waachie watu wazima wenzie. Yule ni bibi kwako"
Jeff akachukizwa na kauli za Dorry dhidi ya Sabrina na kumuuliza,
"Umemaliza? Hiki ndicho ulichoniitia Dorry? Yani kunitoa kwetu hadi hapa nia yako ni kumuongelea Sabrina!"
Jeff aliinuka kwa hasira na kutaka kutoka, Dorry akamvuta shati ili asiondoke ila kwavile Jeff alishapandwa na hasira tayari alijikuta akimnasa kibao Dorry kisha akaondoka zake na kumuacha Dorry akiugulia kibao alichopigwa.

Jeff alirudi nyumbani kwao na kwenda kulala moja kwa moja kwani aliumizwa na kile kitendo cha kusemwa Sabrina wakati yeye ndio chanzo cha mambo yote.
Aliona ni bora mtu atokee na kumtukana yeye matusi yote ya duniani lakini sio kwa kumtukana Sabrina kwahiyo moyo wake uliumia sana.

Sam alifika nyumbani kwake akiwa na Ritha, ambaye alishangazwa na ukubwa na uzuri wa nyumba hiyo huku magari yake yakiwa vizuri yamejipanga na kujiuliza kama mke wa Sam ana akili timamu kweli kukimbia nyumba nzuri kiasi hicho na licha ya vyote ni kumkimbia mwanaume mwenye pesa kiasi cha Sam wakati ni wanawake wengi sana wanaopenda kuishi na wanaume wenye pesa kwani hakuna mtu anayependa maisha ya shida.
Sam alimkaribisha Ritha vizuri sana na kuongea mambo ya hapa na pale.
"Kwahiyo Sam mkeo kaondoka na watoto?"
"Ndio kaondoka nao, nimebaki mpweke tu hapa"
"Pole sana"
"Asante, ila ukitaka kulala niambie kuna vyumba vingi tu vya kulala hapa"
"Kwahiyo wewe leo hutolala?"
"Kama nikipatwa na usingizi basi nitalala hapa hapa sebleni"
"Kwanini wakati chumbani kwako kupo? Kwani chumba unacholalaga kiko wapi?"
Sam akamuonyeshea tu Ritha kwa mkono kisha wakaendelea na maongezi mengine bila ya Ritha kudai kwenda kulala wala nini mpaka pale Sam aliposinzia pale pale sebleni.
Ritha akaamua kutumia uungawana na kuanza kumkongoja Sam mpaka chumbani kwake ambapo Sam alilala tu kisha Ritha kumfunika shuka na yeye kwenda sebleni kukaa.

Kwakweli nyumba ya Sam ilikuwa ni kubwa na kwa mtu muoga tena kama Ritha aliyefiwa na rafiki yake siku za karibuni ilikuwa ni ngumu kwa yeye kukaa mwenyewe pale sebleni na kugundua kuwa ni kwanini Sam hakutaka kurudi kwake.
Hivyo na yeye akaingia chumbani kwa Sam na kulala pembeni yake.

Sabrina aliwaza usiku kucha kuhusu Neema, maneno aliyoyaandika Neema kwenye ile barua yalimjia kichwani kwa mfululizo haswa neno la kusema kwamba,
"Sam ni muuaji"
Lilikuwa likijirudia kila mara kwenye akili yake na kupata wazo la kwenda kuonana tena na Sam ingawa ile barua ilikuwa imepotea.
Kwahiyo alipoamka tu alfajiri kabla ya watoto kuamka, yeye alidamka na kujiandaa ili amuwahi Sam kabla ya kwenda kazini ili hata badae apitie kwao waongee kwani kwa kipindi hiki Sabrina hakuwa na simu na hakuweza kuwasiliana na Sam kwa kupitia simu ya mama yake.

Sam naye kulipokucha akashangaa kuona Ritha kalala pembeni yake, alimuangalia tu bila ya kumuamsha huku akiinuka kutoka kitandani.
Akasikia mtu akigonga mlango, moja kwa moja akahisi ni mlinzi wake kuwa huenda ana tatizo.
Sam akaenda kumfungulia na Sabrina akaingia moja kwa moja ndani,
"Kheee mbona asubuhi asubuhi sana Sabrina?"
"Kwani mke anapangiwa muda wa kwenda nyumbani kwa mumewe?"
Sam hakusema cha zaidi ila alimkaribisha tu, muda huo Ritha nae akatoka chumbani kwa Sam na kumfanya Sabrina ashtuke na kusema kwa mshangao,
"Kheee Sam utaua wangapi?"
Ritha alibaki kuduwaa tu kwani hakujua kinachoongelewa, Sam naye alishangazwa na kauli ya Sabrina.


Sam hakusema cha zaidi ila alimkaribisha tu,
muda huo Ritha nae akatoka chumbani kwa Sam
na kumfanya Sabrina ashtuke na kusema kwa
mshangao,
"Kheee Sam utaua wangapi?"
Ritha alibaki kuduwaa tu kwani hakujua
kinachoongelewa, Sam naye alishangazwa na kauli
ya Sabrina.
Sabrina aliendelea kuwatolea macho kama anahitaji jibu kutoka kwao.
Sam akaona hapa lazima Sabrina ataleta longolongo na kumuomba Ritha aondoke mahali pale, Ritha naye hakubisha zaidi ya kuchukua mkoba wake kisha Sam akamsaidia kumtoa nje ila alimshangaa Sabrina leo bila ya kufanya vurugu zozote zaidi ya yale maneno ya kwanza tu.
Sam alirudi ndani na kumtazama Sabrina kwa lengo la kutambua tatizo lake.
"Haya niambie Sabrina"
"Hivi unajua wewe Sam hujielewi, hivi unajua kama Neema amekufa?"
"Sasa kama amekufa mimi nifanyaje?"
"Hivi Sam unathubutu kweli kusema maneno hayo? Si unajua kama amekufa kwaajili yako?"
Sam akajua moja kwa moja kuna maneno ambayo Neema alimwambia Sabrina hivyobasi akaamua kujigelesha tu kwani Sabrina alishaujua ukweli.
Sam akaanza kwa kucheka,
"Amekufa kwaajili yangu? Hebu acha kunichekesha Sabrina, mtu anakufaje kwaajili yangu bhana!"
"Kwahiyo unaniona mimi kama nimekuja kukutania vile. Au huyu mtu ametania kwa kusema wewe ni muuaji?"
"Kama mimi ni muuaji mbona sijakuua wewe? Au huyo Neema alipokuwa anakufa uliniona mimi nimekuja na kumpiga risasi au ni nini?"
Sabrina alimuona Sam akijaribu kukwepa tu ukweli wa mambo ila kwavile hata yeye hakuimalizia ile barua ya Neema ikawa ngumu kwake kujua kila kitu kilichomkabili Neema.
Alijikuta akimuangalia Sam kwa jicho la hasira sana kwani hakuona kama Sam ni mtu mzuri kwake.
"Naondoka, ila Sam uende msibani"
"Hapa tutaondoka wote, na huko msibani tutaenda wote"
Kisha Sam akaenda kufunga mlango wake kwa funguo ili aweze kujiandaa halafu Sabrina asiweze kutoka.

Jeff naye alipoamka alikaa na kutafakari yale mambo yanavyoenda, alijiuliza kuwa ni nani alimpa ujasiri Dorry na kumfanya aweze kuropoka kuhusu yeye na Sabrina.
"Huyu Dorry huyu sio bure, lazima kuna mtu anayempa ujasiri wa kufanya mambo ya kijinga kila mara. Ndiomana limezaa na mchina kisha kutelekezwa na kubaki kudandia tu wanaume wa kiswahili kuwa mtoto ni wao. Yani huyu mwanamke huyu na nitamkomesha"
Yani Jeff alikuwa amechukizwa sana na yale maneno aliyoambiwa na Dorry kuhusu Sabrina.
Alikaa sasa na kutafakari, kisha akakumbuka barua aliyoiokota toka kwa Sabrina, kisha akaitafuta ilipo na kuifungua kwa kuanza kuisoma na kushangaa barua iliyokuwa kama stori au risala.

"Kwako Sabrina, najua ni ngumu wewe kukubali kuja kwangu na kunisikiliza yale ninayotaka kukwambia ndiomana nimeamua kuandika hii barua ili angalau upate kwa kidogo kile ambacho nilitaka kukwambia.
Kwanza kabisa nisamehe sana kwani kuna mengi mabaya nimeyafanya kwako, tafadhari nisamehe sana.
Ila kabla ya yote napenda ujue kuwa Sam ni muuaji, tena ni muuaji kabisa. Ametumaliza wengi sana ingawa hadi nakufa sitaweza kujua kuwa uuaji wa Sam umesababishwa na nini ila Sam ni muuaji.
Nimeteseka sana mimi, nimeumia sana lakini chanzo cha yote ni Sam. Mauti itanifika ila ujue wazi kuwa Sam ndio chanzo cha mauti yangu. Wadada wengi wamekufa, tafadhari Sabrina kuwa mlinzi wa karibu kwa wadada wote wanaojisogeza kwa Sam kwani mauti itawakumba tu kama mimi.
Ila nakuomba utakapomaliza kuisoma barua hii uifiche, sitaki watu wajue aibu ambayo nakufa nayo.
Lakini sijui kama utafanikiwa kuimaliza barua hii kabla ya mimi mauti kunikumba.
Sabrina sina kinyongo chochote na wewe, na pia naomba tena na tena unisamehe.
Ni mimi niliyeenda kwa mganga na kushirikiana na rafiki yangu Rose ambaye naye ni marehemu kumvuta Sam kimapenzi. Na kweli tulifanikiwa kwani hata wewe ulisahaulika, pia tukakusababishia magonjwa mbali mbali. Leo nakiri kwako Sabrina kuwa ni sisi tuliokutupia jini na kukufanya upoteze kumbukumbu, mganga alitupa masharti mazito sana kuwa hairuhusiwi Sam kuja kukuona kwani akija tu inanifanya mimi kama muhusika mkuu kupatwa na magonjwa ya gafla, hivyobasi tukafanya juu chini ili Sam akusahau kabisa na tukafanikiwa kwa hilo.
Leo mimi nakufa kwani najiona kabisa mauti ikiniangalia, ila kinachoniua ni tamaa.
Tamaa ya pesa na mali, tamaa ya utajiri na maisha mazuri. Nakuomba Sabrina uwasihi sana wadada wenye tamaa kama mimi, tamaa ni mbaya Sabrina.
Mwanzoni nilijua ni wewe umefanya dawa kwa mumeo kuwa tukilala nae tuangamie ila jibu likaja kuwa ni kila mwanamke anayethubutu kulala na Sam basi anaenda na maji. Najua unajiuliza kuwa hilo jibu nimelipataje ila hata mimi nakufa huku nikijiuliza kuwa wewe umewezaje kuzaa na Sam ikiwa tu kila mwanamke anayelala nae lazima afe? Najua jibu unalo mwenyewe kuwa umewezaje ila walinde wadada waliobaki Sabrina.
Nilianza mimi ila nikakaa kimya kutunza siri hii kwa maumivu makali sana na mwisho wa siku nakufa, akafatia Rose ambaye hakuweza kukaa na siri hata masaa ishirini na nne tu naye akafa, amekuja Sia naye uzalendo ukamshinda na ameenda na maji. Nami sasa uzalendo umenishinda ila ikitokea nimepona basi nitakuwa ushuhuda katika jamaa na hata kama nikifa basi jambo hili ulishuhudie wewe.
Naumwa Sabrina, ugonjwa wangu ni toka siku ya kwanza kuingiliwa kimwili na Sam, kwakweli Sam si mwanaume wa kawaida hata nashangaa wfwe umewezaje kulala nae? Ilikuwaje hadi mkapata watoto? Ila jibu langu ni kuwa Sam sio mwanaume wa kawaida. Ningeandika mengi zaidi ila nimechoka Sabrina, nimechoka sana. Muulize Sam mwenyewe akueleze vizuri ila weka akilini kwamba kila msichana atakayethubutu kulala na Sam basi ataenda na maji kwani Sam ni zaidi ya ugonjwa wa ukimwi maana hapa nilipo ni kheri ningepata ukimwi saivi ningetumia dozi na kuendelea vizuri kuliko hali ambayo Sam anatuacha nayo.
Kwaheri Sabrina, pole kwa kukufanya uteseke na watoto, nisamehe sana.
Najutia makosa yangu kwakweli, najutia kwenda kwa mganga nipendwe badala yake nimejitesa.
Asante kwa kuisoma barua yangu hii ambayo kuna baadhi ya sehemu utakuwa na maswali ya kuniuliza ila sitaweza kukujibu kwavile nitakuwa marehemu, nenda kamuulize vizuri Sam na umwambie ukweli kuwa nilimpa dawa ya kukusahau, nilimwekea kwenye chakula ila yeye amenifanya kikubwa kuliko dawa niliyompa.
Kwaheri tena Sabrina.
Ni mimi Neema."

Jeff alipumua kwa nguvu sana baada ya kumaliza barua hii, akamfikiria Sabrina.
Akakumbuka maneno aliyowahi kuambiwa na Sabrina kwenye barua pia kuwa hajawahi kufanya tendo la ndoa na Sam, ni hapo akapata jibu kuwa kwanini alimkuta Sabrina akiwa bikra, akatambua kuwa Sabrina hakufata mkondo wa wenzie kwavile hajawahi kulala na Sam,
"Hivi inakuwaje watu waishi kama wapenzi, halafu kama wachumba na kumalizia na ndoa kabisa kama mke na mume kwa miaka hii yani walale wote na kuamka wote bila ya kufanya chochote? Mmh inawezekanaje hii? Mwanzoni niliposoma barua ya Sabrina nilijua kuwa Sam si mwanaume kamili sasa kama si mwanaume kamili amewezaje kulala na hawa? Amewezaje?"
Jeff akajifikiria sana bila ya kupata jibu la aina yoyote.
Aliikunja ile barua na kuiweka kisha akainuka na kujipanga kwenda kwakina Sabrina ili aone kama kweli ameisoma ile barua.

Sam alipomaliza kujiandaa alitoka ndani na kumwambia Sabrina,
"Haya twende sasa"
"Twende wapi na wewe?"
"Twende nyumbani tukachukue watoto wetu tulee"
"Eti tukachukue watoto wetu tulee, watoto wako na nani wale? Mwanaume wa ajabu sana wewe unajua kulala na wanawake wengine wakati mkeo hata kumgusa hujawahi ila watoto ndio useme wako"
"Hivi Sabrina hayo maneno yanakutoka wewe au? Hivi ni mwanaume gani anayekubali kulea watoto wa mwanaume mwingine?"
"Mwanaume gani anayekubali kulea watoto wa mwanaume mwingine? Inamaana hujijui au?"
Sabrina alikuwa akiongea kwa hasira na kupaniki tu bila hata ya kufikiria mara mbili kile anachoongea au madhara yake.
Sam naye alimuangalia kwa kumsikitikia tu,
"Shukuru Mungu nakupenda, shukuru Mungu sipendi kuumiza wewe wala kizazi chako. Sina kawaida ya kupenda kwani chuki niliwekewa toka nilipokuwa mtoto mdogo ila wewe nakupenda na kukuthamini shukuru sana hilo. Na usifikiri sijui kama wale watoto umezaa na mtoto mwenzao Jeff, mimi ni mtu mzima Sabrina na ninatambua kila kitu"
Sabrina alikuwa kimya gafla kama kamwagiwa maji baada ya kusikia kuwa Sam anajua kila kitu kuhusu yeye na watoto wake.
Kwahiyo ilikuwa kama mtu aliyeumbuliwa vile, Sam akamuangalia na kutabasamu kisha akasema
"Wapo watu wa kuwaficha ila sio mimi Sabrina, huwezi kunificha mimi. Nilijua kitambo sana ila sikuchukua hatua yoyote sababu nakupenda na sitaki uumie kwani najua ningemdhuru Jeff basi ningekuumiza wewe. Najua ni jinsi gani unampenda Jeff ila huweki wazi kwavile unaogopa jamii itakuchukuliaje. Sabrina, huna la kunificha mama. Haya twende sasa"
Sabrina aliinamisha kichwa chini na kuamua tu kutoka na Sam pale ndani.

Jeff alifika kwakina Sabrina na kumkuta mama wa Sabrina,
"Mmh Sabrina hata mimi namshangaa, yani kaondoka hapa asubuhi asubuhi ila hajarudi hadi muda huu. Kama unavyoniona hapa nahangaika na hawa watoto."
"Kwani ameenda wapi?"
"Alipoenda sijui kwakweli, na kama ujuavyo sasa hivi hana simu kwahiyo hata mawasiliano naye sina"
Jeff akatafakari kidogo juu ya alipoenda Sabrina bila ya kupata jibu, ila wazo likamjia kuwa huenda ameenda kwenye ule msiba wa Neema kisha akapata wazo la kwenda kumfata huko.

Inaendeleaah




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.