HAKUNA MWANAUME ANAYEBADILIKA KWAKUA UNA KISIRANI!
Kila siku alilia akinilalamikia kuwa nina kelele sana hivyo hawezi kukaa na mimi. Niliponunua Kitabu chako nilisema ni lazima nikutafute kwani sikukielewa kabisa. Lakini kabla ya kukutafuta kuna siku uliweka post kuhusu mwanamke alikuomba ushauri, aisee nilisoma nilijiona mimi kabisa, ila jibu ulilompa lilinishikisha adabu.
Ulimuambia ana kisrani hivyo ana machaguo mawili, kupunguza kelele na kuongea na mume wake kama mtu mzima au kupuuzia kuendelea na kelele. Ulimuambia ukweni wahsamchoka hivyo ni jambo la muda tu mwanaume naye atamchoka. Basi huyo dada sijui alikujibu vibaya iola hakufuata ushauri wako.
Mrejesho wake ilikua ni mume wake kaondoka na kwenda kupangisha sheemu nyingine na kumuambia kuwa atahudumia watoto tu kwani hataki ugomvi wa kila siku. Niliposoma nikajiona mimi, niliamua kubadilika, kwani niligundua kweli nina kisirani, mume akichelewa nilikua nampigia simu mpaka Mama yake kuwa leo kachelewa, natuma meseji hata kumi ila sijibiwi.
Kaka nimebadilika mpaka mume wangu akaanza kuhisi nachepuka, akahisi nina mwanamume mwingine akachunguza simu yake ndipo nikamuonyesha hiyo Makala ambayo niliiscreenshot nikamuambia sababu za kubadilika. Nashukuru sasa hivi tuna amanai, mume wangu anawahi kurudi, kuna kipindi anachelewa ila ananipa taarifa na sasa hivi sijali sana kufuatilia kama ni kweli au la zamani nilikua napigia rafiki zake wote kuwauliza ila sasa kisirani kimepotea.
No comments: