Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi Sehemu Ya Ishirini Na Mbili (22)

Siku hiyo hadi giza linaingia Sam alikuwa bado k wa Sabrina ingawa alitoka mapema ofisini lakini hadi usiku unaingia bado alikuwa kwa Sabrina, na muda mwingi alikuwa kimya huku akitafakari mambo mbali mbali kwenye akili yake.
Sabrina alitaka kwenda kupika,
"Hapana Sabrina unaumwa usiende kupika, sema unachojisikia kula nikakuletee"
"Labda chips mayai ila zikauke sana"
"Hakuna tatizo"
Sam akainuka na kwenda kumnunulia Sabrina chakula.
Wakati Sam ameondoka tu, mlango wa Sabrina ukagongwa.
Alipokwenda kufungua alimkuta Japhet pale mlangoni na kumfanya Sabrina achukie, ila Japhet aliingia moja kwa moja mpaka ndani.
"Hivi wewe Japhet wewe una shida gani na mimi jamani? Kwanini unapenda kunisumbua wewe jamani? Haya niambie umefata nini?"
"Jana si nilikupigia simu na kukwambia kuwa leo nakuja? Si ndio nimekuja sasa."
Hapa Sabrina akakumbuka kuwa simu aliyopigiwa jana yake na namba mpya ndio ilikuwa ya huyu Jeff.
"Sasa umekuja kufanya nini?"
"Nimekuja kulala hapa kwako leo mpaka ukubali kunisamehe na kurudiana na mimi Sabrina"
"Jamani Japhet, mi nilishakusamehe kitambo sana. Ila kurudiana na wewe sitaweza sababu nina mchumba tayari, sitaweza kuwa na wewe Japhet"
"Tafadhari Sabrina nihurumie, nakupenda sana. Nahitaji kuoa ila sijamuona mwanamke anayefaa kuwa mke wangu zaidi yako Sabrina, tafadhari kubali uwe wangu nakuomba"
"Siwezi Japhet, siwezi kabisa nawe nielewe tafadhari"
Japhet hakutaka kuondoka bado alimng'ang'aniza Sabrina juu ya swala la kumpenda sana.
Sabrina alijitahidi kwa kila njia kumfanya Japhet amuelewe ila bado alikuwa mgumu na aligoma kutoka mule ndani.

Muda Sam anarudi akasikia mzozo baina ya Sabrina na sauti ya kiume, akajikuta akitawaliwa na roho ya wivu katika moyo wake.
Alipoingia akamkuta Japhet amepiga magoti mbele ya Sabrina akimuomba msamaha, Sam kwa hasira akatoa bastora yake ambayo hupenda kutembea nayo siku zote.
Sabrina kuona vile akaamua kukaa mbele ya Japhet kumkinga huku akimsihi Sam airudishe ile bastora.
"Tafadhari Sam nakuomba, nakuomba sana mpenzi wangu usifanye chochote"
"Sabrina niache nimmalize huyo mjinga maana namuona tu akikusumbua kila siku"
"Nakuomba Sam, shusha hiyo chini tafadhari"
Sabrina akajaribu kumsogelea Sam ili kumzuia asimpige Japhet, na muda huo Jeff nae alifika na kufungua mlango, akapatwa na mshangao kwa lile tukio na kumfanya Japhet nae apate upenyo wa kukimbia.
Jeff aliendelea kushangaa huku akimuangalia jinsi Sam anavyotulizwa pale na Sabrina ili asifanye mambo ya ajabu.
"Ungeniachia yule ng'ombe nimmalize mie yani yule tena asirudie tena kuja hapa"
Halafu Sam akamuangalia Jeff na kumwambia,
"Tena ukimuona mtu yeyote anamsumbua mke wangu hapa unipe taarifa, mi nitamaliza watu mimi huwa sipendi ujinga"
Jeff hakujibu kitu ila alimuangalia Sabrina na kumwambia,
"Nimepita kukuaga mamdogo, kwahe ri"
Tena hata hakusubiri Sabrina ajibu kwani alitoka nje na kuondoka.

Sabrina alitulia huku akimuangalia Sam bila hata ya kumaliza kumtafakari alivyo.
"Chipsi ulizotaka hizo hapo, ule sasa"
Sabrina alichukua zile chipsi ili ale, ila alipokula kidogo tu akajihisi vibaya na kwenda kutapika.
Sam akamuonea huruma sana Sabrina,
"Pole sana, itabidi leo nibaki hapa kukuangalia mpenzi wangu jamani"
"Hapana Sam, usijali juu ya hilo. Mi nitakuwa sawa tu mpenzi wangu. Usiwe na shaka tafadhari"
"Hapana, siwezi kuondoka na kukuacha na hiyo hali. Au basi nikupeleke kwenu ili ukapate uangalizi wa karibu toka kwa mama yako"
Sabrina akafikiria na kukataa huku akiendelea kumsisitizia Sam kuwa atakuwa sawa tu huku akili yake ikiendelea kupanga mipango mingine.
"Kama ndio hivyo basi mimi leo siondoki kwakweli, nitalala hapa hapa hadi nihakikishe afya yako iko vizuri"
"Basi sawa, bora tu ulale hapa hapa"
Moyo wa Sabrina ukaridhia kuwa Sam alale pale ili ajaribu kufanya kitu cha kuokoa uchumba wao.

Muda wa kulala ulipofika, Sam akataka kulala pale kwenye kochi.
"Sio vizuri bhana Sam, utalalaje kwenye kochi wakati vitanda vipo"
"Kwahiyo nikalale kwenye chumba cha Jeff?"
"Hapana bhana, chumba chetu kipo twende tukalale chumbani"
"Kumbuka bado sijakuoa Sabrina!"
"Hilo sio tatizo Sam, si tunalala tu jamani kwani tatizo liko wapi wakati ni kulala tu?"
Ikabidi Sam akubaliane na Sabrina na kwenda chumbani kulala.
Walipofika kitandani, Sam akachukua shuka akajifunika na kulala.
Sabrina akamuangalia Sam bila kummaliza, akajiuliza kimoyomoyo
"Hivi huyu ni mwanaume kweli? Au ananitega tu? Mwanaume gani hata hajali kama amelala na mwanamke? Hata kama ndoa bado mbona wengine huwa wanafanya tu kwanini huyu jamani? Mbona ananitesa mie"
Sabrina alimuangalia Sam kwa jicho la hasira sana na kujaribu kulala ila hakupata usingizi.
Akaamua kuuchukua mkono wake na kuupitisha kwenye kiuno cha Sam ili ajaribu kumpapasa papasa, ila Sam akamgeukia Sabrina na kumwambia,
"Kumbuka bado sijakuoa"
"Kwani kuna tatizo jamani Sam! Wewe si mchumba wangu jamani!"
"Ndio mimi ni mchumba wako, kwani unataka nini Sabrina?"
Ikabidi Sabrina ajitoe aibu na kumwambia,
"Nataka tufanye Sam"
"Si unaumwa wewe? Na si uliniambia hujawahi kufanya? Mbona unataka kuniletea makubwa Sabrina jamani! Nakuheshimu sana, sitaki kukuchezea ndiomana nangoja tufunge ndoa kwanza"
Sabrina alitamani hata kulia kwa majibu ya Sam ila hakujua afanye nini, na kuendelea tena kumpapasa.
"Tafadhari Sam nakuomba tufanye leo tu tafadhari"
"Hapana Sabrina, usitake kunipa dhambi muda huu. Ni mengi niliyafanya hapo zamani ila siku hizi nimebadilika, nakuheshimu sana tena nakupenda sana"
Sam akainuka na kwenda sebleni kukaa kwenye kochi, Sabrina akajisikia aibu sana kwa kushindwa kumshawi shi Sam kulala naye.
Akajikuta akikaa tu pale pale chumbani kwa hasira.

Palipokucha, Sam akaingia kwenye chumba cha Sabrina na kumuaga.
Ingawa Sabrina alikuwa amenuna, ila Sam hakujali.
Alienda na kumbusu kwenye paji la uso kisha akamuaga na kuondoka kuelekea kwake kwaajili ya kujiandaa kwenda kazini kwake.
Sabrina alibaki na hasira sana huku akimchukia Sam waziwazi kabisa.
Naye akainuka na kujiandaa kwa lengo la kwenda kuzungumza na mama yake nyumbani kwao.

Alipokuwa kwenye daladala kuelekea kwao, alikuwa amekaa siti ya nyuma ambako alipakana na wadada watatu ambao mazungumzo yao yalimfanya Sabrina atege sana sikio kwao,
"Hivi jamani kuna mwanamke kweli anayeshindwa kumtega mwanaume hadi akaingia laini?"
"Mmh labda huyo mwanamke wa kijijini, watoto wa mjini sie hakuna mwanaume anayeweza kupingua"
"Umeona eeh! Sie wadada tuna vivutio vyote vya kuwapata wanaume. Yani hakuna mwanaume wa kupingua kama kwan gu nikiamua kumuweka mwanaume kwenye kumi na nane zangu hawezi kupindua"
Wote watatu wakacheka, kisha mwingine akaendelea,
"Mi si ndio nimelishangaa zoba moja hivi, mi nimelivutia jamaa hadi ndani eti limeshindwa kumseti. Mimi sasa nilichokifanya jana jamani hadi yule kaka alipagawa"
"Eeh ulifanyaje shoga?"
"Basi yule kaka alipokuja, nikamkaribisha ndani. Halafu nikaenda kuoga kwa makusudi na kujifunga khanga ili inishike, sasa wakati......"
Konda akataja kituo nao wakamwambia ashushe, gari ikasimama na wakashuka.
Yani Sabrina akatamani hata ashuke nao ili na yeye asikilize kilichoendelea ila ndiohivyo tena walikuwa ni watu asiowafahamu ikabidi atulie tu.

Sam alipokuwa ofisini alifikiria sana kuhusu Sabrina,
"Ila siwezi kufanya hivi, lazima nitimize ahadi yangu kwa Sabrina na pia sitaki Sabrina ajue madhaifu yangu mapema kiasi hiki. Acha anichukie kwasasa ila ni lazima nimuoe kwanza."
Muda huo Joy nae alifika kwenye ofisi ya Sam kumsalimia na kujua kinachoendelea baina ya Sam na Sabrina.
"Niambie kaka, wifi yangu Sabrina anaendeleaje?"
"Anaendelea vizuri tu, ila Joy huwa sikuelewi kwakweli. Au ulidhania kuwa Sabrina ana mimba?"
"Sio nilidhania, huo ndio ukweli kaka"
Sam akamcheka Joyce na kumwambia,
"Usilolijua litakusumbua, wee nenda zako tu dada yangu"
Joy alikaa kimya baada ya kushushuliwa na kuamua kubadilisha mada kisha akaaga na kuondoka.

Jeff akiwa nyumbani kwao alikuwa akiwaza tu jinsi ambavyo Sam akigundua ukweli kitu atakachokifanya.
"Sijui kama Sabrina anaweza akamuachia anipige mimi na kuniua. Najua kuwa naye ananipenda ila tu anashindwa kuwa na mimi kwavile mimi ni bado mdogo."
Mama yake akamsikia akiongea peke yake,
"Mbona unaongea peke yako Jeff?"
"Aaah hapana ni muingiliano wa mawazo tu"
"Basi naomba nikutume kidogo"
Jeff akakubali kisha Sakina akampa Jeff mzigo ambao alihitaji aupeleke kwa mama wa Sabrina.

Sabrina alipofika nyumbani kwao, alimkuta mama yake na kuamua kukaa naye ili kumueleza yanayomsibu.
"Yani mama, hivi unionavyo hapa mwanao nina mimba."
Joy akashtuka sana na kumuuliza kwa mshangao,
"Una mimba! Ya nani?"
Akatokea Jeff na kudakia,
"Ni yangu"
Joyce akamuangalia Jeff kwa mshangao.

Joy akashtuka sana na kumuuliza kwa mshangao,
"Una mimba! Ya nani?"
Akatokea Jeff na kudakia,
"Ni yangu"
Joyce akamuangalia Jeff kwa mshangao.
Sabrina akainuka kwa hasira na kumzaba Jeff kibao, na ili kupotezea maana kwa mama yake akaanza kumwambia Jeff kwa ukari,
"Unafikiri kila muda ni masikhara tu, muone. Tena tuondokee hapa nisije nikakuharibu bure."
Jeff hakusema kitu zaidi ya kukabidhi ule mzigo aliyopewa,
"Mama kanipa nikuletee"
Kisha akaondoka zake.
Joy akamuangalia Sabrina aliyekuwa kavimbwa na hasira na kumwambia,
"Achana nae yule ni utoto tu unamsumbua ukizingatia ulishamzoesha matani tangu siku nyingi"
"Kamenikera sana, watu tunaongea mambo ya maana hapa halafu yeye analeta maneno ya kipuuzi"
"Msamehe bure mwanangu"
"Nishamsamehe tayari"
Sabrina alimjibu hivyo mama yake ila moyoni mwake bado alikuwa na chuki juu ya Jeff ukizingatia anaona kuvurugiwa mambo yake mengi na huyu Jeff.
"Basi tuendelee na maongezi yetu mwanangu"
"Subiri mama, ngoja nipumzishe akili yangu kidogo"
Sabrina akaamua kwenda kulala.

Alishtuliwa na simu yake ya mkononi, alipomuangalia mpigaji alikuwa ni Sam akaipokea na kuongea naye
"Uko wapi mpenzi?"
"Nipo nyumbani"
"Nyumbani ya wapi? Mbona huku haupo?"
"Aah samahani sikukwambia, nimekuja huku kwa mama"
"Basi nakuja"
Kisha Sam akakata simu na kumfanya Sabrina ainuke sasa na kumfata mama yake, ila akamkuta mama yake akiongea na Sakina,
"Yani akili za Jeff jamani hata sijui zikoje labda Sabrina ataweza kunisaidia"
"Ndio Sabrina ataweza sababu wanapatana sana, yani leo Sabrina alivyomnasa kibao Jeff nikajua atalalamika, ila wala alikuwa kimya kama sio yeye vile. Ila angepigwa na mtu mwingine sasa loh hilo balaa lake nisingeingilia"
Sakina akacheka na kuuliza,
"Kwani alifanya nini?"
Ikabidi Sabrina aingilie kati yale mazungumzo ili yasije chimbua na mambo mengine yaliyojificha nyuma ya pazia.
"Mwanao ni mjinga tu yule, eeh niambie dada yangu za siku?"
"Kumbe ulikuwa unatusikia Sabrina jamani, nimekukumbuka sana mdogo wangu"
Wakafurahi pale na maongezi mengine yakaendelea.
Huku Sabrina akijitahidi kukwepesha mada ya awali.
"Badae au kesho nitakuja kwako dada, nina mengi ya kuzungumza na wewe"
"Hakuna tatizo uje tu Sabrina"
Sakina akaaga pale na kuondoka.
Baada ya muda kidogo Sam naye akawasili pale nyumbani kwa wakina Sabrina na kumkuta Sabrina na mama yake.
Alipomsalimia tu mama yake Sabrina, hapo hapo Sabrina akadakia ili mama yake asiingizie khabari za mimba.
"Ndio umekuja kunipitia eeh, basi twende"
Kisha Sabrina akamgeukia mama yake na kumuaga,
"Mama, nitarudi badae. Kuna mahali naenda na Sam"
Ikabidi Sam akubaliane na maneno ya Sabrina kisha naye akaaga na kuondoka pamoja.

Walipokuwa kwenye gari, Sam akayaanza mazungumzo
"Ila Sabrina umenitoa kwenu haraka sana, nilitaka kuzungumza kidogo na mama yako"
"Ulitaka kuzungumza naye kuhusu nini?"
"Kuhusu harusi yetu Sabrina, unajua kwenu ndio wanachelewesha mambo."
"Usijali, utazungumza nae siku nyingine"
"Au umechukia usiku wa jana Sabrina?"
"Hapana, achana na hayo mambo ya usiku yalisha pita tayari"
"Sawa mpenzi"
Sam alikuwa akifata kile anachokisema Sabrina ili kuepuka kumkera.
"Sasa twende wapi muda huu?"
"Twende hata baharini kupunga upepo"
Ikabidi Sam ampeleke Sabrina mahali alipopataka.

Sakina aliporudi nyumbani kwake akamtania mtoto wake,
"Nasikia leo Sabrina kakuzabua hata hujalalamika"
Jeff akacheka na kumuuliza mama yake,
"Kwani wamekwambia kuwa chanzo ni nini?"
"Hata hawajaniambia, kwani chanzo ni nini?"
"Aah mambo ya Sabrina na mimi yaache kama yalivyo mama, utachanganyikiwa bure"
"Una maana gani Jeff?"
Jeff akambadilishia mada mama yake,
"Kesho naenda kufanya usahili kuna kazi nimeomba"
"Na shule je? Yani hapo ndio huwa unanichosha mwanangu jamani, kwanini huwa unapenda kubishana na mimi jamani? Nenda shule kwanza, halafu hayo mengine yatafata. Yani huyo mwanamke aliyekushika masikio huyo nikimjua wallah atanitambua"
Jeff akamuangalia mama yake na kutabasamu tu.

Sabrina akiwa ufukweni na Sam, walimuona Joy akiwa maeneo hayo pamoja na kaka wa Sabrina yani James, wakaamua kuungana nao ili waweze kubadilishana mawazo.
Waliwafata na kuwasalimia,
"Kumbe na nyie mpo huku?"
"Ndio, tupo kubadilishana mawazo tu"
Sabrina akamuuliza kaka yake,
"Eeh ndoa lini?"
"Ni hivi karibuni tu, tunamngoja baba arudi ili niweze kuambatana naye pamoja na mama kwenda kutoa mahari na mshenga wangu"
"Basi vizuri, na sisi tunamngoja baba arudi ili Sam akanitolee mahari nyumbani. Si ndio hivyo Sam wangu!"
Sam akatikisa kichwa huku akitabasamu, muda huo wote Joy alikuwa kimya kabisa na hakuchangia chochote hadi wanaondoka eneo lile.
Ikabidi Sabrina amuulize Sam,
"Mbona vile dada yako, ana matatizo gani kwani?"
"Achana nae yule ana kisirani tu, nilimshushua alipokuja ofisini kwangu kuleta umbeya."
"Aaah kumbe!"
"Mi huwa sipendi maneno ya kuambiwa na watu, napenda kitu nikishuhudie mwenyewe ili hata kama nikichukua hatua basi nichukue hatua kihalali"
"Nimekuelewa"
"Kesho ni Jumamosi, ni siku fupi kwa kazi yetu. Je utaenda ofisini?"
"Naendelea vizuri kwasasa, kwahiyo nitaenda"
"Basi nitakupitia twende ila mi sitakaa ofisini, kuna mahali naenda kuwafanyia vijana usaili wa kazi"
Sabrina hakuwa na tatizo kwani anaelewa wazi kuwa Sam anamiliki vitengo mbali mbali na ndiomana ana pesa za kufanyia chochote atakacho.

Wakapanda kwenye gari kwaajili ya safari ya kurudi nyumbani kwa Sabrina kwanza.
Wakati wapo kwenye gari, Sam akamuuliza kitu Sabrina,
"Utajisikiaje siku ukiwa na mimba yangu?"
Sabrina akashtuka sana na kupumua kidogo kisha akamjibu Sam,
"Nitakuwa na furaha sana yani kupita maelezo ya kawaida"
"Kama ni hivyo basi itakuwa vizuri, naomba nikua hidi kitu Sabrina"
"Kitu gani hicho?"
"Siku utakapokuwa na mimba yangu napenda uniambie ni gari gani utapenda nikununulie ili iwe inakupeleka kliniki."
Sabrina alikuwa akimsikiliza Sam huku moyo wake ukiugua kwa maumivu makali na kumfanya hata atamani kurudisha siku nyuma ili awe salama.
"Ukiwa na mimba yangu, sitapenda uteseke na kazi. Sitapenda uwe na mawazo, ndiomana nataka nikuoe kwanza kabla ya mambo yote"
Sabrina alihisi kuchefuka tu na haya maneno ya Sam na kuamua kumbadilishia mada,
"Hivi bado hatujafika kwangu kweli!"
"Tunakaribia kufika usijari"
"Yani nimechoka halafu nina usingizi sana, nikifika tu ni kulala"
Sam akamuangalia Sabrina bila ya kusema chochote kile cha zaidi na kuendelea na safari.

Sabrina alipofika akamuaga Sam na kushuka huku akidai kuwa ana usingizi sana, hivyobasi alihitaji kwenda kupumzika.
Kwahiyo Sam akaamua kurudi nyumbani kwake tu na yeye.
Sabrina alikaa na kuilaumu sana ile mimba, alitamani kama isingekuwepo kwenye tumbo lake.
Ila ndio tayari ilishakuwa kwake.
Akaamua kulala tu kama alivyopanga kuwa amechoka, ila kabla hajalala akapigiwa simu, kuangalia mpigaji alikuwa ni Jeff,
"Sijui kanataka nini usiku huu"
Alipokea ile simu huku akiwa ameshapandwa na hasira tayari, ila iliongea sauti ya kike na alipoisikilizia ilikuwa ni sauti ya Sakina,
"Sabrina nakuomba kesho uje nyumbani kwangu kama utapata muda"
"Hakuna tatizo, nilishakuahidi kwahiyo lazima nitakuja"
"Sawa basi usiku mwema"
"Nawe pia"
Akakata simu na kuiweka pembeni, mara ikaita tena alipoiangalia ni namba ya Jeff akajua ni Sakina,
"Sijui kasahau kuniambia kitu gani"
Akaipokea ile simu ila sasa aliongea Jeff,
"Na mimi naomba nikutakie usiku mwema"
"Kwenda zako, usiniletee balaa mie"
"Sawa, ila kuna kitu nataka kukwambia"
"Kitu gani?"
"Mimi ndio yule Prince J niliyekuwa nakusumbua kipindi kile kwenye Facebook"
"Nyoko zako wewe"
Sabrina akaikata ile simu kwa hasira na kujisemea,
"Hivi huyu mtoto huyu ananitafutia kitu gani mimi jamani! Kwanini mimi, kwanini nikose raha sababu ya mtu mmoja? Aaaah, sijui kwakweli."
Sabrina akatafuta usingizi kwa lazima ila ukakawia kuja sababu ya mawazo aliyokuwa nayo kwa muda huo.

Usingizi ukampitia, akajiona anaolewa.
Amevaa shela zuri sana, na Sam nae kavaa suti nzuri sana.
Watu wengi wamejaa kushuhudia ndoa yao, ila wakati Mchungaji anataka kuwafungisha ndoa, akatokea Jeff na kusema,
"Ana mimba yangu huyu"
Sabrina akashtuka pale pale kutoka usingizini, alikaa chini na kujikuta akilia kwa uchungu huku roho yake ikimuuma sana na kuilaumu ile mimba pamoja na kiumbe alichonacho kwenye tumbo lake, akajikuta akisema
"Ewe mtoto uliye kwenye hili tumbo langu, tafadhari kama unanihurumia mama yako jitoe mwenyewe. Naumia mimi, sina raha, sina amani, sina furaha. Unafikiri nitakupenda kweli wakati umeharibu maisha yangu kiasi hiki? Tafadhari nihurumie ili niepukane na hii fedhea"
Alikuwa akiongea kamavile anaongea na mtu pembeni yake kumbe anaongea na mimba yake.
Na hakulala tena hadi palipokucha.

Kama kawaida, Sam alimfata Sabrina kwaajili ya kwenda kazini.
Walipokuwa kwenye gari Sabrina akampa hoja Sam,
"Baba anarudi wiki ijayo, unaonaje sasa wiki hiyo uje utoe mahali na tufunge ndoa kabisa"
"Ni jambo linalowezekana kabisa tena lipo ndani ya uwezo wangu. Ila kwanini tufanye haraka kiasi hicho? Ni kitu gani tunakimbilia?"
"Hivi wewe Sam hupendi kuishi nyumba moja na mimi? Hupendi kula na mimi? Kuoga pamoja na kulala wote hupendi?"
"Sabrina, yote haya nafanya kwa kufata ushauri wako. Unakumbuka siku ile niliyokuomba ukalale kwangu? Japo kwa maongezi tu? Ukagoma, nikakurudisha nyumbani ila ukaenda kulala unapopajua wewe ila kwavile nakupenda sijakuhoji hadi leo. Unadhani mimi sikuumia? Au unadhani nina moyo wa chuma ambao haupenyezi maumivu? Nataka tupate muda mzuri wa kufahamiana, swala la kutoa mahari sio tatizo kwangu, kwahiyo nitaitoa tu. Na swala la ndoa pia sio tatizo kwangu, kwahiyo nitakuoa tu ila sio kuharakisha kiasi hicho"
"Kwahiyo Sam umeamua kunilipizia eeh"
"Hapana, sio kukulipizia. Ila hatuwezi kuharakisha kiasi hicho kwakweli"
Sabrina alikaa kimya kwani alijua wazi kuwa hata kama akiendelea kuongea ni kazi bure.

Walifika ofisini, Sam akamuacha Sabrina pale ofisini na kuondoka zake mahali alipotakiwa.
Kisha Sabrina akaendelea na kazi, muda ulipofika tu wa kutoka, akaondoka kwaajili ya kwenda nyumbani kwa Sakina.
Njiani akakutana na Fredy ambaye alimpa taarifa ambayo hakuijua.
"Francis anaoa mwezi ujao"
"Nini? Francis anaoa?"
"Ndio anaoa"
"Mbona hakuniambia?"
"Atakuja tu kukwambia mwenyewe"
Wakaagana pale huku Sabrina akipata mawazo kuwa bora angekuwa na Francis labda ndio ungekuwa muda wake wa kuolewa.
Aliachana na Fredy pale huku akiwa na mawazo tu.

Alifika nyumbani kwa Sakina na kumkuta, wakasalimiana ila hoja kubwa ilikuwa ni kuhusu Jeff,
"Yani Sabrina, huyu mtoto Jeff hataki kusoma tena eti anataka kufanya kazi. Majibu ya kidato cha sita yalishatoka na amefanya vizuri tu ila hataki kusoma anataka kufanya kazi"
"Umejaribu kumuhoji kuwa kwanini anafanya hivyo?"
"Huwa haeleweki, sijui anataka kuoa na umri ule jamani si kuniletea mizigo tu mimi hapa, na wasichana wote ninaomletea mimi hawataki, hata sijui anamtaka nani"
"Sasa mimi nitajaribu kuongea nae, yuko wapi kwani?"
"Kaenda kwenye usaili wa kazi huko"
"Sehemu gani?"
Sakina akamtajia Sabrina na kumfanya moyo umlipuke kwani alijua wazi ndio huko ambako Sam alisema kuwa kuna watu anatakiwa akawafanyie usahili,
"Vipi Sabrina, unapajua eneo lenyewe?"
"Ndio napajua, ila ngoja kidogo niwasiliane na mtu fulani"
Sabrina akainuka na kwenda pembeni kisha akampigia simu Sam,
"Uko wapi?"
"Si ndio nipo huku kuwasahili watu bhana, ila nimekaona na kaJeff hapa na yeye anataka kazi"
Sabrina akapumua kidogo baada ya kugundua kuwa alikuwa anahisia kitu cha kweli.
"Ukitoka hapo unaenda wapi?"
"Nikitoka hapa, kuna baa pembeni nataka nikae na huyu bwana mdogo Jeff nizungumze nae mawili matatu"
"Vipi na mimi nije?"
"Hapana, usiwe na shaka nitakufata badae"
Kisha akakata simu, Sabrina akarudi kuongea na Sakina ila havikukalika akaamua kumuaga na kumuahidi kurudi badae.
"Mbona gafla hivyo Sabrina?"
"Kuna mtu nataka nikamuwahi kidogo"
Hakutaka hata kupoteza muda, akatoka na kuondoka.

Inaendeleeaaah.......



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.