MWANAMKE ANADUMU KWENYE MAHUSIANO AMA NDOA KWA KUANGALIA PENDO LA MWANAUME JUU YAKE


💯
Kama Mwanamke akibaini kile aliamini ama kukitarajia kimetoweka kama sio kuisha AUTOMATICALLY huanza harakati za kulivua PENDO kwa usalama wa MOYO wake😂
Wanawake ni wabinafsi Kweli kweliiii, wengi tunaamini WANAWAKE WANA UPENDO WA DHATI❤️ Ila haina maana ni vipofu wasiweze kuishi na Mwanaume kwa kutazama mienendo ya kile Mwanaume aliahidi wakati wanakutana, Wanaume wengi huishi na Wanawake Kwa MAZOEA kwa sababu Mwanamke kwa uhalisia ni wenye kusamehe kwa mdomo ila MOYONI nao ni bin adam maumivu huwapeleka mbali ki fikra, Mwanamke kama akisamehe kwa dhati hawezi kubadilika mienendo yake💯
Wanawake wengi ili kuponya jeraha zao pindi wanapokuwa wameumia HUJARIBISHA MAHUSIANO NJE YA MAHUSIANO/NDOA zao na kama wakifanikiwa kupona niamini hawawezi kurudi ndani ya mahusiano ama ndoa zao ki akili na moyo ila ki mwili📌
Utamuona Mwanamke akiwa nawe ila niamini MOYONI mwake amebeba mtu Mwingine kabisa na akili yake iko nje yako, Wanawake wanatabia ya kujivua pendo taratibu kama nyoka anayevua ngozi yake😂😂
Akiisha maliza yale aliamini yatamuumiza akiondoka kwako wallah HUTAAMINI KAMA NDIYO YULE ALIKUWA ANAKUNYWA SUMU JUU YAKO😂😂
Kama unampenda Mwanamke usijaribu kuumiza MOYO wake maana majibu ya hilo ni hatari kwako, Mapenzi yanabeba dhamana kubwa kuliko UNDUGU lakini Mapenzi hayo hayo ndiyo husababisha MAJANGA DUNIANI💯
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria 🔨
Image may contain: 4 people, people sitting and stripes




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.