KAMA WEWE HUMCHANGAMSHI RAFIKI ZAKO WATAKUSAIDIA KUMCHANGAMSHA!

Photo by IDDI MAKENGO🇹🇿 on August 18, 2020. Image may contain: 1 person, indoor
“Mimi siwezi kukaa na mke wangu kupiga umbea, naonge anaye nini? Yaani mimi nikirudi nyumbani ni kula na kulala, mwanamke ataniambia nini?” John alikua akiongea na Kaka zake, hiyo ilikua ni miezi miwili tu baada ya kuoa. Baba yake alikua kakaa pembeni anawasilikiza. Waliongea sana, lakini jioni John alikua amekaa na wadada wawili, jirani zake, wanaongea wanacheka, ulikua ni muda wa kurudi nyumbani lakini yeye alikua anacheka na wale akina dada.
“Unajua wanakutaka, wanavyojichekesha chekesha wanakutaka kimapenzi!” Baba yake alimuambia baada ya wale wadada kuondoka.
“Hapana, mimi nimeoa Baba nampenda mke wangu, hawa tumezoeana tu!” Alijitetea.
“Mmezoeana wakati kila siku ukija hapa kumuona Mama yako wanakuja mnaongea mpaka usiku, hawajaolewa hawa…”
“Najua lakini mimi nina mke, napiga nao umbea tu, si unajua umbea unapoteza mawazo, hawawezi kunipata nampenda mke wangu…”
Baba yake alimuangalia kisha akacheka na kumuambia.
“Kwahiyo unapiga umbea na wanawake wengine, wanakufurahia, unawachekesha, wanasikia raha kuwa na wewe, yaani wakikuangalia ulivyomchangamfu wanakutamani mpaka kuloana. Halafu ukifika kwa mke wako ndiyo unajifanya mwanaume huwezi kuongea eti hupigi umbea unanuna nuna tu?”
“Lakini Baba mwanamke nitaongea naye nini?” John alijitetea.
“Kwahiyo hawa uliokua unaongea nao ni wanaume?”
“Hapana lakini?”
“Mwanangu kila mwanamke anahitahi mwanaume wa kumfanya acheke, kama humchekeshi mke wako basi jua hata mbuzi anaweza kumchekesha. Wakati nafanya kazi mwanangu nilikua na rafiki yangu kama wewe, basi akiwa kazini alikua anacheka, anachangamkia kila mwanamke, lakinia kifika nyumbani kanuna utafikiri yuko msibani.
Mke wake akawa kila sikua ananilalamikia kuhusu tabia za rafiki yangu, mimi nikawa nashangaa kwani mbona kazini ni mchangamfu. Basi nilijaribu kuongea naye kumuambia anachokifanya si sawa ila hakunielewa. Basi shemeji akanizoea akawa ananiambia shida zake, nikaamua na mimi kumchangamsha, miaka kumi namchangamsha na kumchekesha mke wake mpaka wakahaama.
Sasa wewe kuwa bize tu kuchangamsha na kupiga umbea na wanawake za watu huku ukijifanya kidume kila ukirudi nyumbani umevimbsiha mashavu mwisho wa siku watamchangamsha vijana wa mtaani!” Baba huyo kaondoka akamuacha John na maswali, “Inamaana Baba alikua anamchangamsha mke wa rafiki yake?” huyo katoka karudi kwa mke wake anaanza kukagua simu kuangalia nani anamchangamsha mke wake.
MWISHO




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.