Simulizi: Je haya ni mapenzi? Sehemu Ya 57
Jeff akiwa anatoka kwakina Sabrina, akapigiwa honi na kuangalia gari akagundua ni moja wapo kati ya magari ya Sam.
Akasimama akiangalia linapoelekea, na lilikuja na kusimama karibu yake kisha Sam na Sabrina kushuka.
Jeff aliwatazama na kuwasalimia huku akijiuliza kuwa imekuwaje kuwaje hadi waamue kuongozana vile.
Sam aliitikia salamu ya Jeff kisha wote kuingia ndani ila Sabrina alikuwa kimya tu.
Mama Sabrina nae alimshangaa mwanae kwenda pale na Sam,
"Sabrina mwanangu, si unajua baba yako hamtaki huyo mtu"
"Naelewa mama, ila kumbukeni kwamba huyu ni mume wangu. Nimefunga nae ndoa takatifu na halali iweje sasa nimfukuze jamani? Mama si jambo jema kwakweli, ni mimi mwenyewe niliyeamua kumleta"
Mama Sabrina alimuangalia Sam na kumwambia,
"Tafadhari baba naomba uende, sitapenda Baba Sabrina akukute mahali hapa"
Sam hakutaka kubisha, ila alimvuta mkono Jeff na kutoka naye nje.
Wakati huo Sabrina alitamani hata kuwafata ili ajue mbivu na mbichi ila mama yake alimzuia na kumsisitiza abembeleze watoto,
"Hivi wewe hujijui kama umeshakuwa mama? Ulivyokuwa unawabebanisha hawa watoto ulikuwa na maana gani? Haya tulia hapo ubembeleze wanao maana mimi kazi yangu ilishaisha"
Sabrina alitulia ila alitamani kujua kinachoongelewa huko nje.
Sam alienda na Jeff hadi mahali pale alipopaki gari yake, kisha akamuuliza,
"Unajisikiaje mimi kufukuzwa hapo kwakina Sabrina?"
"Kwakweli najisikia vibaya kwani hata mimi ningekuwa ni wewe ningeumia tu"
"Unauonaje upendo wangu kwa Sabrina?"
Jeff akatulia kimya kidogo kwani maswali haya ya Sam yalimpa mashaka na kumfanya ajiulize kuwa kwanini Sam amuulize maswali hayo ila alijikaza na kumjibu,
"Naona una upendo mkubwa sana juu ya Sabrina"
"Kushinda upendo uliokuwa nao wewe?"
Jeff akawa kimya akimtazama tu Sam na kumfanya Sam atabasamu,
"Ok, but sio tatizo ila ukweli utabaki pale pale"
"Ukweli gani?"
"Wewe ni mwizi"
Kisha Sam akafungua gari yake na kuingia halafu kuondoka eneo lile na kumuacha Jeff akitafakari yale maswali aliyoulizwa na Sam.
Sam alitaka kwenda moja kwa moja kwenye msiba wa Neema ila alihisi moyo wake kumuuma sana, hakuwa tayari kushuhudia Neema akizikwa au watu wakiomboleza kwa kuondokewa na Neema.
Hakuwa tayari kuona chochote na aliamua kwenda hotelini ambako alienda jana yake.
Na kwavile alikuwa mpweke sana, akaona ni vyema apate kampani kama aliyoipata jana yake, ile kampani ya Ritha na kuamua kumpigia simu.
Ritha hakusita na kuamua kwenda hotelini alipo Sam.
"Ila leo sitaenda nyumbani kwako maana ile asubuhi duh ningepigwa mie"
"Usijali, hata mimi leo sitarudi nyumbani. Leo nitalala hapa hapa hotelini"
Sam alizungumza mambo ya hapa na pale na Ritha huku wakila na kunywa.
Mwisho wa siku aliamua kwenda kwenye chumba alichokodi pale hotelini, Ritha hakuacha kumsindikiza kuelekea kwenye chumba hiko.
Wakiwa chumbani, Sam alimshukuru sana Ritha kwa moyo wake wa upendo na huruma.
Kwavile Ritha alikuwa anaaga kuwa anarudi kwao, Sam aliamua kutoa kiasi cha pesa na kumpatia kama shukrani tu.
Ritha alishukuru sana kwa hilo, kisha akainuka na kuondoka kwani muda nao ulikuwa umeenda sana.
Ila alipotoka nje Ritha alijifikiria kuwa ni zawadi gani ampatie Sam kwa pesa anazompa? Aliona kumpali kwa kumpa kampani si zawadi pekee, ukizingatia kikubwa anachokitaka toka kwa Sam ni kupata kazi katika kampuni yake.
Akajifikiria sana, kisha akajipatia jawabu na kurudi ndani.
Sam alienda maliwatoni kupunguza maji ya bia alizokunywa kwa usiku huo, na kurudi zake kwa lengo la kulala sasa.
Akashangaa kumuona Ritha akiwa kajilaza kitandani huku akiwa mtupu kabisa kwani nguo zote alitoa na alikuwa akitabasamu.
Sam alienda maliwatoni kupunguza maji ya bia
alizokunywa kwa usiku huo, na kurudi zake kwa
lengo la kulala sasa.
Akashangaa kumuona Ritha akiwa kajilaza
kitandani huku akiwa mtupu kabisa kwani nguo
zote alitoa na alikuwa akitabasamu.
Sam akamuangalia kwa kutikisa kichwa na kumuuliza,
"Unafanya nini Ritha?"
Ritha aliendelea kutabasamu na kumfanya Sam aongee tena,
"Ritha tafadhari, usitake nifanye makosa niliyoyafanya zamani sana na yanayonitesa hadi leo"
Huku Ritha akitabasamu pale kitandani akamuuliza Sam kwa sauti ya kimahaba,
"Makosa gani hayo?"
Ila kabla Sam hajajibu, tayari Ritha alishainuka na kumfata Sam alipo kisha kuanza kumpapasa katika mwili wake na kumnong'oneza kwa sauti laini kabisa hata Sam nae akalainika,
"Usiwe na tatizo mpenzi, mi ndio tiba yako"
Maneno ya Ritha yalimuingia vizuri Sam na kujikuta akikubali,
"Ila Ritha kama hii ni tiba kwangu basi ngoja nifanye"
Ritha akataka kumvua Sam nguo ila Sam akapinga na kumwambia Ritha,
"Tafadhari tuzime taa kwanza"
"Hilo si tatizo"
Ritha alihisi kuwa huenda Sam anaona aibu, na kwenda mwenyewe kuzima taa na kuhakikisha mlango kuwa umefungwa vyema, kisha akarudi alipo Sam na kuendelea na zoezi lake.
Muda kidogo Ritha alitoa kelele ya juu na kufanya watu karibu wote kwenye hoteli ile kushtuka na gafla ile kelele haikusikika kabisa.
Moja kwa moja Ritha alikuwa amezimia na Sam kumalizia shughuli yake.
Sam alipomaliza alijilaumu sana kwa kitendo kile alichomfanyia Ritha kwani alijua wazi kuwa na huyo lazima atafata nyayo za wakina Neema.
Alijikuta akijipiga piga mwenyewe kwani hata msiba wa Neema haujapita huku wa mwingine ukinukia.
"Hivi hawa wasichana wana majini au ni nini jamani? Mbona kunipa dhambi nisiyotaka kuitenda kila siku? Mbona wakinifanyia hivi? Mbona Sabrina hajawahi kuyatenda haya ingawa nimeishi nae, tuseme ni mshamba wa mapenzi au ni kitu gani? Nakumbuka nilipokuwa nikimwambia tusubiri alikuwa akichukia tu na kununa. Inakuwaje kwa hawa? Na kipi kinanivuta hivi hadi natenda mambo yasiyo stahiki?"
Sam alijiuliza maswali bila majibu huku akimtazama Ritha pale alipozimia na kupanga jinsi ya kutoka naye pale hotelini.
Sam akapata wazo la kusema kuwa amezidiwa ili aweze kumkimbiza hospitali na iwe njia moja wapo ya kuondoka naye pale hospitali.
Cha kwanza kabisa alifuta damu iliyokuwepo pale chini kisha kumvalisha nguo Ritha na kumbeba begani kisha kutoka naye.
Mlinzi wa ile hoteli aliwaona ila akajua ndio mahaba ya kileo na pia hakuweza kufatilia zaidi kwani alimtambua kuwa ni Sam na anatambua ni jinsi gani anavyopatana na mabosi wao.
Sam alimpakiza Ritha kwenye gari kisha kuondoa gari eneo lile huku akifikiria pa kwenda naye, hapakuwa na mahari pengine pa kwenda zaidi ya nyumbani kwake ili amsikilizie Ritha atakapozinduka.
Alifika na kuingia nae vizuri ndani kisha akamlaza kwenye kiti pale sebleni na hakutaka hata ashtuke muda huo kwani alijua wazi kuwa lazima angefanya fujo.
ITAENDELEA
No comments: