MAKOSA 5 AMBAYO WANAWAKE WANAOTESEKE KATIKA MAHUSIANO WAMEYAFANYA

utamuzaidiapp
Lengo kubwa la mahusiano ni furaha lakini si kila mtu hubahatika kuwa na furaha katika mahusiano yake. Lakini unaweza kujiuliza hivi ni kwanini mwanaume ambaye alikua akimpenda mpenzi wake au mke wake ghafla anaanza kubadilika na kumpiga.
Anakua mbogo na mahusiano hayana furaha tena mwanamke kila siku ni kilio. Binafsi siamini kuwa ni ghafla, tatizo kubwa nikuwa wanawake wengi huona dalili na huzipuuzia au hufanya makosa ambayo hulea mateso ya mahusiano.
Kama uko kwenye mahusiano kuna mambo ambayo hutokea kila siku, unayapuuzia na kuyaona ya kawaida. Lakini kwa kiwango kikubwa wanawake wanaopigwa, wanaosalitiwa na kunyanyaswa walipuuzia mambo hayo, haya ni makosa madogo madogo ambayo unayafanya wewe na yatakuja kukugharimu yaone hapa;
(1) Unaomba Msamaha Ukikosewa; Hili ni kosa la kwanza kabisa mabalo wanawake wengi hulifanya, kuna kitu ambacho wanawake huambiwa kila siku, kuwa kwenye mapenzi ni lazima kujishusha, sasa wanawake hudhani kujishusha ni kuomba msamaha hata bila kosa.
Kwamba mwanaume kakusaliti unamuomba msamaha kwa kumfumania, kakupiga unaomba msamaha eti kwa kumkasirisha, na makosa mengine mengi. Kinachotokea hapa unapomuomba msamaha kwa kosa lake kwanza unamuambia kuwa yeye hafanyi makosa hivyo hawezi kujutia wala kuliona lile kama kosa.
Pili unamuambia kuwa unamhitaji sana huwezi kuishi bila yeye hivyo unaweza kuvumilia upuuzi wowote atakaoufanya. Hii humpa kiburi na badala ya kumbadilisha basi humfanya azidi kukunyanyasa, kama mwanaume akikukosea, tena kosa kubwa kamwe usiombe msamaha, hata kama yeye hataomba lakini usijishushe na kuomba msamaha wewe.
Muache akae akijua kua kakukosea na hauko tayari kuomba msamaha kwa makosa yake. Wanawake wengi ninao kutana nao, wanaanza kwa kukuambia alikua ananisaliti nikamuomba msamaha, alikua ananipiga nikamuomba msamaha na wengi huishia kuachwa kwani hakuna mwanaume anapenda kuishi na mwanamke wa namna hii.
(2) Unavumilia Vitu Vidogo: Ndiyo mwanaume haanzi kwa kukupiga tu, huanza kwa kukutukana, kukudhalilisha, anatoa vijimaneno vidogo vya kashifa. Kama mvuta sigara au mlevi ambaye huanza na bia moja akizoea hunywa mbili mpaka kuwa mlevi kabisa.
Mwanaume ataanza kwa kukukosoa, kukudhalilisha kisha kukupiga. Hivyo unatakiwa usikubali tangu awali, kitu hata kama ni kidogo vipi kama kikikukera muambie, hata kama hataomba msamaha lakini muambie hiki ulichifanya si kitu kizuri na siwezi vumilia.
Hapo moja kwa moja anajua kuwa wewe si mtu wa mchezo na kama huwezi kuvumilia kutukanwa basi hata kupigwa huwezi. Lakini ukivumilia anavyokukejeli na kusema wanaume ndiyo walivyo unampa njaa ya kuendelea kukudhalilisha kikubwa zaidi na hata kukupiga na hapo ndiyo unajikuta unaingia kwenye mahusiano ya mateso.
(3) Houngei Na Yeye Unaongea Na Watu; Ndiyo wanawake ni wataalamu sana wa kuelezea matatizo yao, akikwazwa kidogo utasikia kaendakwa Mama mkwe, kwa rafiki au kwa Mma yake. Lakini mara nyingi wanawake ni wakimya kwa wapenzi wao, mpenzi wako anafanya mambo mabaya anakukwaza badala ya kumuambia kuongea naye unaongea na rafiki yake.
Unataka watu wengine wakusaidie kuongea naye, hapa unamuambia kuwa nakuogopa hivyo siwezi kukuambia. Lakini wanaume unapotangaza matatizo ya ndoa yenu kwa watu hata kama ni Mama yake unazidi kumpa kiburi. Wanaume tunakitu kimoja ni kama kaujeuri flani kuwa sipangiwi.
Sasa unapoenda kwa Mama yake, rafiki yake au ndugu, ukamuambia matatizo yake kabla ya kuongea naye, kujaribu kusuluhisha naye, akiitwa na kuonywa anaona kama watu wanamuingilia hivyo kwakua ana ujeuri wa kutotaka kupangiwa basi hukasirika zaidi. Hembu ukipata tatizo na mwenza wako muambie yeye kwanza, muambie namna ambavyo huridhiki na unavyoumia kabla ya kutafuta ushauri wka ndugu zake.
(4) Huongei Unalalamika; Hiki ni kitu kingine ambacho wanawake hukosea wanapoamua kuongea na wapenzi wao. Badala ya kuongea na mwenza wako kama mtu mzima, kumuambia hili linanikera, hili sitaki, hili siwezi kuvumilia, jicho kavu, sauti kavu, wewe unaanza kulia, kulalamika na unakua kama unaomba msamaha.
Mwanzoni nimezungumzia kuhusu kuomba msamaha kwa makosa yake, hiki ndicho kinachotokea unapolalamika. Kakuslaiti unaanza kumlilia aache huku ukionge amapungufu yako na unavyoumia. Hapo unampa nguvu, unampa kiburi kuwa wewe ni mdhaifu unaanza kuoneyesha kama unaonewa hivyo unamuambia anweza kukuonea.
Hembu badilika, kama mwenza wako kakosea kitu flani, kafanya kitu kakuumiza badala ya kulialia, kulalamika kuwa mtu mzima kwa mdua. Muambie jicho kavu, bila kulia ongea kama unaongea na mtu mzima mwenzako, mtu ambaye mko sawa na muambie, hiki hapana, hiki sawa, hiki kimenikera basi acha kulalamika!
(5) Umejisahau Wewe; Mwanzo wa mahusiano mwanaume ndiyo hujali, lakini mwanaume akishampata mwanamke mara nyingi huacha kujali. Hapa ndipo wanawake wengi hunza kunyanyekea, kujishusha mpaka kujifukia, wanaacha kuishi maisha yao na kuanza kuishi maisha ya mwanaume.
Alikua na chumba haongezi kitu kisa mwanaume, alikua na kazi anaweza kuacha kisa mwanaume, anaakili ya kufanya mambo ya maendeleo anaacha kisa mwanaume, ndiyo unajishusha ili mwanaume asikuone una akili, una uwezo flani, huchangii hata mambo ya maana kisa mwanaume.
Unafanya kila kitu wanaume anchotaka, ili kumridhisha kuanzia chumbani mpaka katika maisha. Unavitu ambavyo uliapa hufanyi lakini uanfanya ili asikuache. Dada yangu hapo ndiyo unajisahau, unakua huna furaha na furaha yako inamtegemea yeye. Kwamba akikasirika na wewe maisha yako ni kama yanasimama vile.
Kila kitu ni yeye, hufanyi maisha yako tena, huangalii kama unafuraha tena na mwisho wa siku hata yeye anakuchoka kwani anakua kama anaishi na mashine ya kumridhisha. Hembu jifunze kuwa na furaha.
Kama una kitabu changu hembu soma shemu ya nne uone namna ya kukabiliana na hali hii, acha kutengeneza ndoa ya mateso chagua furaha. unapaswa kukumbuka kuwa wewe ni binadamu unahitaji furaha ya peke yako, hivyo jifunze kuwa na furaha na si kuwafurahisha watu.




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.