Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? sehemu ya 51
Nyumbani kwakina Joy nako walikazana kumdadisi Sam kuhusu mkewe Sabrina na mtoto wao.
"Wako salama hao na wanaendelea vizuri"
"Ila mbona nimepata khabari kuwa toka Sabrina apoteze kumbukumbu umemrudisha nyumbani kwao na umesema humtaki tena? Sio vizuri hivyo anko, mwanamke hakimbiwi kwenye matatizo"
"Sijamkimbia mjomba ila kuna mambo tu yaliingiliana, hivi karibuni nitaenda kumchukua na kumrudisha nyumbani ili niishi nae kama zamani"
Sam aliongea hayo huku akifikiria hilo swala na kuona kuwa ni muhimu sana kufanya hivyo ukizingatia kisheria bado ana haki kwa Sabrina kama mumewe.
Rose alianza kumueleza Neema kilichotokea na kumfanya Neema amshangae sana,
"Rose jamani rafiki yangu kwanini umefanya hivyo? Kama ni pesa ungeniambia tugawane, sasa mimi nitauguzwa na nani wakati sote ni wagonjwa?"
"Tamaa, tamaa imeniponza Rose mimi."
"Pole rafiki yangu, ila hukutakiwa kunieleza"
"Siwezi kuwa kimya, nikufiche vipi wakati wewe unajua kila kitu? Kuficha kwako wewe ndio kulikonitesa mimi leo, ungeniambia ukweli hakika nisingeangukia shimoni"
"Nisamehe rafiki yangu, ila hutakiwi kusema. Ibaki kuwa siri yako"
"Nishasema tayari, liwalo na liwe"
Muda huo huo Neema akamshuhudia Rose akianguka chini na kuwa kimya kabisa.
"Nisamehe rafiki yangu, ila hutakiwi kusema. Ibaki
kuwa siri yako"
"Nishasema tayari, liwalo na liwe"
Muda huo huo Neema akamshuhudia Rose
akianguka chini na kuwa kimya kabisa.
Neema alishtuka sana na kumuangalia Rose kwa makini huku akiwa haamini anachokiona.
Akaanza kumtingisha kwa nguvu huku akimuita,
"Rose, Rose usiniache peke yangu Rose. Nabaki na nani mimi? Rose rafiki yangu, Rose msiri wangu nabaki na nani mimi Neema?"
Neema akasikia mtu akigonga mlango wake, hakuweza hata kumkaribisha kwani tayari alishachanganyikiwa.
Mtu huyo aliamua kuingia hivyo hivyo ndani kwa Neema, alikuwa ni yule mchumba wake John akiwa ameambatana na rafiki yake, nao hawakuweza kuamini walichokiona mbele yao.
Walishangaa sana, ikabidi watafute usafiri na kumuwahisha Rose hospitali.
Walipokuwa pale hospitali ndipo wakapewa majibu kamili kuwa Rose aliaga dunia.
Kwakweli Neema alichanganyikiwa kupita maelezo ya kawaida na kujikuta akilia sana hadi kuzimia.
Hapakuwa na wa kumuuliza chanzo cha kifo cha Rose ila ndio hivyo alikuwa amekufa na kufanya wote wabaki kushangaa tu kwani hawakutegemea kumkuta Rose amekufa kwa namna ile.
Ila hapakuwa na namna nyingine zaidi ya kuwaita ndugu wa Rose tu ili waweze kufika pale hospitali na kupanga taratibu za mazishi.
Sam akiwa bado nyumbani kwakina Joy, akashangaa moyo ukimuuma gafla na kugundua kuwa lazima kuna kitu kimetokea.
Hakuweza kuendelea kuwa pale kwani aliwaaga na kuondoka, na hakuweza tena kwenda kutembelea ndugu wengine bali alienda moja kwa moja nyumbani kwake.
Alijiuliza sana kuwa ni tukio gani limetokea bila ya kupata jibu ila roho ilimuuma sana na kujua lazima hilo tukio litakuwa linamuhusu yeye tu kwa lazima.
Wazo la kumuhusu Rose lika mjia kwenye akili yake, kengele ya khatari ikagonga kichwani mwake,
"Mungu wangu, Rose hayupo tena. Itakuwa ni Rose tu Mungu wangu"
Swali lake ni je Rose alimwambia nani hadi amepoteza maisha hakupata jibu,
"Kwanini hawawezi kustahimili kuwa kimya? Ni Neema tu ndio namuona kuwa mwanamke pekee aliyeweza kuvumilia kusema hadi leo. Niliapa kutokufanya wanawake waangamie tena kwaajili yangu ila sasa najiona kwenda kinyume na kiapo changu"
Ikabidi atulie na kuanza kupeleleza msiba ulipo ili aweze kwenda.
Joy alirudi kwa mumewe James huku akiwa amepatana na wazazi wake kwahiyo ikawa ni furaha baina yao.
Kisha akamueleza James kuhusiana na stori aliyoambiwa na Sam na kumfanya James amsikitikie sana Sam na kujiona yeye ni kijana mwenye bahati kwa kupendwa na baba zake wote wawili.
"Sasa imekuwaje Sam akawa tajiri kiasi kile? Maana mi nilijua kuwa ametokea familia ya kitajiri"
"Kwakweli sikujua maisha ya Sam kabla, ninachokumbuka ni baba tu kunitambulisha kuwa ni ndugu yangu yani mtoto wa dada yake. Na hata mimi nilijua kuwa yule Sam ni tajiri kutokana na familia ya kwa baba yake kumbe pale alipo hana hata baba ni yupo yeye kama yeye. Sasa utajiri wa namna hii sijui ameutoa wapi, inaweza kuwa ni siri yake au basi akiamua anaweza akatushirikisha na hilo pia"
"Sasa hata baba hawasilianagi na hao nduguze au ni nini"
"Nadhani huwa wanawasiliana ila ukoo wao siuelewi, sababu wengi wanaishi Arusha. Ila huyu Sam anajulikana sana sababu ya utajiri alionao"
Wakazungumza mengi na kwakweli siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwao mpaka muda wa kwenda kulala ulipowadia.
Kwenye mida ya saa nane usiku, Joy alishtuka kutoka usingizini na kuanza kulalamika maumivu ya tumbo na kiuno, ikabidi James amkimbizie mkewe hospitali.
Asubuhi na mapema siku hiyo, Sabrina alikuwa wa kwanza kuamka baada ya kuitwa na mama yake kuwa kuna mgeni wake anamsubiri.
Sabrina alitoka na kumshangaa yule mgeni kwani sura ilikuwa ni ngeni kwake kutokana na kukosa kumbukumbu ila huyo mgeni hakuwa mwingine bali alikuwa ni Fredy, mwanaume ambaye aliwahi kuwa na mahusiano naye hapo zamani.
"Nimepita kukusalimia Sabrina ila pia nina khabari mbaya"
"Khabari gani mbaya? Na mbona sikukumbuki?"
Fredy akashangaa,
"Kumbe nilivyoambiwa kuwa huna kumbukumbu siku hizi ni kweli? Dah pole sana, khabari mbaya niliyonayo ni kuwa yule rafiki wa dada yangu Neema yule wa kuitwa Rose amekufa"
Sabrina akashtushwa tu na khabari ya kifo lakini hakuna aliyemkumbuka kati ya hao aliowataja.
Fredy akajikuta akimsikitikia sana Sabrina kwani hakutegemea kabisa kumkuta akiwa hana kumbukumbu kiasi hicho kisha akawaaga na kuelekea zake msibani.
"Nitakuja tena baada ya msiba tuongee vizuri Sabrina"
Kisha akaondoka zake.
Sabrina alibaki akimuhoji mama yake juu ya huyu kijana kwani hakumfahamu kabisa.
"Na kwanini aje aniletee hizi khabari za msiba wa mtu ambaye simfahamu kabisa? Na kwanini hakuwahi kuja kuniona hapo kabla?"
Mama Sabrina ikabidi ajaribu kumueleza kidogo mwanae juu ya Fredy ingawa hakuna ambacho Sabrina alielewa wala kutambua kwani aliona kama kumpigia mbuzi gitaa tu.
Muda kidogo simu ya mama wa Sabrina ikaita na alipoipokea akapewa taarifa ya kujifungua kwa mkwe wake Joyce na kumfanya atabasamu na kufurahi sana.
Kisha yeye na Sabrina wakajiandaa kwaajili ya kwenda kumuona Joy.
Wakiwa kwenye msiba wa Rose, kila mtu alijua tu kuwa Rose amekufa gafla lakini hakuna aliyejua kitu kilichomuua Rose.
Hawakujua ni ugonjwa gani aliumwa ila daktari alishauri kuwa maiti yake isikae sana hivyo wakapanga mazishi kuwa siku hiyo kwani watu wengi, ndugu, jamaa na marafiki walikuwepo mahali pale ukizingatia kuwa walishapata khabari ya kifo chake tangia jana yake.
Mdogo wa Rose aliyejulikana kwa jina la Aisha ndio pekee alikuwa karibu na Neema kwani wengi walikaa mbali kidogo na Neema kutokana na harufu waliyosikia huku wengine wakisikika kumsema vibaya.
Aisha alikuwa karibu na Neema huku akimfariji,
"Dada, achana na maneno ya watu. Wanasema hapa kuwa wewe ni mfu anayetembea. Achana na maneno yao. Hapa roho inaniuma sana kwa kumpoteza dada yangu kipenzi Rose, na watu ninapowasikia wakikusema wewe vibaya inaniuma sana"
Alikuwa karibu akifarijiana nae hadi muda wa mazishi ulipofika.
Ambapo wakati wanaenda makaburini, Neema alishangaa kumuona Sam eneo lile na kujikuta akijawa sana na hasira moyoni mwake ila muda wote Sam alikuwa akimtafuta Neema na muda ambao Neema alimuona Sam ndio muda huo huo Sam alimuona Neema na kuwafata pale walipokuwa wamesimama na Aisha.
Neema hakutaka kupaniki pale ila kiukweli katika moyo wake hakupenda kabisa kukaribiana na Sam,
"Jamani poleni sana, najua mnavyoumia. Najua sasa tunaelekea makaburini ila kwa heshima na taadhima naomba twendeni mkapande kwenye gari yangu"
Neema akamuuliza kwa dharau,
"Kwanini tupande kwenye gari yako?"
"Najua huko mvua itanyesha, na sipo tayari kuwaona mkilowa kwenye lile gari la uwazi juu. Tafadhari Neema usikatae"
Aisha akamuangalia Neema na kumwambia kuwa bora wakubali tu kupanda kwani hata hivyo lile gari walilotaka kwenda kupanda limejaa na ukizingatia watu wanavyomtenga ndio itakuwa tatizo zaidi.
Neema akakubali na kuwafanya waingie kwenye gari ya Sam huku wakielekea makaburini.
Sabrina na mama yake wakafika hospitali alipopelekwa mke wa James na kuwakuta pale wazazi wa Joy ambapo walisalimiana pale kisha kwenda kumuona Joy na mtoto wake.
Ingawa baba wa Joy bado alikuwa na kinyongo dhidi ya mama wa Sabrina ila tu hakutaka kujionyesha mbele za watu ila kiukweli bado alikuwa na maumivu ya kutosha juu ya mama yake Sabrina.
Walitulia pale hospitali, muda kidogo mama wa Sabrina alikuwa nje akiongea na simu akamuona binti akikimbizwa leba, alipomtazama vizuri akagundua kuwa alikuwa ni Dorry na kujikuta na mshangao tu kuwa siku hiyo imekuwa ni siku ya kujifungua, na muda huo huo akachukua simu na kumpigia Sakina juu ya alichokiona hapo.
Sakina akiwa nyumbani alifurahi sana baada ya kupoka simu kuwa Dorry ameonekana hospitali akielekea leba kwani alijua moja kwa moja kuwa hiyo ni khabari njema kwake.
"Eeh Mungu, asante kwa kumfanikisha mkwe wangu"
Kisha akajihimu na kujiandaa haraka haraka kisha kwenda hospitali kumuona huyo mkwewe Dorry.
Sam alienda na wakina Neema hadi makaburini, kisha akasimamisha gari mbali kidogo huku wakina Neema wakitaka kushuka.
"Hapana, msishuke"
"Kwanini tusishuke"
"Mvua itanyesha hapa"
"Unamaana gani Sam? Toka tumetoka kule umekazana na huo huo usemi kuwa mvua itanyesha wakati hakuna mawingu wala dalili yoyote ya mvua"
"Nina maana yangu kuwaambia hivyo"
Hata Aisha naye akamshangaa huyu Sam ila Neema akaelewa kuwa Sam anajutia kitendo chake cha kuwauma sasa anasema maneno kama kujihami tu.
Wakaamua kupuuza maneno yake na kushuka ila yeye wakamuacha mule mule kwenye gari yake akiwa amejiinamia kwa mawazo.
Sam alikuwa akifikiria vitu vingi sana mule ndani ya gari, alifikiria misiba mingi sana aliyosababisha.
Alikumbuka alichokuwa anaambiwa kilichoendelea katika misiba hiyo, siku zote huwa anatuma watu ambao walienda kwa niaba yake na kumletea khabari ila huu ulikuwa ni msiba wa kwanza kuhudhuriwa na yeye kati ya wanawake wengi aliowasababishia vifo vya aina hiyo.
Alimfikiria na Neema pia na kugundua kuwa ni wazi Rose alimwambia Neema kwani kungekuwa na yeyote mwingine aliyemwambia basi yeye angekuwa akinyooshewa vidole tu pale msibani.
Alimuangalia Neema na yule binti aliyeongozana nae wakielekea mahali husika kwenye makaburi, aliwaangalia kwa jicho la huruma sana.
Neema na Aisha walisogea mpaka karibu na karibu, muda kidogo wakashangaa mvua kubwa kuanza kunyesha.
Kitu pekee kilichosaidia ni kwavile walishaanza kufukia lile karibu kwahiyo ikabidi vijana wa pale wajitahidi kufukia vile vile na mvua ila mvua nayo ilikazana na kuwafanya watu wakimbie kwenda kujibanza kwenye makazi ya watu na wengine wakimbilie kwenye magari, wakati huo Neema hata hakutaka kukimbia eneo lile na kujikuta ameachwa peke yake pale makaburini.
Aisha aliyekuwa naye amekimbia, akamuonea huruma Neema pale makaburini na kutamani kwenda kumfata ila anamfata vipi ikiwa mvua inanyesha kwa kiasi kile? Kwa bahati akapata mwamvuli kwa mtu na kuutumia mwamvuli huo kumfata Neema pale makaburini kisha akarudi nae hadi kwenye gari ya Sam ambapo Sam alifungua milango na kuwaomba wapande na walipopanda tu, Sam akaondoa lile gari na hapo hapo ile mvua iliyokuwa inanyesha pale makaburini ikakatika.
Sam akamrudisha Neema nyumbani kwake akiwa na yule Aisha kwani alishajua wazi kuwa Neema amechanganyikiwa na pengine anajiona na yeye kifo kikimkaribia.
Neema nae hakuongea lolote ila alilia sana mule ndani kwake,
"Rose, Rose wewe rudi rafiki yangu. Rose wewe ndio ndugu yangu, rudi Rose. Kwanini umekufa Rose, umeniacha na nani mimi? Rose rudi mama, njoo uone nilivyolowana Rose. Nitacheka na nani mimi, nitaongea na nani mimi?...... Kwanini Rose kwanini?"
Aisha alipata kazi kubwa ya kumtuliza Neema, hata Sam nae machozi yakamtoka na kumfanya ashindwe kustahimili, ashindwe kuvumilia na kuamua kuondoka pale nyumbani kwa Neema.
Aisha naye aliendelea kumbembeleza Neema na kumfariji bila kuchoka, Neema alikuwa akifikiria kifo chake, akifikiria jinsi mvua itakavyonyesha na watu watakavyomkimbia.
Alipatwa na uchungu sana katika moyo wake, hakuweza kuyazuia machozi yake kabisa.
Sakina alifika hospitali kwa muda muafaka kabisa kwani akapata khabari kuwa Dorry amejifungua mtoto wa kiume.
Tabasamu likajaa kwenye sura yake huku akifikiria jina la haraka haraka la kumpa mjukuu wake huo.
Dorry alipopelekwa kwenye wodi ya wazazi ndipo waliporuhusiwa kwenda kumtazama huku Sakina akiwa na hamu ya kumuona mjukuu wake tu.
Na alipoingia kitendo cha kwanza kilikuwa ni kumshika mjukuu wake huyo.
Ila alipatwa na mshangao kuona mjukuu wake huyo kuwa mweupe sana na macho madogo utafikiri ni mtoto wa kichina yani kamavile kazaliwa na mzazi mwenye asili ya China.
Na alipoingia kitendo cha kwanza kilikuwa ni
kumshika mjukuu wake huyo.
Ila alipatwa na mshangao kuona mjukuu wake
huyo kuwa mweupe sana na macho madogo
utafikiri ni mtoto wa kichina yani kamavile kazaliwa
na mzazi mwenye asili ya China.
Sakina alimshika yule mtoto huku maswali mengi akijiuliza kwenye akili yake na kukosa jibu ila hakuweza kuhoji chochote ukizingatia pale ni hospitali.
Kisha baada ya muda kidogo akamrudisha mtoto mikononi mwa wengine.
Muda kidogo wakasogea Sabrina na mama yake pale kumsalimia Dorry.
Na badae wote kutakiwa kwani Dorry naye alipewa ruhusa ya kurudi nyumbani na hapakuwa na namna nyingine zaidi ya Dorry kuongozana na Sakina ili kuelekea nyumbani kwake kwani asingeweza kwenda kwao ukizingatia mama yake ambaye ndio angemuhudumia ndiye alikuwa mgonjwa.
Inaendeleaah
No comments: