Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? sehemu ya ishirini na moja (21)


Kulipokucha, kama kawaida Sam alimfata Sabrina kwao na safari ya kwanza ilikuwa kwenda kumuona Jeff na kisha kumuona Fredy.

Jeff leo alikuwa vizuri na aliweza hata kukaa na alifurahi sana kumuona Sabrina.
"Siamini kama nakuona tena mamy"
"Usijali nilipona"
Sabrina hakutaka Jeff azungumze zaidi kwa kuhofia kuwa atasema mengi na kumuharibia kwa Sam.
Kwahiyo wakaongea nae kidogo tu kisha wakamuaga na kuondoka.

Walipofika kwa Fredy hali yake ilikuwa ni nzuri pia.
"Leo wanaweza kuniruhusu nirudi nyumbani"
"Pole sana Fredy"
"Asante Sabrina"
"Najua umeumia kwa kuniokoa mimi Fredy"
"Usijali hilo Sabrina, cha muhimu ni kuwa hata mimi nimepona."
Wakaongea pale mawili matatu kisha Sabrina na Sam wakarudi ofisini.

Walipokuwa ofisini, Sam alimuita Sabrina kwenye ofisi yake na kumwambia,
"Kuanzia leo Sabrina, huruhusiwi kutoka kwenda sehemu yoyote bila ruhusa yangu. Ukitoka bila ruhusa usije ukanilaumu kwa nitakachokufanyia. Na hilo sio ombi bali ni amri Sabrina. Nimemaliza, nenda ukaendelee na kazi"
Sabrina alirudi kwenye ofisi yake akiwa kanyong'onyea huku akijilaumu kuwa yote ameyasababisha yeye mwenyewe maana kila akionywa huwa anajifanya asikii.

Zikapita wiki mbili, Jeff alikuwa kapona kabisa na alirudi nyumbani kwao. Hata Fredy nae alikuwa ni mzima kabisa hata aliweza yeye mwenyewe kwenda kwa kina Sabrina,
"Unajua Fredy, mi hadi leo huwa nakosa majibu ya ile ajali. Hivi ulijuaje kama kutatokea ajali hadi kuniambia kuwa nishuke.?"
"Kiukweli hata sikujua kama itatokea ajali, ila wakati nakuendesha gafla moyo wangu ukawa mzito, nikahisi kuna kitu kibaya kinataka kutokea ila sikujua kama ni ajali. Ndiomana nikakwambia ushuke Sabrina"
"Mmh basi ni khatari"
"Yote sababu nakupenda Sabrina ila wewe hujui tu, laiti kama ungeingia kwenye moyo wangu basi ungegundua kuwa mimi ndio mwanaume wa pekee unayepaswa kuwa naye. Jaribu wewe mwenyewe kuangalia, ni mambo mangapi mabaya yananipata mimi kwaajili yako? Kumbuka nishawahi kuwa kipofu mimi kwaajili yako Sabrina. Hivi nifanye kitu gani ili uelewe upendo uliopo ndani yangu juu yako Sabrina? Niambie tafadhari."
Sabrina alikuwa kimya tu akimsikiliza Fredy ila hata yeye hakujua la kumwambia kwavile alishakubaliana na Sam tayari.
"Ni kweli unanipenda Fredy, hata moyo wangu unatambua hilo. Ila siwezi kuwa nawe sababu nina mwingine tayari"
Fredy aliumia ila akamjibu Sabrina,
"Hakuna shaka, nitasubiri hadi siku utakayokubali kuwa wangu"
Sabrina aliona ni vyema kubadilisha mada ili kuweza kumkatisha Fredy na mwisho wa siku Fredy akaaga na kuondoka.

Sam alikaa na Sabrina na kuamua kupanga naye maswala muhimu,
"Sabrina, nataka kukuoa"
"Mmh Sam, ya kweli hayo?"
"Ndio ni kweli, kwanini nikuongopee mpenzi? Sitaki kukuharibia maisha mpenzi wangu, ndiomana nahitaji tufunge ndoa ili mambo mengine yote tufanye tukiwa ndani ya ndoa"
Sabrina akafurahi sana na kujilaumu kwa kuchelewa kumkubali mwanaume wa muhimu kama Sam, mwanaume anayejua thamani ya mwanamke, mwanaume ambaye haitaji ngono tu bali mapenzi ya dhati ndiomana yuko tayari kumuoa kwanza kabla ya mambo yote.
Moyo wa Sabrina ukamwambia kuwa huyu ndiye mwanaume ambaye amekuwa akimuhitaji siku zote za maisha yake, huyu ndiye mwanaume sahihi kwake.
Sabrina akainuka na kumkumbatia Sam kwa furaha ya hali ya juu kisha akamwambia,
"Nipo tayari kuolewa na wewe Sam, nakupenda kwakweli"
Sam naye akafurahi baada ya kuona kuwa Sabrina ameridhia ombi lake.

Sam alimzungusha Sabrina kwa ndugu zake wote ili wamtambue, na wote hawakuwa na pingamizi lolote kwani walimuona Sabrina ni mtu muelewa na mzuri pia.

Miezi miwili kupita hali ya Sabrina ilikuwa haieleweki kwani mara nyingi alikuwa mgonjwa na mara nyingine alijikuta akiwachukia watu bila sababu za msingi na kufanya wengi wamshangao na wao kuanza kumchukia pia.
Ila yeye aliona kuwa ile hali ni ya kawaida tu na wala haikumshtua na kitu chochote kile.

Siku moja walisafiri na kwenda Arusha kumsalimia mama wa Sam, ambapo alimuita mwanae pembeni na kumuuliza,
"Vipi mwanangu tayari nini?"
"Tayari nini mama?"
"Si huyo binti, tayari namaanisha ana mimba?"
Sam akamcheka mama yake,
"Ndivyo alivyo bhana mama, hana mimba wala nini"
"Mmh mwanangu hadi mimi mama yako unanificha?"
"Sikufichi mama, ila huo ndio ukweli"
"Haya, ila ile kitu huwa inaenda mbele hairudi nyuma basi tutaona tu"
Sam akataniana pale na mama yake na kumaliza maongezi yao kisha wakarudi alipo Sabrina na kuendelea na mazungumzo mengine ambapo mama wa Sam alimkaribisha sana Sabrina kwenye ukoo wao.
Sabrina na Sam wakafurahi sana kuwa pale Arusha,
"Yani huku Arusha pananikumbusha mbali sana Sam"
"Kwanini?"
"Nakumbuka ile siku ya kwanza mimi nafahamiana na wewe, mmh isingekuwa mimi kuja Arusha basi tusingefahamiana jamani"
"Sabrina, kila kitu hupangwa na Mungu kwahiyo labda tungekutana sehemu nyingine"
"Ila saivi naelewa ule usemi usemao kuwa kila jambo hutokea kwasababu"
Sabrina aliyafurahia sana mapenzi yake na Sam huku akingojea ndoa yake kwa hamu kubwa sana.
Muda wa kulala ulipofika, Sam alimpeleka Sabrina kwenye chumba cha kulala kisha na yeye akalala kwenye chumba kingine.

Kulipokucha wakafunga safari na kurudi jijini ili kuendelea na taratibu zao za kazi.
Walipokaribia mjini, Sabrina akamuona Jeff akikatisha njiani na kumwambia Sam,
"Si Jeff yule? Hebu simamisha"
Sam akasimamisha, kisha Sabrina akashuka na kumuita Jeff ambapo Jeff aliitika na kusogea alipo Sabrina,
"Unaenda wapi?"
"Kuna mdada fulani hivi mama kanituma nikamchukulie mzigo wake"
Sabrina alijikuta akimuangalia Jeff kwa hasira iliyotawaliwa na chuki, kisha akamwambia.
"Panda kwenye gari tukupeleke"
"Hapana, nimeshafika ni hapo tu"
"Unanisikiliza au hunisikilizi?"
"Nakusikiliza"
"Haya panda kwenye gari"
Ikabidi Jeff apande kwenye lile gari kisha Sabrina nae akapanda kwenye gari na kumwambia Sam,
"Haya sasa tuendelee na safari yetu"
Sam akawasha gari na kuendelea, Jeff akamuuliza Sabrina
"Inakuwaje na mimi safari yangu?"
"Huendi popote, nakurudisha kwenu. Kwa huyo mdada ataenda mwenyewe mama yako"
"Jamani mamdogo!"
"Tena usinilalamikie ng'ombe wewe"
Hata Sam akamshangaa Sabrina kuwa kwanini amekuwa na hasira kiasi kile.
Walimpeleka Jeff hadi kwao na kumshusha kisha Sam akampeleka Sabrina nyumbani kwake ili atulize akili.

Kesho yake, Sam kama kawaida alimfata Sabrina na kwenda naye kazini ila Sabrina alikuwa akijisikia vibaya na muda wote alikuwa akilalamika tu.

Walipokuwa ofisini, Sabrina akaona vyema kwenda kumuomba ruhusa Sam ili akaangalie afya yake.
"Najihisi vibaya kwakweli, nadhani nina malaria au typhodi"
"Basi ukapime ila uniletee majibu na mimi hapa"
Sabrina akakubaliana na Sam kisha Sam akampa Sabrina dereva wake ili ampeleke hospitali.

Alipofika hospitali, alipimwa vipimo vyote kisha daktari akamletea majibu.
"Hongera sana dada"
"Hongera ya nini?"
"Una ujauzito"
"Mungu wangu"
Sabrina alijishika kichwa na kuanguka chini.


Alipofika hospitali, alipimwa vipimo vyote kisha
daktari akamletea majibu.
"Hongera sana dada"
"Hongera ya nini?"
"Una ujauzito"
"Mungu wangu"
Sabrina alijishika kichwa na kuanguka chini.
Daktari akaamua kumuinua Sabrina na kuanza kumpa huduma ya kwanza, na moja kwa moja akagundua kwamba hii mimba itakuwa ni zile za bila ya kutarajia.
Akaendelea kumpa huduma Sabrina huku akiwaza jinsi ya kumsaidia.
Akili ya Sabrina ilipokaa sawa kidogo, akakaa pale ofisini na yule daktari ila hawakuweza kuongea chochote hivyobasi yule daktari akamwambia Sabrina kuwa aende nyumbani akapumzuke kwanza,
"Ila hakikisha kesho unakuja ili nikupe ushauri mzuri na unaokufaa"
Sabrina akaitikia na kutoka kwenye chumba cha daktari na kuelekea mahali lilipo gari lile la Sam lililompeleka pale hospitali.
Sabrina alipanda kwenye lile gari na kumuamuru yule dereva kuwa ampeleke nyumbani kwake,
"Lakini madam, bosi si amesema nikurudishe ofisini?"
"Tafadhari tusiharibiane siku, kama huwezi sema nishuke nichukue usafiri mwingine."
Yule dereva akaogopa na kuamua kumrudisha tu Sabrina nyumbani kwake.

Sabrina alipofika nyumbani kwake, aliingia ndani na kukaa huku akili yake ikiwa imechoka kabisa kimawazo,
"Hata sijui nifanyeje kwakweli, sijui Sam nitamweleza nini, sijui itakuwaje kwenye swala zima la ndoa baina yangu na Sam mmh!!"
Sabrina aliona kamavile dunia imemuelemea leo, alihisi akili yake kugoma kufanya kazi.
Akaona ni vyema achukue simu na kumpigia Jeff,
"Uje nyumbani kwangu haraka"
"Kwani kuna nini mamdogo?"
"Nimekwambia uje haraka sitaki maswali"
Sabrina akaikata ile simu na kuendelea kuwaza hatma yake na lile tumbo.

Jeff alijiandaa haraka haraka na kwenda nyumbani kwa Sabrina ili ajue ni kitu gani ameitiwa haraka vile.
Akamkuta Sabrina akiwa amejawa na hasira zisizopimika, na Sabrina alipomuona Jeff aliinuka na kumzaba kibao, Jeff akashika shavu lake na kuuliza,
"Mbona unanipiga lakini?"
"Ni haki yangu kukupiga, tena usiniulize maswali. Umenitia aibu sana wewe"
"Kwani ni vipi?"
"Nina......."
Sabrina akasita kuongea, huku akimuangalia Jeff kwa jicho kali.
"Una nini kwani?"
"Hayakuhusu, na pia uondoke mbele ya macho yangu upesi"
Jeff hakutaka kubishana pale na Sabrina, hivyo akaamua kuondoka tu.

Jeff alipoondoka, Sabrina alikaa kimya na kujifikiria jinsi gani ataweza kukabiliana na hali yake, hakuweza kumwambia Jeff moja kwa moja hali yake kwavile aliona kama ni kujidhalilisha kwa kijana huyo.
"Hata sijui nifanyeje kwakweli, au nikatoe? Naona vyema nikatoe, ni kheri Jeff asijue chochote hata Sam pia asijue. Mmh mie jamani, huyu Jeff huyu kanipa doa jamani"
Sabrina alikuwa akijilalamisha tu bila ya kuwa na muafaka wa majibu yake.

Sam alimshangaa dereva wake kurudi mwenyewe bila Sabrina,
"Mbona umerudi peke yako?"
"Madam kasema nimpeleke nyumbani"
"Kwani kazidiwa?"
"Hapana, ila amesema kuwa anahitaji kupumzika"
"Basi sawa"
Sam akaona kuwa ni vyema siku hiyo atoke mapema ili akamuangal ie Sabrina nyumbani kwake.
Na muda ulipofika, moja kwa moja akaianza safari ya kwenda kwa Sabrina, njiani akamuona Jeff na kusimamisha gari lake kisha akamuita, naye Jeff akasogea alipo Sam na moja kwa moja Sam akamuuliza Jeff
"Umetoka wapi?"
"Kwa mamdogo"
"Kufanya nini?"
Jeff akamuangalia tu Sam bila ya kusema chochote, kisha Sam akamwambia tena Jeff,
"Ulienda kufanya nini? Si alikwambia usiende tena wewe!"
"Hayo yalishapita tayari, hata hivyo aliniita mwenyewe"
Sam akamuangalia Jeff kwa chuki ya wazi wazi hata yeye mwenyewe hakujua ni kwanini anamchukia Jeff.
Kisha akarudi kwenye gari yake na kuondoka huku Jeff naye akiondoka huku na yeye akiwa na hasira za wazi kabisa dhidi ya Sam.

Sam alipofika kwa Sabrina alimkuta akitapika,
"Pole sana Sabrina mpenzi"
Kisha akaingia naye ndani,
"Kwani dokta kasema kuwa una tatizo gani?"
Sabrina akakaa kimya huku akifikiria kitu cha kumwambia Sam ili aridhike.
Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Dokta kasema majibu kamili nikachukue kesho"
"Nini? Kesho? Kwani ni vipimo gani hivyo hadi kesho?"
"Mi sijui ila dokta ndio kaniambia hivyo"
"Basi itabidi hiyo kesho twende wote mpenzi"
"Hapana bhana, haina haja ya kwenda wote. Nitaenda tu mwenyewe"
Sam akamuangalia Sabrina kisha akamwambia,
"Ila angekwambia Jeff muende wote ungekubali"
Sabrina akashtuka sana, kisha akachukia,
"Hivi Sam kwanini unapenda kujifananisha na Jeff jamani? Jeff ni mdogo sana kwako na pia hadhi yake ni tofauti na yako, wewe ni mume wangu mtarajiwa na yeye ni mwanangu"
"Wewe unaona hiyo tofauti ni ndogo sana ila bado ukweli utabaki pale pale kuwa yeye unampenda kuliko mimi"
Sabrina ikabidi amuonyeshe Sam kuwa amechukia sana ili Sam asiendelee kujilinganisha na Jeff.
Sam naye alipoona kuwa sura ya Sabrina imebadilika akaamua kubadilisha mada ili aweze kumridhisha Sabrina.

Jeff akiendelea na safari yake ya kurudi kwao akakutana na mwalimu wake njiani na kumsalimia,
"Mbona umepooza hivyo madam?"
"Najisikia vibaya, nahisi nina homa"
"Pole sana, unatakiwa uende hospitali madam"
"Nitaenda kesho, kuna daktari mmoja ni rafiki yangu sana"
"Basi sawa madam"
"Hivi yale mambo yako ulikamilisha?"
"Kiasi madam, ila bado naumia moyo. Nikipata muda, tutaongea vizuri madam"
Jeff akakubaliana na mwalimu wake ambaye ni Joy kuwa waonane nae siku ya kesho yake.

Jeff aliporudi nyumbani kwao alimkuta mama yake akiwa amekaa na binti fulani anayemfahamu. Binti ambaye aliyekuwa akisifiwa katika shule yao kwa uzuri wake, Jeff akashangaa kumuona pale kwao kuwa anahitaji kitu gani.
Alipofika akawasalimia na kuingia ndani, ila mama yake akamuita,
"Mbona hata hujamsalimia vizuri mwenzio?"
Jeff akamuangalia mama yake tena bila ya kujibu chochote kisha akaingia ndani kwao.
Sakina akamuangalia sana mwanae bila ya kummaliza.
"Yani hili toto hili kweli aliyemroga amekufa jamani mbna angekuwa hai angenionea huruma mimi"
Yule binti alikuwa kimya tu akimuangalia Sakina,
"Mwanangu Doris, msamehe bure huyu Jeff sio kosa lake kwakweli ni hajielewi tu"
"Usijali mama, nitakuja hata siku nyingine"
Yule binti akainuka kisha akamuaga Sakina na kuondoka.
Muda huo huo Sakina akamfata mwanae ndani,
"Ila wewe Jeff una matatizo gani mwanangu? Yani binti mzuri kama yule umeshindwa hata kumsalimia vizuri"
"Nisamehe mama kichwa kilikuwa kimevurugika"
"Hao wamama watu wazima ndio wanakuvuruga, na siku nikigundua Jeff! Yani nikimgundua huyo mwanamke nakwambia atataja jina langu kwa kilugha"
Jeff akamuangalia mama yake na kutabasamu, na kumfanya Sakina apandwe na hasira zaidi
"Wee cheka tu, unadhani ni mazuri haya! Yani nitamwambia Sabrina tusaidiane zaidi ili siku tukimgundua huyo jimama awe mboga yetu"
Jeff akacheka na kumfanya mama yake achukie na kuondoka kabisa.

Sam alimuaga Sabrina pale na kuondoka kuelekea nyumbani kwake.
Sabrina alitulia huku akiwaza cha kufanya kwa siku ya kesho.
Wakati akiwaza, simu yake ikaita. Moja kwa moja Sabrina akajua kuwa ni Sam anataka kumwambia kuwa ameshafika, ila alipoichukua ile simu akaona ni namba ngeni.
Sabrina akaipokea ile simu,
"Hallow"
"Kesho nakuja nyumbani kwako"
"Kwani nani wewe?"
Ile simu ikakatika na kumpa mashaka Sabrina kwani hakuelewa kuwa mpigaji ni nani na ile sauti ilikuwa ya kiume.
Ila aliamua kuachana na huyo mpigaji ili kujipunguzia mrundikano wa mawazo.

Kesho yake asubuhi na mapema, kama kawaida Sam alipita kumfata Sabrina ila siku hiyo Sabrina alichelewa sana kuamka na kushindwa kujiandaa upesi.
"Mbona leo umechelewa sana Sabrina?"
"Si unajua kuwa naumwa jamani Sam"
"Basi leo pumzika, nitakuagizia dereva ili akupeleke tena huko hospitali ukapewe majibu na uanze tiba mapema. Sawa mpenzi?"
"Sawa baba nimekuelewa"
Sam akaondoka pale na kumuacha Sabrina ajiandae.
Muda kidogo ulipofika, Sabrina akafatwa na dereva wa Sam kwaajili ya kwenda hospitali.

Sabrina alipofika pale hospitali, moja kwa moja akaenda kwa yule daktari ili aweze kuzungumza nae.
"Daktari, nina ombi moja"
"Ombi gani hilo?"
"Nataka kutoa hii mimba, lakini pia naomba kwenye cheti changu uandike kuwa nina typhoid"
"Hilo swala la kuandika kuwa una typhoid lipo kwenye uwezo wangu ila kutoa mimba hapana"
"Jamani daktari kwanini jamani, nisaidie tafadhari jamani"
"Kuna mwenzangu nitakupeleka, yeye ndio mtaalamu wa hayo mambo, sababu anakupima kwanza. Na uzuri wake hata mambo ya kienyeji anayajua"
Sabrina akaona kuwa ni vyema akakutane na huyo daktari ili aweze kutatua tatizo lake alilokuwa nalo.
Huyu daktari hakuwa na papara sana, hivyo akamtaka Sabrina asubiri kidogo ili akakutane na huyo dokta maarufu kwa kutoa mimba aliyejulikana kwa jina la Dr.Mambo, kutokana na hayo mambo yake.

Muda kidogo, Sabrina akaenda kukutanishwa na huyo Dr.Mambo ili aweze kumshughulikie lile swala la mimba.
Dr.Mambo akampima Sabrina, huku akiguna guna
"Vipi dokta, si itawezekana?"
Dokta akakaa kwanza na Sabrina kwaajili ya mazungumzo,
"Ni hivi Sabrina, mimi ni dokta maarufu sana wa kutoa mimba hapa mjini. Watu wengi wananifahamu, ila wewe nilipokuona kwanza kabisa nikashtuka sana. Na pia nilipokupima, inaonyesha kuwa mimba yako imekaa vibaya kwahiyo nikikutoa naweza kuhatarisha maisha yako. Ila kwa ushauri wangu kwako sasa, nakuomba uje na huyo jamaa mwenye hiyo mimba. Kuna kitu nataka nimuelekeze cha kufanya ili tuweze kuitoa"
Maelezo ya huyu daktari yalimvunja moyo kabisa Sabrina, alijikuta akikosa raha kabisa na kuamua kuondoka tu huku akiwaza jinsi ya kumleta Jeff mahali hapo.
Wakati Sabrina anatoka nje ya kile chumba cha Dr.Mambo, akamuona Joyce yule dada wa Sam akiwa kwenye benchi huku ikionyesha kuwa naye anangoja huduma toka kwa Dr.Mambo.
Sabrina alivyoona vile, akarudi kwa Dr.Mambo upesi,
"Dr, huyo dada wa nje huyo najua naye atakuwa amekuja kutoa mimba. Tafadhari mkatalie, ni mimba ya kaka yangu"
Dr.Mambo akacheka sana huku akimuangalia Sabrina na kumjibu,
"Usijali kitu Sabrina, nitakusaidia kwa hilo"
Sabrina akatoka, bila ya kumuangalia tena Joyce na kuondoka zake.

Sabrina, alirudi moja kwa moja nyumbani kwake huku akipanga namna ya kuzungumza na Jeff ili aweze kumkubalia yeye aitoe ile mimba.
"Naimani atakubali sababu hata yeye anajutia kitendo alichonifanyia mimi kipindi kile. Hii ni aibu jamani, hata sijui pa kuificha sura yangu."
Akachukua simu yake na kumpigia simu Jeff kuwa aende nyumbani kwake, naye Jeff alikubali bila kinyongo chochote.

Sam alitulia ofisini huku mawazo yake yote yakiwa juu ya Sabrina.
Alijiona wazi kuwa hawezi kufanya lolote bila ya uwepo wa Sabrina.
Hivyo akajipanga kutoka mapema ili kwenda kumuwahi Sabrina nyumbani kwake na ili waweze kupata muda muafaka wa kuzungumza.
Ila kabla Sam hajatoka pale ofisini, akapatwa na ugeni wa dada yake ambaye ni Joyce.
"Kaka kuna mambo nataka tuzungumze"
"Mambo gani hayo?"
"Kwani wewe hutaki mtoto?"
"Nataka sana, hata sasa hivi ningempata ningefurahi sana"
"Basi kuna kitu nimekusaidia leo, wewe mwenyewe utafurahi"
"Kitu gani hicho Joy?"
"Leo sitakwambia, ila utajua tu ni kitu gani. Nimekusaidia kaka yangu jamani, hata mi mwenyewe natamani kuitwa shangazi"
"Mbona sikuelewi Joy?"
"Ipo siku utanielewa tu"
Kisha Joy akamuaga Sam na kuondoka, na kumfanya Sam apatwe na maswali bila ya majibu kwani alifikiria mara mbili mbili ila hakuelewa kuwa ni mtoto gani anayezungumziwa hapo na ni kwa mantiki ipi.
Sam akaamua tu kuachana na hayo mawazo kwavile aliona kuwa yanamchanganya tu.
Alikamilisha kazi yake na kuanza kujikusanya ili kwenda nyumbani kwa Sabrina kumuona.

Jeff kama kawaida alifika kwa Sabrina kusikilizia wito wake, ila alimshangaa kumuona Sabrina leo akiwa mwanamke mpole kuliko siku zote.
"Jeff, nimekuita hapa kukwambia kuwa mimi nina mimba"
Jeff akashtuka sana kwani hakuamini, akajikuta akiropoka,
"Hatimaye ndoto zangu zimetimia"
Hapo ndipo alipomtibua Sabrina,
"Yani wewe kweli huna akili, mimi nimekuita hapa ili ukanisaidie kuitoa hii mimba halafu wewe unasemaje?"
"Namshukuru Mungu, ndoto zangu zimetimia"
Sabrina akazidi kupatwa na hasira,
"Mbwa mkubwa wewe, ndoto zako zimetimia kitu gani? Unafikiri mimi nafanyeje na hii mimba?"
Muda huo huo Sam naye aliwasili pale ndani na kuuliza kwa mshangao,
"Mimba?"
Sabrina na Jeff nao wakashtuka kumuona Sam pale ndani.


Muda huo huo Sam naye aliwasili pale ndani na
kuuliza kwa mshangao,
"Mimba?"
Sabrina na Jeff nao wakashtuka kumuona Sam pale
ndani.
Sam akawaangalia kwa makini na ule mshtuko wao kisha akawauliza tena,
"Nasikia kuhusu mimba hapa, haya niambieni ni mimba ipi na imefanyaje?"
Sabrina akachekecha akili yake na kutafuta jibu la kumpa Sam.
Wakati huo Jeff naye akaanza kujibu,
"Ni mimba yangu ipo kwa......."
Sabrina akamkatisha Jeff kwa kumpiga kibao,
"Yani wewe huna akili kabisa, unajua wazi una makosa halafu unataka kuelezea nini sasa? Huna akili wewe."
Kisha Sabrina akamuangalia Sam na kumwambia,
"Yani hili litoto usilione hivi, limenipa kesi hapa balaa"
"Niambieni sasa ni kitu gani? Hivi unajua kama hapa mnazidi kunichanganya tu"
Jeff akataka kusema tena, ila Sabrina alimuangalia Jeff kwa jicho kali sana na kumuogopesha kisha akasema,
"Basi mwambie ukweli mwenyewe mamy"
Sam akiwa na hamu ya kujua kinachoendelea, akadakia
"Ndio niambieni ukweli"
"Unajua mimi naumwa Sam"
"Ndio unaumwa ila niambie ukweli kuhusu nilichokisikia hapa cha mimba"
Sabrina akapata maneno ya kujitetea muda huo huo,
"Ni hivi, unakumbuka kipindi kile nilipomfukuza huyu Jeff hapa kwangu?"
"Ndio nakumbuka, niambie sasa"
Kwa mawazo ya Jeff akajua kuwa Sabrina anataka kumwambia Sam ukweli, akaamua kuinuka kwa aibu na kwenda jikoni ili kama likitokea lolote la kutokea awe amejiandaa.
Sabrina akamuangalia Jeff alipokuwa akienda jikoni na kuendelea kumuhabarisha Sam,
"Basi huyu Jeff bhana kuna binti alikuwa ana mahusiano nae, nilipokuja kugundua nikaambiwa kuwa ni mtoto wa mwanajeshi, ili kuepuka matatizo nikaamua kumfukuza Jeff. Sasa jana nimegundua kuwa yule binti ana mimba ya Jeff. Yani huyu mtoto ananiletea balaa jamani"
"Mbona makubwa hayo, itakuwaje sasa?"
"Mie leo nilipoenda hospitali nimepitia kwa daktari mmoja hivi kumuuliza mlolongo wa kutoa mimba sababu yule binti amekubali kuitoa ila tatizo ndio kwa huyo Jeff namwambia hapa anakataa ndiomana nikawa nafoka"
Sam akamuangalia Sabrina na kuwa kama vile amemuelewa na kumuamini kiasi kisha akamuuliza,
"Na wewe je unaumwa nini? Si ulienda kuchukua majibu leo?"
Sabrina akachukua mkoba wake na kutoa kikadi kidogo na kumkabidhi Sam,
"Nimeambiwa nina typhoid, yani hapa nimechomwa sindano na kupewa dawa za kunywa"
"Yani typhoid ndio ugonjwa ambao jana ulishindikana kuonekana Sabrina?"
"Mi sijui mambo ya kidaktari"
Jeff akatoka kule jikoni na kuwapita pale sebleni na kuondoka.
Sabrina akapata mwanya zaidi wa kumueleza Sam,
"Si unamuona alivyo na kiburi mtoto mwenyewe!"
"Namuona ila ngoja mimi nipate nafasi ya kuzungumza naye ili tujue cha kufanya"
"Hata asikusumbue akili, mi najua cha kufanya hata usijali"
Sabrina akajitahidi kumpa maneno Sam yatakayomfanya asizungumze na Jeff kwani alihofia kuwa Jeff anaweza kumwambia ukweli Sam.

INAENDELEAAAH



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.