Simulizi: Je haya Ni mapenzi? Sehemu ya Ishirini Na Tatu (23)

Usahili ulivyoisha, Sam akamuita Jeff na kwenda naye kwenye baa ya pembeni ili kuzungumza naye kama alivyokuwa amepanga awali.
"Eeh Jeff, niambie kwanini umeamua kutafuta kazi"
"Nataka kupambana na maisha"
"Kwanini usingemaliza kusoma kwanza? Yani kama ungemaliza tu mi ningekuajili kwenye kampuni yangu moja kwa moja, kwanini sasa umeamua kutafuta kazi kwanza?"
"Nina majukumu tayari, kuna mwanamke anaujauzito wangu"
"Hivi kumbe alivyoniambia siku ile Sabrina ni kweli? Mwanamke gani huyo?"
"Tena huyo huyo Sabrina ndio ana........"
Sabrina akatokea mbele yao, na kufanya wote wawili wamuangalie.

"Hivi kumbe alivyoniambia siku ile Sabrina ni kweli?
Mwanamke gani huyo?"
"Tena huyo huyo Sabrina ndio ana........"
Sabrina akatokea mbele yao, na kufanya wote
wawili wamuangalie.
Jeff akainama chini kwa aibu, kisha Sam akamgeukia Jeff na kumuangalia, halafu akamwambia
"Endelea kusema, Sabrina ana nini?"
Jeff akainua kichwa na kumtazama Sabrina.
Akaiona sura ya Sabrina ilivyojawa na mashaka, Jeff akashikwa na kigugumizi kilichofanya ashindwe kuongea zaidi.
Sam akamshtua tena pale Jeff,
"Vipi mbona kimya cha gafla huongei tena?"
Sabrina nae akasogea karibu yao na kumfanya Jeff apate ujasiri wa kuongea kiasi ingawa aliongea pale alipoulizwa tena na Sam,
"Sema sasa, Sabrina ana nini?"
"Sabrina ndio huwa ananikataza nisiseme hovyo kwavile naweza kufungwa ukizingatia yule mtoto mwenyewe ni mtoto wa mwanajeshi"
Sabrina hakuamini kama Jeff angeweza kutunga maneno kiasi hicho, alitamani hata ampongeze ila alisita kwavile alihisi kuwa huenda Sam akagundua ukweli.
Akavuta kiti na kukaa, halafu Sam akamuuliza Sabrina,
"Si nilikwambia upumzike wewe! Sasa mbona umekuj a?"
"Nimekumiss sana ndiomana, sikuweza kuvumilia nyumbani nikikusubiri ndiomana nikaamua nikufate tu"
Sam akatabasamu na kuona sasa kazi kwake imepungua ukizingatia tayari Sabrina kampenda mwenyewe.
Kisha akamwambia Sabrina,
"Nilikuwa naongea na huyu mtoto hapa kuwa kwanini anatafuta kazi kwavile nimemkuta akiwa ni miongoni mwa watu niliokuwa nawasahili"
"Hata mi nimeambiwa na mama yake, ila sikujua kama yupo huku. Basi hili halina tatizo, nitazungumza nae mimi mwenyewe."
Kisha Sabrina akamwangalia Jeff na kutoa funguo kwenye mkoba wake na kumkabidhi,
"Shika hizo funguo uende nyumbani kwangu leo, ili nikirudi nije tuongee vizuri."
"Sawa mamdogo"
Jeff aliitikia bila hata kusita,
"Ila tafadhari sana kuwa makini na nyumba yangu, tena usitoke toke kabisa usije kuniletea balaa mie"
Jeff akaitikia kwa kichwa na kuondoka.
Sam akamuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Mbona umemuondoa huyu mtoto hata kabla sijamaliza mazungumzo naye?"
"Mwache aende bhana, mi nitazungumza nae nyumbani. Jamani Sam nimekumiss sasa huyu mtoto angefanya tushindwe kuzungumza vizuri mpenzi. Au hupendi uwepo wangu niondoke?"
Sabrina akatishia kama kuondoka,
"Hapana sio hivyo mpenzi, napenda sana uwepo wako tena nakupenda sana"
Kisha Sam akamkumbatia Sabrina na kumkalisha tena eneo lile huku wakiongea mawili matatu.
Baada ya muda kidogo, Sam akamshauri Sabrina kuwa akubali kubadilisha eneo naye Sabrina akakubali na wakaondoka pale kuelekea sehemu nyingine.

Walipofika eneo ambalo walipenda kukaa, walimuona Joy akiwa amekaa na kijana wa tofauti.
Kisha Sabrina akamuuliza Sam,
"Yule si dada yako Joy yule?"
"Ndio ni yeye"
"Na yule kijana ni nani?"
"Kwakweli simjui"
"Mmh! Huyu dada yako hajatulia Sam, yani hajatulia kabisa. Si amevishwa pete ya uchumba na kaka yangu juzi tu hapo halafu leo kakaa na mkaka mwingine!"
"Huwezi jua, labda wapo kwenye mazungumzo ya kibiashara"
"Mmh! Wewe mtetee tu ila nitaona mwisho wake leo, twende tukakae pale"
Sabrina alimuonyesha eneo Sam ambapo waliongozana na kwenda kukaa ila macho ya Sabrina muda wote yalikuwa kwa Joy na kijana aliyekuwa amekaa naye.https://ift.tt/2TR5Sxj
Muda kidogo Joy na yule kijana wakainuka huku wameshika mikono wakielekea mahali, Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Si umeona? Mi nilijua tu ni kibwana chake kile, si unaona wanapoelekea? Kule kuna nyumba za kulala wageni"
Sam alikuwa kimya tu huku akimtazama Sabrina na kumfanya Sabrina aendelee kuongea,
"Nahisi hata ile mimba sio ya kaka yangu ndiomana alikuwa anaenda kuitoa"
Sam akaongea na yeye sasa,
"Tatizo lenu nyie wanawake wengi hamjatulia, huwa mnaponzwa na tamaa zenu"
"Kwahiyo hata mimi sijatulia?"
"Siwezi jua nyuma ya pazia"
Sabrina akakaa kimya na kujitafakarisha moyoni huku akijua wazi kama Sam atagundua kuwa na yeye ana mimba basi lazima atamuwek a kwenye kundi la wanawake ambao hawajatulia.
Roho yake ikahudhunika na kusononeka, kisha akamwambia Sam
"Tuondoke turudi nyumbani"
"Mbona gafla hivyo Sabrina?"
"Mi dada yako kashaichefua roho yangu, bora twende tu"
"Unataka ukamwambie kaka yako?"
"Lazima nimwambie ndio, huu ni upuuzi kwakweli. Tusije poteza hela ya mahari bure kwa mtu asiyemaana"
"Sabrina mpenzi wangu, usipende kuingilia mambo ya watu. Kama kweli atayashuhudia mwenyewe kwa macho yake, usipende kuwa chanzo cha kuachana kwao"
"Mmh! Unamtetea sana wewe, ila kaka yangu lazima nimwambie"
Sam akamwangalia tu Sabrina bila ya kuongezea neno lolote, Sabrina nae alipoona Sam asemi chochote akainuka na kuanza kuelekea upande ule ambao Joy alielekea na yule kijana.
Sam akainuka na kuanza kumuita Sabrina ili arudi,
"Wee Sabrina, sasa wapi huko jamani. Njoo tuondoke sasa"
Sabrina hakugeuka nyuma, aliendelea kwenda huku akijisemea,
"Kama angetaka tuondoke basi muda ule ule niliomwambia angeinuka ili twende ila yeye kajifanya kiburi, na lazima nikamuharibie dada yake"
Sabrina aliendelea mbele huku Sam akimfata nyuma ili kumuwahi.

Sabrina alipofika kwenye ile nyumba ya kulala wageni na kuingia ndani moja kwa moja, akamuona Joy na yule kijana wakielekea kwenye chumba na kumuita Joy kwa nguvu,
"Eeh Joy nimekuona tena kwa macho yangu, sasa ngoja matokeo"
Joy akarudi nyuma na kumfata Sabrina,
"Jamani Sabrina mbona hivyo? Sina nia mbaya mimi na wala sina mahusiano na yuke kijana, tafadhari nakuomba usimwambie James"
Sabrina akayaiga yale maneno ya Joy kwa kubana pua moja juu,
"Eti tafadhari usimwambie James, nyooo namwambia kila kitu, la sivyo ondoka hapa sasa hivi"
Joy aliondoka bila hata kumuaga yule kijana aliyekwenda naye eneo lile.
Kisha Sam akamvuta mkono Sabrina ili waondoke eneo lile.
Alimvuta hadi kwenye gari yake kisha wakapanda na safari ya kumrudisha Sabrina nyumbani kwake ikawadia.
Walitembea kimya kimya kwenye gari hadi walipofika nyumbani kwa Sabrina.

Walifika, wakafungua mlango na kuingia ndani.
Sabrina akamuita Jeff ila Jeff hakuitika na kumfanya Sabrina atambue kwamba Jeff hakuwepo ndani,
"Umeona hili litoto sasa, limeondoka na kuacha mlango wangu wazi"
Sam akamwambia Sabrina,
"Ila wewe na huyo mtoto mnajuana wenyewe, ngoja nikuache upumzike"
"Haya mpenzi, kwaheri"
"Sawa, najua sasa moyo wako umeridhika"
Kisha Sam akambusu Sabrina kwenye paji la uso na kuondoka.
Kisha Sabrina akaendelea kujitafakarisha alipoenda Jeff,
"Sijui kaenda wapi kwakweli, yani huyu mtoto ananiumiza kichwa sijapata kuona maisha yangu yote."
Akainuka na kwenda kufunga mlango wake na funguo zilizokuwa zikining'inia pale mlangoni ili Jeff akirudi agonge mlango.
Alipomaliza kufunga na kurudi kukaa, akamuona Jeff nae amekaa kwenye kochi, ilibaki kidogo tu Sabrina aanze kupiga kelele.
Jeff akacheka na kumuomba Sabrina amsamehe,
"Inamaana ulijificha humu ndani?"
"Nilifanya hivyo ili yule bamdogo aamini yale maneno yako ambayo huwa unamwambia kuwa mimi situlii nyumbani"
Sabrina alitikisa tu kichwa chake na kusema,
"Kwakweli wewe Jeff wewe sijui hata akili zako zilivyo"
Kisha akakaa chini ili kuweza kuzungumza na Jeff.
"Jeff nakuomba unisikilize haya machache tu ninayotaka kuzungumza na wewe"
"Niambie tu hata usijali"
"Najua unatambua wazi kama umenikosea sana tena sana"
"Natambua hilo, na pia nakiri makosa yangu. Najua inakuwa ngumu kunisamehe ila nakuomba unisamehe"
"Nilishakusamehe Jeff najua ni akili ya balehe ndio iliyokutuma vile, ingawa moyo wangu uliumia sana na kufadhaika, hata sasa naumia ila nilishakusamehe. Lakini naomba unisaidie jambo moja tu"
"Jambo gani hilo?"
"Nakuomba hii mimba ibaki kuwa siri baina yako na yangu, sitaki mtu yeyote yule ajue kuhusu hii mimba. Mie tumbo likijitokeza kiasi hata cha mtoto mdogo kujua, nitawaambia nyumbani kuwa nilibakwa kwahiyo baba mtoto simjui. Tafadhari Jeff naomba iwe siri"
"Inamaana hata huyo mtoto asitambue kamwe kama mimi ni baba yake? Nitaweza kweli? Najua nimetenda dhambi kwako ila yote ni sababu nakupenda ingawa hutaki kukubaliana na upendo wangu kwako"
"Sasa hapo ndipo unaponichefua, tafadhari. Mambo ya kunipenda weka kando na unisaidie kwa hili"
"Mmmh!"
"Usigune Jeff tafadhari, hebu wewe jaribu kukaa katika nafasi yangu na uangalie maumivu niyapatayo. Angalia jinsi walimwengu wakijua ukweli aibu nitakayoipata! Angalia na utafakari Jeff, nimekulea kama mwanangu wa kuzaa kabisa, halafu leo hii jamii igundue nimezaa na wewe, hivi hii sura yangu mimi nitaiweka wapi? Tafadhari Jeff nihurumie, mimi nimekusamehe naomba na wewe unisaidie kwa hili"
Jeff aliamua kukubali ili aweze kumfurahisha Sabrina, na kufanya waingie katika makubaliano ya kufanya hiko kitu kiwe siri siku zote.
"Mimi nimekubali ila kwa sharti moja"
"Sharti gani hilo?"
"Naomba nikae kwako ili niwe nakuona kila siku maana mimi furaha yangu ni kukuona wewe"
"Basi sawa, hilo sio tatizo ila na mimi ombi langu jingine ni kuwa uachane na swala la kutafuta kazi na umalizie kwanza elimu yako sawa!"
"Sawa, ila ningependa kukusaidia katika kulea huyo mtoto"
"Usijali kuhusu hili, najua cha kufanya wala usipate tabu. Ila wewe usome"
Sabrina alimaliza kuongea na Jeff na kushukuru kueleweka kwake ili ile mimba yake na mtoto atakapojifungua ibaki kuwa siri yake na Jeff tu.

Siku ya leo Sabrina alilala akiwa ameridhika moyoni mwake, alijiona sasa anaweza panga mipango mingine kwa ufasaha zaidi ili kuepuka wasiwasi na mashaka yampatayo kila siku.
Kulipokucha siku hiyo, kwavile ilikuwa mwisho wa wiki, Sabrina akajiandaa na kwenda kumtembelea mama yake.

Kama kawaida alimkuta mama yake akiendelea na kazi zake za hapa na pale.
Sabrina akamsalimia mama yake na kuanza kumueleza shida zake,
"Halafu wewe Sabrina uliniambia kuwa una mimba, mbona hukuniambia kama ni ya Sam au la"
"Hicho ndio kitu kilichonileta mama, ni kweli nina mimba ila sitaki umwambie Sam sababu nataka nimfanyie surprise."
"Khee mwanangu kumbe una mimba kweli! Dah kweli Mungu mkubwa sana, na harusi inanukia"
"Ndio mama, ila naona baba anachelewa sana kurudi. Hivi mashangazi hawawezi kuja wao ili wawe na wewe mpokee hiyo mahari mama ili mimi nikaishi kwa mume wangu?"
"Inawezekana, ila inatakiwa baba yako akubali. Sasa kwa ushauri wangu, nenda kwa yule shangazi yako ambaye ni wajina wako, mshawishi yule. Yani yule akikubali tu mambo yametiki, kwakuwa yule anapatana sana na baba yenu"
Sabrina akaona wazi kuwa ushauri aliopewa na mama yake ni mzuri zaidi na akaona ni vyema afanye hivyo ili waweze kuharakisha mambo ya ndoa, ili yafanyike haraka.
"Basi mama naenda leo leo"
"Sawa mwanangu, hakuna tatizo"
Sabrina akamuaga mama yake na kuondoka kuelekea huko kwa shangazi yake.

Alipofika alimkuta shangazi yake akiwa mwenyewe tu na kuona ni afadhari ili aweze kumweleza aliyonayo kwa uhuru zaidi.
Alimsalimia na kuanza maongezi naye, alimwelezea lengo lake na shangazi yake akamuelewa ila akamuuliza,
"Mbona unataka kuharakisha hivyo hiyo ndoa?"
"Si unajua shangazi vijana mambo ni mengi, bora kuharakisha"
"Sabrina wewe una mimba"
Sabrina akashtuka na kumuuliza shangazi yake,
"Umejuaje?"
"Mimi ni mtu mzima Sabrina na nimepitia mambo mengi, nina utambuzi mkubwa sana"
"Ndio nina mimba shangazi ndiomana nataka kuolewa mapema ili nikazalie ndani ya ndoa"
Shangazi akatikisa kichwa kama ishara ya kusikitika na kusema,
"Kweli nimeamini maji hufata mkondo, Sabrina unataka kufanya kitendo alichofanyaga mama yako miaka ya nyuma iliyopita"
"Kitendo gani hicho?"
"Sabrina unataka kumbambika mimba mtu asiyehusika, unajua wazi kabisa kuwa huyo mwanaume anayetaka kukuoa sio muhusika wa hiyo mimba"
Sabrina akashtuka sana na kumuuliza shangazi yake,
"Inamaana wewe unamjua muhusika?"
Shangazi yake akaanza kucheka na kumfanya Sabrina kujawa na wasiwasi.

Inaendeleaaa



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.